UVCCM yasifu ujasiri wa Rais Samia kuongoza maridhiano nchini

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Na Bwanku Bwanku.

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesifu na kupongeza hatua madhubuti alizoanza kuzichukua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuliweka Taifa katika hali ya amani, umoja na mshikamano kupitia kuongoza maridhiano ya kisiasa nchini yenye lengo la kusisitiza Taifa kufanya siasa za kistaarabu na zenye tija kwa Taifa.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Taifa Ndugu Mohammed Ali (Kawaida) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Afisi Kuu ya UVCCM Zanzibar- Gymkana Jana Jumatano Januari 04, 2022.

Kawaida amesema maamuzi ya Rais Samia kusimamia maridhiano nchini yameonyesha mwelekeo chanya wa Serikali ya Dkt. Samia wa kuongoza Taifa letu kufikia ndoto za maendeleo endelevu ikiwa nchi yenye kusikilizana, yenye amani, utulivu na ustahimilivu wa hali ya juu huku Serikali ikilinda haki za watu wote bila upendeleo.

"Maridhiano ni mchakato unaohitaji muda wa kutosha katika kufikia malengo yake, hivyo hatua ya mabadiliko ya sheria na kanuni zinazoongoza Tume ya uchaguzi, sheria ya vyama vya siasa ili kuweza kufanya siasa za kistaarabu na kupata jawabu sahihi la Katiba kuendana na mazingira yetu litafikiwa bila shaka chini ya Mwenyekiti wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan." Alisema Kawaida.

Ndugu Kawaida pia, aliendelea kwa kuvipongeza vyama vyote vya siasa nchini vilivyoshiriki kwenye kila hatua ya maridhiano na kuendelea kusisitiza kwamba, CCM chini ya Dkt. Samia Suluhu itaendelea kuwa mlezi wa maridhiano haya nchini na kuwasisitiza Viongozi wa vyama vya upinzani kuendelea kutimiza wajibu wao ili kwa pamoja tuendelee kulinda amani na utulivu wa Taifa letu na asitokee kamwe mtu kutoka ndani ama Nje ya Nchi kuvuruga amani yetu.

Soma: Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan: Hadi sasa sijaona dalili yoyote ya utashi wa kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa nchini

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Vijana Taifa alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kueleza msimamo wa Umoja wa Vijana wa CCM kuhusu uamuzi wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kusimamia vyema maridhiano ya kisiasa nchini na hatua ya kutoa zuio la kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na mengine mengi kwenye uwanja wa siasa.
bwankubwanku1_1672899459492400.jpg

bwankubwanku1_1672899479559676.jpg

Tasnia ya BA. Chawacracy inakuwa kwa kasi.

Sasa hii ni habari, taarifa au ni kitu gani.
 
aisee yani sijui wana nini hawa.kuna watu wanawaelewa
hawa UVCCM mataira
 
Na Bwanku Bwanku.

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesifu na kupongeza hatua madhubuti alizoanza kuzichukua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuliweka Taifa katika hali ya amani, umoja na mshikamano kupitia kuongoza maridhiano ya kisiasa nchini yenye lengo la kusisitiza Taifa kufanya siasa za kistaarabu na zenye tija kwa Taifa.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Taifa Ndugu Mohammed Ali (Kawaida) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Afisi Kuu ya UVCCM Zanzibar- Gymkana Jana Jumatano Januari 04, 2022.

Kawaida amesema maamuzi ya Rais Samia kusimamia maridhiano nchini yameonyesha mwelekeo chanya wa Serikali ya Dkt. Samia wa kuongoza Taifa letu kufikia ndoto za maendeleo endelevu ikiwa nchi yenye kusikilizana, yenye amani, utulivu na ustahimilivu wa hali ya juu huku Serikali ikilinda haki za watu wote bila upendeleo.

"Maridhiano ni mchakato unaohitaji muda wa kutosha katika kufikia malengo yake, hivyo hatua ya mabadiliko ya sheria na kanuni zinazoongoza Tume ya uchaguzi, sheria ya vyama vya siasa ili kuweza kufanya siasa za kistaarabu na kupata jawabu sahihi la Katiba kuendana na mazingira yetu litafikiwa bila shaka chini ya Mwenyekiti wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan." Alisema Kawaida.

Ndugu Kawaida pia, aliendelea kwa kuvipongeza vyama vyote vya siasa nchini vilivyoshiriki kwenye kila hatua ya maridhiano na kuendelea kusisitiza kwamba, CCM chini ya Dkt. Samia Suluhu itaendelea kuwa mlezi wa maridhiano haya nchini na kuwasisitiza Viongozi wa vyama vya upinzani kuendelea kutimiza wajibu wao ili kwa pamoja tuendelee kulinda amani na utulivu wa Taifa letu na asitokee kamwe mtu kutoka ndani ama Nje ya Nchi kuvuruga amani yetu.

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Vijana Taifa alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kueleza msimamo wa Umoja wa Vijana wa CCM kuhusu uamuzi wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kusimamia vyema maridhiano ya kisiasa nchini na hatua ya kutoa zuio la kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na mengine mengi kwenye uwanja wa siasa.
View attachment 2470155
View attachment 2470156
View attachment 2470158
UVCCM hii hii ya wabeba mikoba au ipi?
 
Back
Top Bottom