Uvumi ktk Facebook wazua vurugu Kisumu

Uvumi ktk Facebook wazua vurugu Kisumu

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
September 13, 2017
Kisumu, Kenya

Vurugu Kisumu baada ya vijana kutaka kuvamia mkutano wa kina mama
Kumetokea ghasia katika mji wa Kisumu, Kenya baada ya wakaazi wa mji huo kusoma habari iliyoandikwa na mtu mmoja katika mtandao wa facebook. Habari hiyo ilikuwa inadai katika mkutano wa kina mama wa Nyanza Women of Faith Network ulioandaliwa na Inter-Religious Council of Kenya waliokusanyika katika ukumbi wa hoteli ya Jumuia mjini Kisumu toka kaunti mbalimbali nchini Kenya walikuwa na ''njama kubwa ya kisiasa''.

Njama hiyo ni ''kuwa'' kina mama hao walikuwa wanauza vitambulisho vyao vya kupigia kura na vya watu wengine ambavyo zingetumika katika marudio ya uchaguzi wa Rais hapo Oktoba 17, 2017 utakao wapambanisha Muungano wa NASA kupitia mgombea Raila Amolo Odinga na Uhuru Kenyatta mgombea kupitia JUBILEE.

Hivyo vijana baada ya kuona habari hiyo ktk mtandao wa facebook walikusanyika na kuvamia hoteli hiyo kuwafurusha kina mama hao. Lakini habari za uhakika ni kuwa madai hayo ktk facebook yalikuwa uvumi usio kuwa na chembe ya ukweli.

Polisi ilibidi kuingilia kati kuzima vurugu hizo zilizosababishwa na vijana wa Kisumu, kwa askari kupiga risasi za moto angani kuwatawanya vijana hao waliotaka kuwaadhibu zaidi ya kina mama 200 na kuharibu mali za hoteli ya Jumuia iliyotumiwa na mkutano wa kina mama hao. Taharuki hiyo iliendelea kwa masaa kadhaa na kina mama ilibidi kujifungia ndani huku vijana wakitaka kuichoma moto hoteli hiyo.

Source: KTN News Kenya
 
Hapo ndipo ninapowapa salute wakenya, hamtaki utani kwenye mambo muhimu ya kitaifa, hongereni sana
 
Hapa bongo kina mama ndo wanatusababishia madhira kwa kudanganywa na madera,khanga na vilemba,mjue kina mama tunawaheshimu sana ila itikadi zenu sometimes mnatia hasira na kuboa[emoji41] [emoji41] [emoji41]
 
Hapo ndipo ninapowapa salute wakenya, hamtaki utani kwenye mambo muhimu ya kitaifa, hongereni sana
Hiyo salute yako eka chini! Mimi ni mkenya lakini hao unaowasalute ni wakenya wajinga sana! Wanavamia mkutano wa kina mama bila hata ya kudhibitisha fununu walizopata? Afu wanawapiga mama zao mateke ya tumbo na kupora handbag zao! Kisha wanaonesha watu kadi moja ya Jubilee kuonesha uhalifu ulokuwa unaendelea kwenye semina. Ni hatia sasa kwa mwanamke wa Nyanza kuwa mwanachama wa Jubilee? Ujinga umekita sana mizizi huko Kisumu!
 
Naona vigilante wa NASA wanahofu kubwa ya kushindwa tena. Sasa serikali ya JUBILEE imepata sababu ya kupeleka majeshi Nyanza na katika maeneo yote yaliyo ngome ya NASA nchini Kenya.
 
Back
Top Bottom