Uvivu na uchafu ni mapacha ambao ukiwakumbatia utaishi maisha ya ovyo ovyo sana

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Binadamu anapaswa kuwa msafi, hii ni moja ya tofauti kati yetu na wanyama ingawa wote ni jamii ya mamalia. Sisi tunaoishi kwenye chumba kimoja ambacho ukifungua macho asubuhi unaangalia vyote unavyomiliki, inapaswa kujiongeza sana. Bila kujiongeza unakaribisha panya na mende ndani.

Unakuta mdada amepaka poda mjini, kucha zinawaka lakini nyumbani hakutandika kitanda na mvunguni mwa kitanda kuna vyombo vichafu. Akitafuta ndala akaoge anaona moja, kumbe moja aliipiga teke jana ikaenda kwenye mvungu wa kitanda. Akiinama aitafute anakutana na vumbi lililounda urafiki na tandabui.

Chumba ni kimoja lakini usipoweka chakula wazi na kukiwa kusafi panya na mende hawaingii. Ukisha pika jipe dakika za kula na kuosha vyombo. Chombo kunachobaki kinatakiwa kuwa sufuria ya ugali nayo ioshwe midimoni na ilowekwe kwa maji safi.

Huku kwetu unaweza kufungua dirisha ukutane na mfereji wa maji kutoka bafuni. Kwakweli ni uvivu tu wa kufikiri lakini kama ni nyumba ya kupangisha na mwenye nyumba analipwa kodi,, kwanini asinunue bomba la kistiri haya maji ya bafuni.

Kuna dada niliongea nae saloon wiki iliyopita, nilimuuliza hivi ni kwanini watu hawajipendi? Alinijibu wengi wanafanya kazi ngumu wakirudi nyumbani wamechoka. Usafi ni nature na ukiwa msafi hata kama umechoka utatenga saa moja la kurekebisha mazingira.

Kuna wengine wanailazinisha nature ya usafi iwaingie na to nawaingia kweli.
 
Aiseh yani unaenda nyumba ya mtu unaomba maji ya kunywa unasikia harufu ya sabuni, muda wa kula sahani linaletwa na mavi ya panya,
Kwani nilikula sikushika tonge hata moja nikaanza sema tumbo linanisokota kumbe nina langu rohoni.
 
Aisee bora awe mwanaume ila mdada kuwa mchafu inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom