Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
my dearest sister sasa huyo mama mdogo watu watasema alikuwa mjinga labda ama hana kazi ama elimu etc. mimi naomba nikupe ushuhuda kidogo tu wa kwangu binafsi na nisemapo nimepita namaanisha.
mume waliwah kununua gari zuri sana sikuwa kulipanda zaid ya kimada aitwae ANA. nakumbuka enzi hizo nikienda salun sinza anakuja na pikipiki ya mume wangu ananitukana matusi ya nguoni na kunidoboleshea wanayofanya na mr ndani ya gari. sikuwah kumjibu hata siku moja wala kulia nillisema silii.
haikuishia hapo nyumba tuliyojenga alijua atahamia yeye akaja kunipa mchambo mtakatifu nikiwa nasuka nywele saluni moja mitaa ya sinza, kurudi home mr ukimweleza anakwambia kabisa wewe kwanini ulienda kusuka huo si unamfuta mwenyewe, ngoja akuumize. hapo napo nilivumilia.
kibaya zaid nilichukulia kama changamoto sikushtaki kwa nani wala nani na niliua hisia za hasira manake natoka kabila moja hivi so sikupende watu wachukulie kama sababu, wala sikumchukulia Rb. nikiwa navumilia bado mr alisafiri aliporudi alishukia kwake na zawadi zote za ulaya nakumbuka sitasahau. na baada ya siku kama 5 ndipo wanakuja wote home usiku nikamkaribisha. waliingia wote ndani hadi kwa rum, sikufichi walilala nikalala na watoto.
asbh wanaamka wanakuta hadi chai na supu iko mezani, walihisi nimetia sumu but niliwahakikishia kwa kula pamoja nao na watoto na nikafuta meza nkawaualiza mchana watakula nini. mtoto wa mume wangu ndiye aliyeuliza baba huyu ni nani? yule mwanamke aliapotaka kujibu tu ikawa kama mume wangu kaumizwa akamwambia tena kwa ukali wewe kahaba toka ndani mwangu. Nilishtuka kama naimepigwa shoti ya umeme. Mr alikasirika sana akataka kumpiga lakini nilimtetea yule mwanamke ili asije akaumizwa. mimi na wanangu tulilia sana.
yule ANA alitolewa ndani kama mwizi kwa mateke akiwa amejifunga kitenge changu kiunoni. na hapo bado mume wangu alikuwa na mtoto wa mashtuzi ambaye nilimkuta na niko nae hadi leo.
mume wangu alishangaa sana moyo wangu jinsi ulivyo, uvumilivu na upendo wangu kwake ulimbadilisha ndio maana nimwambiapo King'asti kuwa uvumilivu humbadilisha hata shetani kuwa malaika ni kweli nimeshuhudia. leo hii nina miaka zaid ya 10 na naifurahia ndoa. naamini hakuna binti ambaye anaweza kupita hapa ila mimi nilichoangalia ni nataka nini kwenye maisha yangu? na je kwanini nitaabishe amani yangu?
haikuwa kazi rahisi kuvumilia ila ni Mungu tu alinivusha sikuwah kushtaki hata siku moja kwa mama wala ndgu wa pande zote mbili wala kwa shosti zaid ya Mungu. niliia hadi mto ukalowa machozi nilisali hadi kung'ata sura za biblia nakumbuka zab 16&17. hadi leo hii hiyo biblia inaalama za meno ambazo nilizitia miaka kama 7 hivi iliyopita.
nihitimishe kwa kumtia mama mwenzangu moyo kuwa Mungu anaweza yote usimweleze mtu sema na Mungu. halafu omba amani uone yani muujiza hutokea punde.

Nakshi ukitaka kuwa mvumilivu usiwe kwanza msemaji sana,msikilizaji wa ushuhuda wa wenzio hasa kwenye maamuzi yakushindwa, usiwe mtu wa kuchukia na kunyooshe kidole mwenzio ila mara zote jiweke wewe kama ndiye sababisho inaumiza kweli hasa pale inapokuwa wewe siyo sababu lakini huwa najiamnisha tu ili niweze kupata amani yangu na kupata suluhu ya swala lenyewe. hii ni tabia yangu hata kama nekosewa na mtu baki huwa nafanya hivyo.ningekuwa na moyo au roho kama ya kwako ningefurahi sana, ila mimi uvumilivu zero kabisa kila nikijatahidi nashindwa
sijuhi nifanyaje?
gfsonwin na sister,uvumilivu ni matokeo ya upendo,lakini kuna uvumilivu na maradhi ya uvumilivu(kihisia).Hili la maradhi sio matokeo ya upendo ni matokeo ya njaa ya kupendwa na kutojiamini.Yapo mambo yanayovumilika kibinadamu lakini yapo yasiyovumilika.Ufujaji kwa mfano,una madhara kihisia na kimwili,na matokeo yake ni kifo kwa anaefujwa.Mfujaji ni kazi sana kubadilika na ni kazi zaidi kuishi nae.Ukimkuta mtu anaishi na mfujaji haujui upendo na hajiamini.Upendo ni pamoja na kujipenda na kuwapenda wengine.Mtu anapokua na tabia za hatari kama ufujaji ni wa kuepukwa,sisemi umchukie,kumuepuka ni kuepuka kuwa kama kuwa nae kindoa n.k,lakini unampenda bado kama mwanadam.Unapovunja uhusiano na mtu wa aina hii haina maana unamchukia,bali unamthamini na unajithamini pia..Unaepusha kudhurika na kumsababishia matatizo.Huo ni upendo,uvumilivu utaeleweka kama mtu ataujua upendo kwani uvumilivu una mipaka yake!
