uvumilivu...

uvumilivu wa kweli au wa kinafiki? kuna uvumilivu huku mtu anasema kwa chinichin au wa kutakatu kuonekana
boss kamwe usiwe wa kinafiki wapaswa uwe wa kweli.
 
Last edited by a moderator:

ningekuwa na moyo au roho kama ya kwako ningefurahi sana, ila mimi uvumilivu zero kabisa kila nikijatahidi nashindwa
sijuhi nifanyaje?
 
Hongera gfsonwin maneno yameniishia.

 
ningekuwa na moyo au roho kama ya kwako ningefurahi sana, ila mimi uvumilivu zero kabisa kila nikijatahidi nashindwa
sijuhi nifanyaje?
Nakshi ukitaka kuwa mvumilivu usiwe kwanza msemaji sana,msikilizaji wa ushuhuda wa wenzio hasa kwenye maamuzi yakushindwa, usiwe mtu wa kuchukia na kunyooshe kidole mwenzio ila mara zote jiweke wewe kama ndiye sababisho inaumiza kweli hasa pale inapokuwa wewe siyo sababu lakini huwa najiamnisha tu ili niweze kupata amani yangu na kupata suluhu ya swala lenyewe. hii ni tabia yangu hata kama nekosewa na mtu baki huwa nafanya hivyo.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin na sister,uvumilivu ni matokeo ya upendo,lakini kuna uvumilivu na maradhi ya uvumilivu(kihisia).Hili la maradhi sio matokeo ya upendo ni matokeo ya njaa ya kupendwa na kutojiamini.Yapo mambo yanayovumilika kibinadamu lakini yapo yasiyovumilika.Ufujaji kwa mfano,una madhara kihisia na kimwili,na matokeo yake ni kifo kwa anaefujwa.Mfujaji ni kazi sana kubadilika na ni kazi zaidi kuishi nae.Ukimkuta mtu anaishi na mfujaji haujui upendo na hajiamini.Upendo ni pamoja na kujipenda na kuwapenda wengine.Mtu anapokua na tabia za hatari kama ufujaji ni wa kuepukwa,sisemi umchukie,kumuepuka ni kuepuka kuwa kama kuwa nae kindoa n.k,lakini unampenda bado kama mwanadam.Unapovunja uhusiano na mtu wa aina hii haina maana unamchukia,bali unamthamini na unajithamini pia..Unaepusha kudhurika na kumsababishia matatizo.Huo ni upendo,uvumilivu utaeleweka kama mtu ataujua upendo kwani uvumilivu una mipaka yake!
 
Aisee kweli leo nimejifunza mengi..
Kiukweli uvumilivu unahitajika sana kwenye ndoa, vinginevyo haitadumu. Ila kama walivyosema baadhi wa watu, kuna vinavyovumilika na visivyovumilika. Hata biblia (sina uhakika na Quran) imeweka bayana mambo haya kwa wanandoa
 

Eiyer mdogo wangu panapo upendo wa kweli, na ukawepo uvumilivu wa dhati, nakushuhudia kwamba hutomuepuka bali utambadilisha. ilinichukua miaka 4-5 kuishi maisha ya tabu dhiki na majonzi na vilio lakini ikanichukua kitendo cha dakika moja ama mbili kubadilisha kila kitu kuwa historia.

ninaposema uvumilivu hauhesabu gharama namaanisha mdogo wangu, usikimbilie kwenye gharama bali angalia wewe amani yako waipata wapi? sikufichi Eiyer wewe ni mdogo wangu nakupenda sana na sipendi kukukuza kwa maneno haya ila naomba nikwambie kwa faida ya wengine pia.

niliangalia haya ili kuvumilia, nimeolewa nikiwa bikira skumjua mwanaume anafananaje, na nikasema sitatoka nje ya ndoa yangu na hiyo iko hivyo manake sitaki, sasa mume amenionyesha sura tofauti nifanyeje? je niondoke halafu nitaweza kuish pasi kutiwa? je kuna magonjwa anaweza kuniletea nikasema kama Mungu upo umeniona nilivyojitunza kama utaruhusu nife kwa UKIMWI sawa ni mapenzi yako ila nakuomba angalia uaminifu wangu kwako, hapo hapo nikawaza hivi huko nje si ndio naufuata ukimwi kabisa? ni bora aniletee kuliko tuleteane kwa wakati huo. nikawaza je kuvunja mwiko niliojiwekea nitakua na amani? Pia niliwaza nina watoto nimezaa, na kunammoja wa mashtuzi wa mr je huyu naye nikiondoka hatima yake itakuwa ni nini?

sikupenda kufanya maamuzi ya papara bali niliitafuta amani ya Mungu na kwa wakati wake alinijibu na sasa napeta kwenda mbinguni. Ni ngumu kama utaamua kwa akili zako na za marafiki ama watu wa karibu yako ila ni rahisi kama Mungu atakuamulia.
 
