uvumilivu...

acha uongo, mbona sie tumevumiliana???


Hujambo lakini?

 
Last edited by a moderator:
gfsonwin nimeguswa sana na ushuhuda wako......
Nilisita kidogo kuchangia mwanzoni kwa sababu nilikuwa nasubiri nione wenzangu watasemaje.
Neno uvumilivu ni msamiati mgumu sana kuumeza, wengi hapa wamekuja na ushuhuda mwingi kuonyesha kwamba yapo yasiyoweza kuvumilika... Je ni kweli wanayosema? hapo ndipo ninapotaka kujikita.
Naomba nikiri kwamba, wakati mwingine kuna ugumu kukabiliana na hali isiyopendeza, kuna wakati mwingine kiwango chetu cha uvumilivu na subira hufika kikomo, ni pale tu imani zetu na matarajio yetu yanapokuwa hayajatikiswa ndipo tunapoweza kumudu kusimama imara na kuwa na subira, na mara nyingi subira huwa inalipa. kuna wakati kelele za nje na kukatishwa tamaa hutuondoa katika urazini (awareness)na kujikuta tukiingia katika ugigili (frustration) na kukosa subira, na hapo ndipo maamuzi yasiyo na busara huchukua nafasi.
naomba niseme tu kwamba ni wachache sana wanaoweza kumudu changamoto kama iliyokupata na wakamudu kuvuka...... Lakini pia kuna kiwango ambacho mtu hufikishwa, uvumilivu ukafika kikomo................
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin , shosty umenigusa kweli kwa hii mada...

Hata kama nampendaje mtu, uvumilivu kwangu una mwisho kwenye vitu fulani..kuna mambo ambayo siwezi kuyavumilia na haya nayawasilisha mapema niwapo kwenye mahusiano (inshallah, nitakapoolewa).. Mfano, sitomvumilia mwanaume atakayenipiga hata siku moja.

Siwezi kuwavumilia marafiki wanafiki, hivyo huwa watu kama hawa wananitoka mapema na kurudi kwenye mzunguko wa maisha yangu ni ndoto.

Kuna mambo mengine duniani kuyavumilia inahitaji moyo wa ziada.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin pole mumie, una moyo wa chuma. Yaani nakuhakikishia ni wanawake wa kuhesabika wangeweza kuvumilia hilo tukio ukizingatia ni dharau ya juu mumeo alikuonyesha kuja na ANA nyumbani kwenu na kulala nae hapo jamani..

Huh, pole sana kwa yote uliyopitia..Kama ulivumilia hilo kwenye ndoa sidhani kama kuna lingine litakuteteresha.
 
Sikujua kama huu mjadala umefika hapa tena pazuri.............Safi sana gfsonwin. Nafikiri pia wanandoa wengi zama hizi huwa wanaingia kwenye ndoa wakiwa na negative expectations...

1. Akinipiga tu naondoka
2. Nikimkuta ana mahusiano ya ngono na mwanaume/mwanamke mwingine hapo mwisho
3. Maisha yakienda kombo sina haja ya kuendelea naye......nani anataka shida
4. N.K

Na Biblia inasema "akiwazacho mtu ndicho kimtokeacho"........na hapo ndipo tunaposhindwa.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin,sikuuliza kama ulimuuliza siku ile ile,hata baadae,ila inaonekana hujawahi kumuuliza na hili ni kosa.Ni kosa kwa sababu kama wewe ndo ulisababisha unaweza kusababisha tena.Kujua chanzo cha tatizo ni tiba ya kudumu.Kuhusu changamoto uliyopitia pamoja na matokeo chanya uliyopata,hukupaswa kuteseka namna hiyo.Kwa nini uteseke hivyo?Trust me,matokeo yoyote hasi kama yangetokea yangekua juu yako.Samahani lakini sikupi sifa kwa uvumilivu huo,na siwezi kumshauri yoyote kufanya uliyofanya,"it's a suicide",leo tunazungumza hapa kwa sababu ulitokea tundu la sindano,plz usimshauri mtu kufanya huo mchezo huo wa kifo.Hayo uliyofanyiwa yalihatarisha maisha yako na Mungu asingehusika na lolote hapo na hakupanga hayo,kumbuka Mungu alitoa ruhusa kuachana kwenye jambo hilo.USIRUDIE!Nenda kasome uzi wa Mtambuzi wenye kichwa cha habari "Mwanaume haonji mara moja" . . . . .. . .!
 
Last edited by a moderator:
Dada gfsonwin baada ya kusoma uzi wako, comments za wachangiaji wengine na majibu yako kwao, nathibitisha kuwa kwa mara ya kwanza nimejifunza jambo la msingi sana kuhusu maisha ya ndoa.

Asante sana kwa ushuhuda uliotoa. Hakika una moyo wa ajabu! Wengine huita moyo wa jiwe. Kutokana na niliyojifunza toka kwako, kuanzia sasa sitalalamika lalamika tena. Nitajipa raha/furaha na mambo mengine yote natumai yatafutia hiyo furaha. God bless you and your family abundantly!
 
Last edited by a moderator:

haya utayasema iwapo tu humpendi mtu kwa dhati binafsi sikufanya ili nisifiwe bali ili kupata amani yangu nafsini. muda mwingine huweza kumjaribu mtu na unajaribiwa siku zote kwa kile unachokipenda believe it.
 

ahsante sana dada mwaJ, nashukuru kwamba umepata kitu cha kukujenga. mpenzi katika ndoa usilalamike wala kulia kwa mtu. hebu mwambie Mungu huku ukifanya bidii kwa uaminifu juu ya ndoa yako naamin atatenda jambo. si jambo la siku moja lakin atafanya kwa wakati wake.
 
