Uvumi/Tetesi: Mtoto wa Kikwete (8) kugombea Uenyekiti Chipukizi?

Status
Not open for further replies.

Hata uchaguzi ukiwa huru, watamchagua. Tumezoea mno kunyenyekea wale tunaoona wametuzidi. Inabidi tubadilike kama tunataka mabadiliko. Kutegemea mtu anayefaidika na hali iliyopo ndiyo alete mabadiliko ni kuota ndoto za Ali Nacha!

Amandla......
 
Mie nasubiri Mbwa wa Kikwete au Paka au house girl, ALETWE KUGOMBEA.

Amini usiamini, hiyo ASILIMIA 70 itamchagua.

Halafu kesho watakuwa wanalalamika "POLISI WANATUUWA".

Yes, uwa tu, piga risasi, nyang'anya mashamba, ongeza foleni za magari, uza rasilimali za taifa kwa bei chee, kula posho mbili, fisadi BoT, uza/iba mashirika ya uma hadi hii asilimia 70 iishe. Labda hawa asilimia 30 wakiwa na wageni walioamua kukaa Tanzania ndiyo watakuja kufanya mabadiliko.

Na bado Mjukuu wa Kikwete akizaliwa hata kama ni mwakani, anapewa CHEO.
 
Wana groom...baada 25yrs anaomba ridhaa ya wananchi atuongoze...sifa mwnyt chipukizi taifa....wapi mwnkt wa zamani chipukizi.......siku hizi mkuu wa wilaya moja hv!!
 
Hata uchaguzi ukiwa huru, watamchagua. Tumezoea mno kunyenyekea wale tunaoona wametuzidi. Inabidi tubadilike kama tunataka mabadiliko. Kutegemea mtu anayefaidika na hali iliyopo ndiyo alete mabadiliko ni kuota ndoto za Ali Nacha!

Amandla......


Usiseme mambo kiujumla jumla eti hata uchaguzi ukiwa huru watamchagua.Wana CUF wakikusikia hapa watakushukia.
Hawa watu ni masikini,wana njaa.Na mbaya zaidi hawana elimu.Ndiyo mana ukienda na kampeni ya kugawa pilau na kanga,utapita.Huyu dogo anatumia jina la baba yake na atapita kwa njaa na ujinga wa makabwela unaosababishwa na serikali inayoongozwa na baba yake.
 
Chipukizi nao wana uongozi? Mpaka ngazi ya taifa? Umeanza lini mfumo huu?
 
Mtoto wa miaka nane ,pesa ya takrima anapata wapi? nahisi kwa baba au mama.Jamani historia itakuja kutuukumu vizazi hadi vizazi,wanaona raha wote kuwa katika nafasi za juu- ahaa tuachiani na sisi makabwela,tupeleke watoto wetu wakagombee.
 
Takrima ni rushwa,kama kweli unaipenda nji hii ungetupea taarifa ya jinsi ulivyo toa taarifa pccb badala kuleta majungu hapa
Hv unadhani hii itajenga?
 
Habari za udaku hizi!

Miaka nane yuko la kwanza au la pili anatakiwa shuleni anagombea nini? does not make sense!

Wanaomchagua katoto hako ndio wasio na akili hata kidogo

Kama itakuwa kweli basi this the end of CCM nahisi ni udaku so far ! lets wait and see.
 

kama amevalishwa joho alivyomaliza vidudu unategemea akiwa darasa la pili ataacha kufikiria uenyekiti wa taifa.
bongo iko juuuu wewe......
 
kama amevalishwa joho alivyomaliza vidudu unategemea akiwa darasa la pili ataacha kufikiria uenyekiti wa taifa.
bongo iko juuuu wewe......

Kitila Mkumbo kamaliza yote, "Wameitana vichaa, ila hadi leo bado ni MAWAZIRI".

Lolote likitokea halinishangazi. Hata Salma Kikwete akiwa PM, nitaendelea na shughuli kama hakikutokea kitu. Kuleta fujo za Cocacola pale inapunguliwa na baadaye unakaa kimya, unakuwa ni wale asilimia 70.
 
hebu wawarudishie watoto umishumta , chipukizi gani hawa ... usanii mtupu! angalau sisi enzi zetu za chipukizi tulikuwa tunacheza gwaride kule Mkwakwani na mwalimu Mandia
 
Kama wapiga kura wote ni watoto wa vigogo unaweza kuwa na wasiwasi,mwanao kama ana uwezo mwambie agombee wakulima wenzake watamchagua kama wakiona anafaa,kuwa mkulima ama mtoto wa kigogo hakumpi haki au kumuondolea haki aliyonayo katiak katiba ya nchi hii.ni vyema kukosoa lakini si vyema kuchukia kiasi cha kuchukia hata haki za watu kwa kigezo cha wadhifa ama kipato
 
Sizani kama wanaweza kupata nafasi ya kurisishana kwakuwa mkubwa mwenyewe yuko yuko tunasubiri ajibu mapigo mpaka leo kimya sasa kwa zama hizi hatuwahitaji itabidi tuweke mamluki ili kuvuruga ndoto zao wanatupotezea timing tu
 
Kwani mwenyekiti wa chipukizi ana impact gani kwa taifa? Na hata akigombea hako kacheo kwani anakuwa amevunja sheria au maadili au utaratibu upi? Hao wasiotaka apate hicho cheo wasimchague, basi!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…