Uvinza: Halmashauri yachukua hatua kupitia video iliyosambaa lakini yashangazwa na aliyechukua video ikidai ameleta taharuki

Uvinza: Halmashauri yachukua hatua kupitia video iliyosambaa lakini yashangazwa na aliyechukua video ikidai ameleta taharuki

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Halmashauri ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma imechukua hatua ya kumpumzisha daktari wa zamu ili kupisha uchunguzi baada video ya Mwanamke anaedaiwa kujifungua na kukosa huduma kwa zaidi ya saa moja katika Kituo cha Afya Kata ya Basanza kusambaa mtandaoni.

Halmashauri baada ya kufatilia ilibaini mteja huyo alifika zahanati ya Basanza Juni 09, 2024 akitokea maabara binafsi kwaajili ya kupata huduma zaidi lakini kabla ya kupatiwa huduma alijifungua.

Muhudumu wa zamu anayeishi umbali wa mita 5 kutoka kituo hicho baada ya kupata taarifa alifika wodini na kukuta mjamzito ameshajifungua mtoto wa kiume

Halmashauri ilimpumzisha kuendelea na majukumu yake kuanzia Juni 14 kupisha uchunguzi na endapo atabainika kuwa na makosa atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Pamoja na hayo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri, Fred Milanzi ametoa wito kwa umma kuwasilisha malalamiko kupitia mfumo uliowekwa ili zifanyiwe kazi na amesikitishwa na mwananchi aliyeingia wodi ya wazazi bila ridhaa na kuchukua video ya tukio hilo na kusambaza mitandao ya kijamii na kuleta taharuki kwa jamii.

Pia SOMA=> Kigoma: Mwanamke adaiwa kujifungua na kukosa huduma kwa zaidi ya saa moja katika Kituo cha Afya Kata ya Basanza
 

Attachments

Kuna zile sanduku za maoni zipo mahospitalini zimejaa vumbi na hazina dalili ya kufunguliwa kwenye baadhi ya zahanati.

Kwa ujumla angefata mifumo ya serikalini hilo jambo lisingeleta impact ya uwajibikaji kama njia aliyotumia..
 
Nitashangaa Mkurugenzi akiendelea kubaki ofisin bila mamlaka yake ya uteuzi Kumuwajibisha
 
Back
Top Bottom