mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,126
- 5,068
Dar es Salaam. Madaktari wamebaini kuwa virusi vipya vya Uviko-19 vinaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.
Hata hivyo takwimu za mwisho zilizotolewa na Wizara ya Afya nchini Agosti 15, zilionyesha kuwa walengwa 207,391 wamepatiwa chanjo ya Uviko-19 mpaka kufikia Agosti 14 mwaka huu.
Takwimu hizo zinaonyesha wanaume wamechanjwa kwa asilimia 58.3 sawa na 121,002 huku wanawake waliochanjwa ni 86,389 sawa na asilimia 41.7.
Madaktari waliofanya utafiti huo kutoka Chuo Kikuu cha Miami nchini Marekani wameeleza kuwa athari hizo zinatokana na ukweli kwamba virusi hivyo vinaathiri zaidi mishipa ya damu hasa ile inayopeleka damu moja kwa moja kwenye uume.
Watafiti hao, wakitumia darubini maalumu ya kitabibu wamebaini kuwepo kwa virusi vya Uviko-19 kwenye vinasaba maalumu vilivyochukuliwa kwa wagonjwa wawili ambao wanadaiwa kupoteza nguvu za kiume baada ya kupata maambukizi, waliyoyapata kati ya miezi sita na minane iliyopita.
Alipoulizwa kuhusu utafiti huo, Daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Elisha Osati amesema kuna ukweli kuhusu utafiti kwani Uviko-19 unaathiri vijana.
“Sitaki kuwatisha watu lakini ukweli ni kwamba unaweza hata kupoteza nguvu na mbegu za kiume kwa kuwa na Uviko-19 na kushambulia mapafu, figo na mishipa ya damu inashambulia pia via vya uzazi kwa wanaume inaweza kuleta madhara na kuzuia utengenezwaji wa mbegu za kiume na kwa wanawake pia.
“Vijana wengi wasibweteke huu ugonjwa ukiupata unaweza kuwaletea madhara kwa namna moja ama nyingine hatutaki kuwa na watu ambao hawawezi kuzaa na kupata watoto au kujenga taifa waende kupata chanjo mimi nakaa na wagonjwa ICU na baadaye wanakuwa wanahudhuria kliniki mrejesho tunaupata matokeo yake si mazuri,” amesema Dk Osati ambaye pia ni mtaalamu na mshauri wa masuala ya afya.
Daktari bingwa wa fiziolojia ya homoni na mazoezi kutoka Chuo Kikuu cha Afya Kishiriki cha Sayansi Muhimbili (MUHAS), Fredrick Mashili amesema kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya damu na nguvu za kiume.
“Ili nguvu za kiume zitokee damu inahusika na ndiyo kisababishi ndiyo maana mtu akiwa na shida katika mishipa ya damu au ugonjwa utakaoathiri mishipa ya damu lazima tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hutokea,” amesema.
Amesema damu na ubongo vinahusika katika tendo hilo lakini kikubwa ni vichocheo ‘homoni ya kiume’ ambapo kiwango cha homoni hii huongezeka zaidi nyakati za asubuhi.
“Kwenye uume kuna mishipa mikubwa ya damu, halafu wenyewe upo kama sponji hivyo mwanaume anavyojengeka kisaikojia kuwa tayari kwa lile tendo damu hutoka katika maeneo mengine ya mwili na kushuka chini damu ikienda katika uume hushibisha ile mishipa inatanuka, uume hurefuka na kunenepa na ndipo nguvu za kiume hutokea,” amesema Dk Mashili
Chanzo: Mwananchi
---------------
Wakuu, shtukeni mkachanje, Uviko-19 usiwaoetee ukosefu wa nguvu za kiume na kutokuwa na uwezo wa kutungisha ujauzito!