Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 471
- 1,217
Kila mtu ana dhahabu maishani mwake inaweza kuwa kipaji, biashara, ndoa, kazi, au
ata rafiki lakini dhahabu nyingi haziji zikiwa zinang'aa.
Dhahabu asili huchimbwa ikiwa imefunikwa na tope, mchanga na mawe ambapo itahitaji kazi, subira, na utayari wa kuchafua mikono kuisafisha.
Shida ni kwamba wengi wetu tunataka matokeo bila mchakato, Tunapoiona fursa ikiwa na changamoto tunaiita mbaya kisha tunaitupa na kusahau kwamba uchafu si thamani bali Uchafu ni ganda tu.
Mifano ya karibu:
1.Biashara
Watu wengi wanaanza lakini wakikutana na hasara za kwanza au malalamiko ya wateja, wanafunga. Walikuwa na dhahabu lakini wamechoka kusafisha tope.
2.Vipaji
Unaweza kuimba, kuandika, au kucheza mpira. Lakini mazoezi ni magumu na hakuna anayekushangilia mwanzoni. Uvivu wa kufanya mazoezi na hakuna wa kukushangilia ndio unafanya wengi wazike vipaji vyao.
3.Mahusiano;
Ndoa au urafiki mzuri una changamoto, Ukikimbia kwa sababu ya ugomvi mmoja huenda umetupa dhahabu kwa sababu ya tope dogo.
#Malenga wa Kiha
#Mwanasayansi Kalivubha