Uvuguvugu wa siasa za upinzani nchini umewasababishia mawenge katika kila wanalofanya

Uvuguvugu wa siasa za upinzani nchini umewasababishia mawenge katika kila wanalofanya

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Hawaaminiki tena, hawaeleweki kabisa kwa wananchi, wamekosa na kupoteza uelekeo, ushawishi wa kisera na mipango mikakati kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa. Kanuni, sheria na katiba viko wazi kabisa kuhusu uchaguzi huu, lakini wanalilia hisani na kutegemea huruma za wananchi.

Walianza kusita na kupuuzia zoezi la kujiandikisha kwajili ya kupiga kura kwajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Wakaendelea vivyo hivyo na mzaha kwenye zoezi la uteuzi ndani ya vyama vyao na sasa kwenye uchukuaji fomu wako na hali hiyo hiyo. Kabla ya hapo upinzan ulikua zigzaga wengine wanadai hawatashiriki uchaguzi na wengine wanadai watashiriki chaguzi zote. Kwasasa wanakosea kila kitu, na hawana uhakika na chochote.

Uchaguzi ni mchakato wenye maandalizi ya muda mrefu sana, muhumu na ghali mno. Ni Lazima wadau kujipanga kwa hali na mali, na kujiandaa vyema na kikamilifu ikiwa kweli wana dhamira na nia ya kushiriki uchaguzi huo.

Natawatakia maandalizi mema vyama ambavyo viko serious hususani chama tawala na wagombea wao, kwenye mchakato na hatua hizi za mwisho kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa na vijijini Nov 27, 2024.

Wengine, hekima na busara ziwaelekeze kujiandaa na chaguzi zingine huko mbele. Kwa uchaguzi huu wa serikali za mitaa na vijiji, muda sio rafiki tena na hakuna muujiza.🐒

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom