UVCCM Yataka Udahili wa Vijana BBT Uongezeke

UVCCM Yataka Udahili wa Vijana BBT Uongezeke

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

UVCCM YATAKA UDAHILI WA VIJANA BBT UONGEZEKE

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Ndugu Mohammed Ali Mohammed (Kawaida) ametaka juhudi ziongezwe kuhakikisha idadi ya wanaodahiliwa katika mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) kila muhula inaongezeka.

Ndugu Kawaida ametoa kauli hiyo jijini Mbeya leo, Jumanne ya Aprili 18, 2023 alipotembelea Kituo cha mafunzo ya mradi wa BBT Uyole, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi katika Mikoa ya Dodoma, Mbeya, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha na Mtwara.

Amesema iwapo katika kila muhula wa miezi minne watakaochaguliwa ni 812, hadi kufikia mwaka 2030 mwisho wa mradi ni vijana 22,736 pekee ndiyo watakaokuwa wamenufaika ambao ni chini ya makusudio.

"Tunalenga kuwanufaisha vijana 3,000,000 lakini kwa idadi hii ya tunaodahili kwa muhula kuna haja ya kuongeza mbinu ili kwa muhula wadahiliwe wengi zaidi na tufikie lengo" - Ndugu Mohammed Kawaida
 

Attachments

Back
Top Bottom