Abdull Kazi
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 337
- 296
SRINAGAR:
NASIRA Akhter, mwanamke Mvumbuzi wa Kashmiri,mwaka huu alikuwa ni miongoni mwa wanawake 29, walionyakua tuzo ya kifahari ya Nari Shakti Puraskar, iliyokabidhiwa wakati wa kilele cha siku ya wanawake duniani na Rais wa India Ram Nath Kovind.
Rais Ram Nath Kovind alimkabidhi Akhter tuzo hiyo ya kifahari ya Nari Shakti Puraska kutokana na uvumbuzi wake kutengeneza mfumo wa dawa za asili(Mitishamba),ambayo husaidia kuharibu vitu vyenye asili ya Plastiki(Nailoni) hali inayosaidia kuhifadhi mazingira
Akiwa anatokea maeneo ya Kulgam, Akhter alitengeneza dawa hiyo ya -mimea inayobadilisha nailoni kuwa majivu, na hivyo kufanya nailoni iweze kuoza.
Akisimulia historia yake Akhter anasema alifika mpaka darasa la 12 kabla ya kuamua kuacha shule na kujishughulisha na tiba za mimea na aina nyingine ya Ubunifu.
Kwa sasa Akhter ni mama wa mtoto mmoja wa kike na wanaishi katika Kijiji cha Kanipora Kulgam baada ya kumpoteza mume wake aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa Saratani.
Akhter aliyezaliwa mwaka 1977 anasema amekuwa akifanyia kazi utafiti huo wa asili kuanzia mwaka 1999 na hatimaye alikuja kufanikiwa mwaka 2008 baada ya kazi ngumu ya muda mrefu.
Anasema kimiminika cha mimea alichokigundua husaidia kuharibu nailoni (vitu vya plastiki) bila kuathiri mazingira.
Katika onyesho la moja kwa moja Mwaka 2015 lililofanyika katika chuo kikuu cha Kashmir Nasia, Akhter alipaka kimiminika kwenye nailoni na kuiwasha na baada ya kuungua, majivu yalionekana
kuharibika.
“Kwa Sasa ameingia makubaliano na kampuni ambayo imetia saini kifungu cha kutofichua taarifa yoyote kuhusu muundo wa ugunduzi wake huo ,” Sayeed Nadeem kutoka Mtandao wa uvumbuzi wa mashinani wa Grassroots innovations Augmentation Network, alisema. “
Aliongeza kuwa Kibali chake kipo katika mchakato na atakipata hivi karibuni na fomula yake inafanyiwa utafiti.”
Alisema utafiti uliofanywa hadi sasa kuhusu fomula hiyo unatia moyo.
“Kimsingi anazungumza juu ya ‘kuozesha nailoni (plastiki)’. Anadai kuwa inapochomwa,
nailoni hubadilika na kuwa majivu yenye moshi kidogo na bila kuchafua mazingira,” alisema.
Rais alitoa jumla ya tuzo 28 - 14 kwa kila mwaka kwa mwaka 2020 na 2021 kwa wanawake ikiwa ni sehemu ya
kutambua kazi yao ya kipekee katika jitihada za kuwawezesha wanawake, haswa walio hatarini na waliotengwa, ikijumuisha wanawake wawili kutoka Jammu na Kashmir.
Pia Rais wa India, Ram Nath Kovind alitoa tuzo ya Nari Shakti Puraskar kwa mwanaharakati wa masuala ya kijamii wa Kashmir, Sandhua Dhar mnamo Machi 8, 2022.
Sandhua Dhar anaendesha shirika lisilo la kiserikali la watu wenye ulemavu maalum huko Jammu, Huku mwenyewe akiwa ni mtu mwenye mahitaji maalamu (ulemavu).
Mwingine aliyepewa tuzo hiyo ni Sandhya Dhar, mfanyakazi wa ustawi,ambaye alipokea tuzo hiyo akiwa kwenye magurudumu.
Alitunukiwa tuzo hiyo kwa mchango wake na kujitolea kuelezea haki za watu wenye ulemavu (divyangjan right).
“Mwaka 2015 alianzisha Taasisi ya elimu Jammu ambayo inaendesha madarasa ya watu wenye ulemavu na watoto wasio na uwezo,” Rashtrapati Bhawan alisema.
Kwa upande wake Mwanaharakati wa haki za walemavu Sandhya ambaye nae anaongoza NGO,Pia ameathiriwa na ugonjwa wa kupooza kwa ubongo.
Nari Shakti Puraskar,ni tuzo ya heshima inayotolewa Wizara ya Maendeleo ya
Wanawake na Watoto kwa kutambua michango ya kipekee iliyotolewa na watu binafsi na
taasisi, na kusherehekea wanawake kama waleta mabadiliko na wachochea mabadiliko
chanya katika jamii.
Waziri Mkuu Narendra Modi aliwapongeza wanawake ambao walitunukiwa kwa michango
yao huko Jammu, LG Manoj Sinha pia aliwapongeza wanawake wawili kwa tuzo hiyo.