Uvivu wa kutisha, uchawi (kulaguza), na vijana kuamini kwenye quick gain ni baadhi ya sababu zilizorudisha nyuma maendeleo ya Mkoa wa Kagera

Uvivu wa kutisha, uchawi (kulaguza), na vijana kuamini kwenye quick gain ni baadhi ya sababu zilizorudisha nyuma maendeleo ya Mkoa wa Kagera

the power

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
407
Reaction score
799
1. UTANGULIZI
Najua watani wangu wa Kagera, akina nshomile mtakuja juu na hawatapenda hili andiko, hasa kwa nini ninawaandama?. Jamani huu ni mwendelezo wa andiko langu la kwanza kuhusu kagera lisemalo "Mkoa uliong'aa (the shiny BK) leo umekuwa mkoa giza (the dark Bukoba) kwenye kila sekta ya maendeleo, ni kitu gani kimetokea Kagera mkowa wetu pendwa?"

2. KIINI CHA ANDIKO
Twende straight kwenye point, viko visababishi vingi vya kuwa na hali mbaya Kagera, nature ya watu wa Kagera (how they have recently been groomed) ni sababu ya jumla na hii ndio ilikuwa mada ya andiko langu la kwanza kwa mfano majivuno, dharau , ubishi, majigambo, ujuaji etc. Leo nataka tuangalia baadhi ya visababishi muhimu kwa wigo mpana; i) Uvivu wa kutisha, ii)Ulevi wa kutisha iii) Uchawi (kulaguza), iv)Vijana kuamini kwenye quick gain, v) ) Roho Mbaya yakutisha

i) Uvivu wa kutisha

Kwa sasa jamii ya Kagera imeingiwa na ugonjwa sugu wa uvivu wa kutisha tofauti na wazee wa zamani waliokuwa hard workers. Ukiacha kuzungukwa na ardhi nzuri, mifugo, ziwa , hali ya hewa safi, nguvu kazi ya kagera hasa vijana wamekuwa wavivu sana, akili ya wengi imedumaa kwa sasa, sorry to say that, tofauti na zamani ambapo vijana walijikita kenye kilimo, uvuvi, ushindani wa kielimu na biashara n.k vijana wa sasa hawataki kujishughulisha kwenye kazi ngumu, wao ni mipira, tungi na story za barabarani tu.

ii) Ulevi wa Kutisha
Simaanishi wazee wetu wa zamini wa watani wangu walikuwa si wanywaji, labda niseme walikuwa wanakunywa kuliko sisi ila walikuwa serious kwenye kazi na kuzalisha chakula na kutafuta hela na elimu, ndio maana pombe haikuwadhuru, ninawazee rafiki zangu zaidi ya 10 wana miaka zaidi ya 80-90 wako fiti mpaka leo mbali ya kupiga ulabu sana,sasa wamepunguza baada ya ulabu kuchakachuliwa. Tofauti na vijana wa sasa wanataka kulewa ila hawataki kuzalisha chakula na kutafuta pesa, wanaishia kuathirika kiafya na kiphyschologia. Huwezi kunywa pombe kali iliyochakachuliwa bila msosi ikakuacha salama.

Mbaya zaidi aina ya pombe ya zamani ilikuwa pure, mfano rubisi, enkonyagi (gongo-both pure-embadule na kaizi-regular),omunanasi zilikuwa pombe-chakula na hazikuchakachuliwa, leo wanachanganya na magamba ya mwarobaini kutengenza enkonyagi etc, Imagine kijana mwenye lishe duni akishindilia sumu hiyo kila siku kwa mwezi ,kwa mwaka, wengi wanaishia kuwa mazezeta.

iii) Uchawi (kulaguza)
Unaweza kukataa, unaweza husiamini lakini Kagera imeingiwa na wimbi la uchawi, sisemi uchawi haukuwepo ila kwa sasa uchawi ni occupation kama kada za kazi nyingine tena tofauti na zamani, kwa sasa the leading age ni vijana na si wazee; kweli umasikini huleta uchawi, familia nyingi zinaishia kurogana tu mchana na usiku.

Kama hufahamu katika aina za uchawi imara, uchawi sugu wa kagera ni uchawi wa kuleta madhara kwenye familia, kuleta ulemavu, kuleta mabalaa; wataalamu wa mambo ya giza humu ndani watatusaidia. Wao wanaita enzigu (kama nimekosea wahaya mtanisaidia hapo), ukizubaa hawakurogi wewe tu , wanaroga wewe na familia yako na ukoo wako na kizazi chako kitakachokuja (mnarithishwa urogwaji kizazi na kizazi). Yaani ni balaa. Kumbuka ukishafika hatua hii lini utafikilia kufanya kazi, kufanya maendeleo, hicho ndicho kizazi cha sasa cha baadhi ya wana-Kagera

iv) Vijana kuamini kwenye quick gain
Hii ni sumu iliyoingia kwenye mentality ya vijana wengi, nafikiri sio tu Mkoa wa Kagera na mikoa mingi Tanzania, wanoana kulima kunachukua muda mrefu, elimu itachukua muda mrefu ndio maana kwa sasa limeingia wimbi la vijana kuamua kuby-pass form 5 na 6 na university, wanachukua short cut ya VETA, certificate na diploma colleges eti ili wapate kazi na pesa mapema, kumbe wanaruin their entire future life. Kundi kubwa la vijana hawa wamechukulia bodaboda kama a quick life solution, kila familia kagera asilimia 50 mpaka 60 ya vijana wao wanaendesha bodaboda, hivi unafikiri mkoa utapata maendeleo makubwa hapa, lini wataongelea Sustaibale Development goals-2025, mtu wa bodaboda?

v) Roho Mbaya yankutisha
Hili nililiongea kwa mapana kwenye andiko langu lililopita . Familia za zamani walikuwa na wivu wa maendeleo, ushindani ulikuwa ni wa maendeleo familia na familia, kijiji kwa kijiji, kata kwa kata, wilaya kwa wilaya ,kushindana kuzidiana kielimu, kibiashara, kwenye kuzalisha chakula na kahawa n.k. Kwa sasa ushindani umelenga kudidimiza familia nyingine hisipate maendeleo, hisisonge mbele,kuwekeana vikwazo, hata kuzibiana nafasi za maendeleo.

Niliwapa mfano wa namna Kagasheki,aliyekuwa mbunge wa BK mjini alivyosigana na meya wa Jiji wa wakati huo wakawa radhi fedha za maendeleo ya miundo mbinu za world Bank zirudi ili tu mmoja kati yao hasionekane kaleta maendeleo (Kagera was turned victims of political personal /individual hatrage). Narudia Kagera imeingiwa na roho mbaya ,shetani anakaa chini. Sasa roho mbaya imeingia ngazi ya kifamilia koo kwa koo, dada kwa kaka, hata wazazi kwa watoto utashangaa.

3. HITIMISHO
Hizi ni baadhi tu ya sababu zinazorudisha nyuma maendeleo ya Kagera. Andiko lingine litahusu nini kifanyike. Uzuri mkoa wa Kagera unaeconomic opportunities nyingi sana, most importantly unawasomi wengi wa zamani, maprofessor, wachumi, walimu, madiaspora wa kutosha wametapakaa dunia nzima mpaka unajiuliza inakuwaje wanashindwa kusaidia au kuleta maendeleo kwenye mkoa wao. Ila tusiwalaumu sana, ni nani angependa kuwekeza kwenye mkoa wenye tabia mbaya, tabia mbovu tajwa hapo juu 1-5. Ila wahenga walisema nyumbani ni nyumbani. Andiko lingine litajikita kwenye suluhihisho la nini kifanyike.

Poleni sana watani wangu wa Kagera, najua nitakuwa nimewakwaza ila kama wewe unahifahamu Kagera ya sasa utakubaliana kabisa na points na maelezo tajwa. nyie wenyewe mna msemo wenu unaosema; "omukaikulu we nshoni, bakamzika nalola" yaani bibi mwenye aibu, badala ya kusema sijafa, akawa na aibu kutamka, familia wakamzika wakizani amekufa kumbe angali hai" .Sasa ni bora kusema hamjafa ili msijekushtuka mnazikwa mkiwa hai(mnahangamia ) bila sababu.
 
Ushirikina kwa mkoa wa Kagera umeanza hivi karibuni lakini wameifunika hadi ile mikoa vinara wa ushirikina wako juu sana kwa sasa
 
Uvivu na kukaa barabarani kuhesabu magari ni jadi ya vijana wa Kagera Sasa na wazee wameiga ,wakimaliza huko ni kuanza kuamini ndugu yao aliyepo nje na mkoa wao ana hela basi ni mwendo wa simu kila muda kuomba hela
Kweli kabisa, mambo ya kuanza kusifia watu wengine. Ila hilo la utegemezi uliokubuhu ni ishu.ilitakiwa iwe sehemu ya visababishi
 
Ushirikina kwa mkoa wa Kagera umeanza hivi karibuni lakini wameifunika hadi ile mikoa vinara wa ushirikina wako juu sana kwa sasa
Na hii ni hatari zamani ilikuwa ni kwa kificho tena vibibi vichache sana. Leo hii husishangae familia nzima, inakuwa ni group witchcraft in mission,
 
Hizo sababu hazina mashiko,kumbuka kuwa Kagera ni moja ya Mikoa ya mwanzo kabisa Tanzania watu wake kupata elimu kama ilivyo Kilimanjaro bahati ya Mkoa wa Kilimanjaro wao walipata hiyo elimu bado pia ni wafanyabiashara.so,tatizo ni kuwa hao watu baada ya kupata hizo elimu hawarudi ku invest kwenye Mkoa wao tofauti-ni kama ilivyo USA na nchi za kiafrika-waafrika wengi wanakimbilka USA wanatumia maarifa yao katika kukuza maendeleo ya USA na kuacha nchini kwako.
 