Aisee kweli leo nimejifunza mengi..
Kiukweli uvumilivu unahitajika sana kwenye ndoa, vinginevyo haitadumu. Ila kama walivyosema baadhi wa watu, kuna vinavyovumilika na visivyovumilika. Hata biblia (sina uhakika na Quran) imeweka bayana mambo haya kwa wanandoa
Eiyer mdogo wangu panapo upendo wa kweli, na ukawepo uvumilivu wa dhati, nakushuhudia kwamba hutomuepuka bali utambadilisha. ilinichukua miaka 4-5 kuishi maisha ya tabu dhiki na majonzi na vilio lakini ikanichukua kitendo cha dakika moja ama mbili kubadilisha kila kitu kuwa historia.
ninaposema uvumilivu hauhesabu gharama namaanisha mdogo wangu, usikimbilie kwenye gharama bali angalia wewe amani yako waipata wapi? sikufichi Eiyer wewe ni mdogo wangu nakupenda sana na sipendi kukukuza kwa maneno haya ila naomba nikwambie kwa faida ya wengine pia.
niliangalia haya ili kuvumilia, nimeolewa nikiwa bikira skumjua mwanaume anafananaje, na nikasema sitatoka nje ya ndoa yangu na hiyo iko hivyo manake sitaki, sasa mume amenionyesha sura tofauti nifanyeje? je niondoke halafu nitaweza kuish pasi kutiwa? je kuna magonjwa anaweza kuniletea nikasema kama Mungu upo umeniona nilivyojitunza kama utaruhusu nife kwa UKIMWI sawa ni mapenzi yako ila nakuomba angalia uaminifu wangu kwako, hapo hapo nikawaza hivi huko nje si ndio naufuata ukimwi kabisa? ni bora aniletee kuliko tuleteane kwa wakati huo. nikawaza je kuvunja mwiko niliojiwekea nitakua na amani? Pia niliwaza nina watoto nimezaa, na kunammoja wa mashtuzi wa mr je huyu naye nikiondoka hatima yake itakuwa ni nini?
sikupenda kufanya maamuzi ya papara bali niliitafuta amani ya Mungu na kwa wakati wake alinijibu na sasa napeta kwenda mbinguni. Ni ngumu kama utaamua kwa akili zako na za marafiki ama watu wa karibu yako ila ni rahisi kama Mungu atakuamulia.
habari za ijumaa wana MMU.
Leo nimekuja na hii mada hapa iitwayo uvumilivu hasa katika maisha ya ndoa. Mara nyingi sana nimekuwa nikisema ndoa yahitaj uvumilivu lakin sidhani kama naeleweka ipasavyo juu ya hili neno.
wataalamu wa lugha watanisaidia kuidefine vizuri bali mimi naomba nieleze nguvu ya uvumilivu panapo mapenzi ya kweli.
Jamani kwanza naomba mnielewe kwamba kwenye mapenzi ya dhati uvumilivu hutangulia, na hii hutokana na ukweli kwamba upendo huvumilia. Panapo upendo ule usiosukumwa na mambo ya nje bali ule wenye msukumo wa ndani tu uvumilivu hutangulia na hii ni kwasababu kuu mbili nazo ni:-
1) uvumilivu huona mapungufu ya mwenza wako kama changamoto wala si kama chuki.
2)uvumilivu hauhesabu gharama za kazi,upendo,kujitolea ama hela.
kwasababu hizi mbili siku zote mimi huwa naishi kwa kuvumilia mbele upendo ukafuata nyuma. na hii ni kwasababu ninapenda kwa dhati na wala si kwababu ya msukumo wa vitu ama kitu.
naona niifupishie hapa nisiwachoshe kwa maneno mengi mkashindwa kudadavua. nakaribisha maswali na maelezo ya nyongeza.
gfsonwin, nakubaliana nawe juu ya thamani ya uvumilivu katika penzi lakini kwangu nahisi hapo kwenye bold cha mbele umeweka nyuma. Ni penzi mbele uvumilivu nyuma.
my dearest Ngekewa yaani ukitanguliza penzi utakua ni mtu wa kuumia sana ukweli ni kwamba hutegemei mpenzi wako akukosee kitu fulan labda akusaliti ukiweka penzi pamoja na ule msukumo wake utajikuta huamini kilichotokea na punde una develop chuki kwa kile alichokifanya. weka uvumilivu halafu upendo ufuate.