Last edited by a moderator:

ubarikiwe kwa kujifunza ma bro mito. sijui kwanini leo nimekumbuka past experiences zangu may be it was meant ili kuwafundisha wengine.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin,unaweza kuwa na uzoefu mkubwa zaidi ya huo lakini,trust me,hukustahili kupata mateso hayo!Labda nikuulize ulishawahi kumuuliza mumeo ni kitu gani kilimfanya afanye aliyofanya?Na kama ulimuuliza jibu lake lilikua nini?Kama hujamuuliza kwanini hujamuuliza hayo?Nijibu halafu mjadala uendelee vyema!
 

Hapo kwa red pamenigusa sana dada gfsonwin, hadi mwili umenisisimka! but in a positive way
 
Eiyer siku mume wangu alipomfukuza kimada wake mbele ya macho yangu na maneno aliyotamka mbele yangu kuhusu mimi na mbele ya wanangu wawili yalinifanya nikose nguvu ya kuuliza swali ama kujadili yaliyopita. kwa mwanaume kutamka maneno haya ' nilikuwa wapi kupoteza amani na furaha yangu siku zote hizi? na niwapi nitakapo mpata mwanamke mwenye utu wa kike kama wewe' akaapiga magoti mbele ya watoto na kulia akiomba samahani yalikauwa mambo magumu ambayo sitoweza kusahau maishani mwangu. kibaya zaid mwanangu ambaye kwa wakati huo alikuwa na miaka 4 alisema baba leo analia miguuni pa mama huku akicheka aisee niliumia kuliko maelezo hata uchungu wa kuzaa haukua hivyo. niliishia kumnyanyua kwenda naye chumbani alipokuwa amelala na yule kimada kumbembeleza asahau na kwamba sina kinyongo.

at that point eiyer you cant ask or say anything
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwa red pamenigusa sana dada gfsonwin, hadi mwili umenisisimka! but in a positive way

usijali mito that is now a hisotry to teach others
 
Last edited by a moderator:

gfsonwin, nakubaliana nawe juu ya thamani ya uvumilivu katika penzi lakini kwangu nahisi hapo kwenye bold cha mbele umeweka nyuma. Ni penzi mbele uvumilivu nyuma.
 
gfsonwin, nakubaliana nawe juu ya thamani ya uvumilivu katika penzi lakini kwangu nahisi hapo kwenye bold cha mbele umeweka nyuma. Ni penzi mbele uvumilivu nyuma.

my dearest Ngekewa yaani ukitanguliza penzi utakua ni mtu wa kuumia sana ukweli ni kwamba hutegemei mpenzi wako akukosee kitu fulan labda akusaliti ukiweka penzi pamoja na ule msukumo wake utajikuta huamini kilichotokea na punde una develop chuki kwa kile alichokifanya. weka uvumilivu halafu upendo ufuate.
 
Last edited by a moderator:

Tatizo ni kuwa uvumilivu hauwezi kuja bila sababu. Utavumilia kwa vile labda unategemea matokeo fulani. Kupenda kwa upande wake kunazalisha mambo tofauti ikiwa uvumilivu ni moja wapo lakini uvumilivu au bila uvumilivu penzi linakuja tu na ndio maana tunawakuta watu wenye wivu wa kupindukia na wengine mayoyoyo kwa wanaowapenda.
 

Afu weye mbona hujanambia kama kuna sredi umeanzisha? Hivi gfsonwin bado uko kwenye mapenzi ya tamthilia? Ambia wote MwanajamiiOne, Mbu, nyumba kubwa, Mamndenyi Dark City na legends wote wa MMU... Kwenye penzi la kweli HAKUNA uvumilivu kwa kuwa penzi la kweli halina kisababisho cha mtu Kuvumilia. UVUMILIVU huja kwenye penzi la kulazimisha.... AMINA
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…