Hata hivyo takwimu za NBS zinaonesha ukanda wote wa ziwa ukiondoa Mkoa wa Mara na ile ya Mikoa ya Wasukuma Kagera, Geita,Shinyanga,Simiyu na Mwanza na ndugu zao Tabora kuna umaskini Mkubwa.
 
Hizo sababu hazina mashiko,kumbuka kuwa Kagera ni moja ya Mikoa ya mwanzo kabisa Tanzania watu wake kupata elimu kama ilivyo Kilimanjaro bahati ya Mkoa wa Kilimanjaro wao walipata hiyo elimu bado pia ni wafanyabiashara.so,tatizo ni kuwa hao watu baada ya kupata hizo elimu hawarudi ku invest kwenye Mkoa wao tofauti-ni kama ilivyo USA na nchi za kiafrika-waafrika wengi wanakimbilka USA wanatumia maarifa yao katika kukuza maendeleo ya USA na kuacha nchini kwako.
Hiyo ni sababu subjectives, hao waliosoma walijitahidi wenyewe na kuvumilia mazingira magumu, huwezi ukawalazimisha kuinvest kwao. Kama hujamalizia paragraph ya mwisho nimetoa hint ni vitu gani vifanyike ili turudishe Kagera ya zamani (to bring the Great Kagera again). Ila huwezi utaatribute jugudi za wengine kwa kudumaa kwa mkoa. Sababu lazima iwe inahuhusiano wa moja kwa moja na tatizo. Hapa tumetaja matatizo ya moja kwa moja yaliyosababisha umasikini wa kutisha mkoa wa Kagera.

Mfano huwezi kusema Nyerere aliona Wahaya wana akili sana , akawa na hofu ndio maana akawatenga na maendeleo hiyo ni sababu hafifu na mtu mwenye akili ya kutafakuli au luanalysie direct and indirect attributable factors of any independent variables utajua kwamba hizi sababu hazina mashiko.Na hata ukija kwenye solution based ukitumia hizi sababu hutapata solution. Tuongelee direct conrtibuting factors.
 
Ujue Kagera ime athiriwa na majanga mengi SANAA kuliko mkoa wowote...

1. Vita vya Kagera wahanga na waathiriwa wakuu ni KAGERA

2.UKIMWI yaan ukimwi ulianziaga KAGERA watu walipukutika Kama njuguu..yaan NYEGERA NYEGERA ZILIKUA NYINGI...NYEGERA WAITU

3.kuzama kwa MV BUKOBA wanakagera walipoteza watu wengi takribani 1000 janga lingine hili..

4. Tetemeko la BUKOBA liliangusha majumba, miundombinu,vifo yaan uchumi na miundombinu mingi Sanaa ilianza kujengwa upya..

Apart ya uliyo ya elezea....Kwaio Kagera Imepitia majanga mengi SANAA kuliko mkoa wowote TZ

Wasalaam
😊😊
 
Ujue Kagera ime athiriwa na majanga mengi SANAA kuliko mkoa wowote...

1. Vita vya Kagera wahanga na waathiriwa wakuu ni KAGERA

2.UKIMWI yaan ukimwi ulianziaga KAGERA watu walipukutika Kama njuguu..yaan NYEGERA NYEGERA ZILIKUA NYINGI...NYEGERA WAITU

3.kuzama kwa MV BUKOBA wanakagera walipoteza watu wengi takribani 1000 janga lingine hili..

4. Tetemeko la BUKOBA liliangusha majumba, miundombinu,vifo yaan uchumi na miundombinu mingi Sanaa ilianza kujengwa upya..

Apart ya uliyo ya elezea....Kwaio Kagera Imepitia majanga mengi SANAA kuliko mkoa wowote TZ

Wasalaam
😊😊
Hizi naweza kusema ni escape goat reasons. Yes ni reasons but their contribution are minor to compare with the downfall speed toward impervished poverty we are currently witnessing in Kagera. Ni bora tu-accept kuna misingi mikubwa ya maendeleo tumeikosea
 
Mtoa andiko kaeleweka sana na yuko sahihi kwa ukubwa ila kwa namna alivyoelezea sisi wa-cuba naye pia ni m-kagera,hvyo basi naamini solution itapatika,kama ambavyo huwa sipendi kudharau maoni na mawazo ya mtu ila naamini kwamba tabia nyingi alizotaja pia zipo mikoa mingi katika nchi hii,nahisi kuna tatizo au matatizo mengine yanayopelekea kuporomoka kwa uchumi ndani ya huo mkoa.asanteni
 
Back
Top Bottom