September 13, 2017
Kisumu, Kenya
Vurugu Kisumu baada ya vijana kutaka kuvamia mkutano wa kina mama
Kumetokea ghasia katika mji wa Kisumu, Kenya baada ya wakaazi wa mji huo kusoma habari iliyoandikwa na mtu mmoja katika mtandao wa facebook. Habari hiyo ilikuwa inadai katika mkutano wa kina mama wa Nyanza Women of Faith Network ulioandaliwa na Inter-Religious Council of Kenya waliokusanyika katika ukumbi wa hoteli ya Jumuia mjini Kisumu toka kaunti mbalimbali nchini Kenya walikuwa na ''njama kubwa ya kisiasa''.
Njama hiyo ni ''kuwa'' kina mama hao walikuwa wanauza vitambulisho vyao vya kupigia kura na vya watu wengine ambavyo zingetumika katika marudio ya uchaguzi wa Rais hapo Oktoba 17, 2017 utakao wapambanisha Muungano wa NASA kupitia mgombea Raila Amolo Odinga na Uhuru Kenyatta mgombea kupitia JUBILEE.
Hivyo vijana baada ya kuona habari hiyo ktk mtandao wa facebook walikusanyika na kuvamia hoteli hiyo kuwafurusha kina mama hao. Lakini habari za uhakika ni kuwa madai hayo ktk facebook yalikuwa uvumi usio kuwa na chembe ya ukweli.
Polisi ilibidi kuingilia kati kuzima vurugu hizo zilizosababishwa na vijana wa Kisumu, kwa askari kupiga risasi za moto angani kuwatawanya vijana hao waliotaka kuwaadhibu zaidi ya kina mama 200 na kuharibu mali za hoteli ya Jumuia iliyotumiwa na mkutano wa kina mama hao. Taharuki hiyo iliendelea kwa masaa kadhaa na kina mama ilibidi kujifungia ndani huku vijana wakitaka kuichoma moto hoteli hiyo.
Source: KTN News Kenya