Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita, Manjale Magambo, amewataka viongozi wa vyama vya upinzani kuacha malalamiko yanayohusiana na uandikishwaji wa wanafunzi wenye umri wa miaka 18 katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mbugani katika harambee ya ujenzi wa ofisi za chama hicho, tawi la Mbugani.
Pia soma: LGE2024 - Mwenyekiti wa UVCCM, Mohamed Kawaida amvaa Lema wa CHADEMA. Aitaka TAMISEMI iendelee kusajili wanafunzi kwenye daftari!
Manjale amesisitiza kuwa wanafunzi hao wanayo haki ya kisheria ya kuandikishwa na kwamba wale wanaoshindwa kuelewa utaratibu huo wanapaswa kuacha malalamiko na kuachia zoezi hilo lifanyike kwa mujibu wa sheria.
Aidha, Manjale ameeleza kuwa vijana wenye uwezo wa kuongoza wanapaswa kupewa nafasi kuanzia ngazi za Serikali za Mitaa, vijiji, na vitongoji. Amesisitiza kuwa ni muhimu kuwawezesha vijana kushiriki kwenye uongozi ili kuleta maendeleo ndani ya jamii.