Mbege umelewa?! Point yako ni kuwasema maboss wa TANESCO, Kila mtu anakerwa na kukatika umeme.Mimi sio mfanyakazi wa TANESCO, nafikiri katika hali tulivu.Ninavyoifahamu jiografia ya Tanzania kusema ukweli tunawalaumu bure watu hawa! HEPs zetu ni ndogo, miundo mbinu ni chakavu, usambazaji wa Kila siku kwa wateja wapya, kubadilisha nguzo, nguzo kuanguka, maji kupungua, transformer kuungua kwa sababu tumeiba mafuta(coolant) na mengine mengi.Umeme sio nyumba ya miti ambayo mtu anaweza kuendelea na ujenzi wakati anaishi ndani! Inapotokea hitilafu,matengenezo, kusambaza ni lazima umeme ukatwe.Let's be considerate and stop blaming the guys who are actually overworked!