Last edited by a moderator:
mh ipo kazi uongo uzinzi uwasherati vipigo matusi wizi utapeli matumizi ya kibinafsi katika kipato cha pamoja je hayo yote kwa ndoa moja unavumilia kuna upendo kweli au
 
Eiyer mdogo wangu hivi umesahau kwamba mtu hujaribiwa kwa kile akipendacho? tena usiseme nyamaza kimya dogo hujakua aisee, manake kama niliwah kupiga goti kumuomba Mungu mume na akanipa mume mzuri kisha akabadilika what does it mean when it comes to faith? kumbuka mpaka uombe kitu ina maana unakipenda na unachokipenda wewe pia kuna wengi hawatamani ukipate, na pia shetani naye anaweza tu kukushtaki kwa Mungu sasa huyu si alikuwa anaaomba ndoa mbona umempa mume mzuri je anaweza kumvumilia? tena ibilisi alivyo atasema wazi naomba nikamjaribu kama kweli alimaanisha kuipenda ndoa yake na ye Mungu atamwambia nenda. hapo ndipo utakapoona mchana ni usikuna usiku ni asubuhi.

sihitaj unisifu Eiyer kwani nia yangu ni kuwafunza wengine wengi tu ndoa ikoje na kwanini wasilalamike na kulia tu. naamini wapo waliojifunza kwenye ushuhuda wangu. jipange upya ma bro.
 
Last edited by a moderator:
platozoom kama mtu anapiga goti kuomba ndoa basi na ajuae kabisa kuwa Mungu atampa ndoa njema sana lakin lazima atapita tu ili kumkuza kiimani na hapo ndipo atakapochagua ama kwenda na ibilisi ama kwennda na mungu.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin,bado sijaona cha kujifunza kwenye mchezo wako wa kifo.Hebu niambie,Mungu alikuoneshaje kuwa huyo ni mume bora mpaka ufikie kuvumilia mambo ya hatari kiasi hicho?Huo sio upendo ni maradhi.Narudia tena siwezi kumshauri mtu afanye hayo.Upendo haupo hivyo.Upendo ni pamoja na kujipenda.Unapojipenda ndipo unajifunza kupenda wengine,kuwapenda wengine ukajiacha wewe ni tatizo.Ni kweli mtu hujaribiwa na kile akipendacho lakini majaribu mengine ni sauti ya kukuambia uondoke mahali ulipo.Sihitaji kukua zaidi ya hapa ili kuyajua haya!
 
Eiyer that is your stance so sina tashwishwi nayo. kwangu mimi from the first time nilipoamua kuwa naingia ndoani i knew kwamba alikuwa ni chaguo langu toka kwa Mungu. na hata alipobadilika nilimuuliza Mungu kama kila kutoa kuliko kwema na kila kitolewacho kilicho kamili hushuka kutoka kwako na kwako hakuna kugeuka wala kivuli cha kubadilika badilika sasa kwanini huyu mume aliye mwema abadilike?? Pia eiyer Mungu alikuwa na uwezo wa kuzuia yote hayoYASITOKEE lakin kwanini aliruhusu yatokee?

ni kweli mungu karuhusu kutalikiana ikiwa ni juu ya maswala ya uzinzi lakin je ningekwenda kuanza kutiwa upya na wanaume wengine?au je ningeweza kuish pasi kutiwa?
 
Last edited by a moderator:

mhhh choice of words
 
gfsonwin,hujajibu swali,nimekuuliza,ulijuaje kuwa huyo ni Mungu amekupa mpaka ukaridhia kuvumilia maswaibu yotn hayo?Tatizo lako linafanana na la wengine,KUJIAMINI.Tunaogopa kuanza upya.Hayo nimeyaona kwenye kauli yako kwenye paragraf ya mwisho.Tatizo lako ni kuanza upya.Hii inatokana na kutokiamini chanzo kilchokupa mume,kama kweli Mungu alikupa huyo mume kwanini usiamini kuwa atakupa mwingine?How do u know kuwa hafanyi tena?Je akirudia?Acha kurahisisha mambo magumu.Unadhani ni kwanini Mungu aliruhusu talaka kwenye suala hili?Unadhani alikosea?I don't think so!
 
Last edited by a moderator:
aisee basi labda hunielewi binafsi huwa napata majibu ya maswala yangu kwenye bible so nikisoma na nkipata neno najua ndilo Munu alilokusudia kwangu. nilijua kwasababu yeye ainifunulia hayo kwenye maandiko yake.

binafsi si kwamba sikujiamini la hasha bali kama nilihsa wah kusema sitovua nguo yangu kwa sec person sidhani kama nilitakiwa niende kinyume na msimamo wangu huu. pia hakunaga malaika humu duniani naweza nikamkimbia huyu amemleta ANA ndani nikakuta kwa mwingine ni mchawi so kwangu tena ni bora kama ndoa ikivunjiak basi mtu ukae usioe wala kuolewa tena.
 
ee Mungu nakushukuru tu kwamba hivi nilivyo ndio maisha............lol dada umenikumbusha mbali sana mimi nakumbuka niliwah kuuliza hapa kwamba nataka kuanguka dhambini kwa matatizo ya kwenye ndoa nikataja sifunguliwi mlango nk nilishambuliwa hapa kama mpira kidogo nihame jukwaa kumbe kuna wanaopita zaid yangu? basi nisameheni sana Mr Rocky nisamehe mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Mi naona upendo ndio cha kwanza, huwezi mvumilia mtu usompenda; ntakuvumilia as long as nina feelings na wewe; lakini kutokana na maudhi feelings za upendo zinaishaga mjue....na zitakapoisha hapo ndio utajua kuwa mi mvumilivu or not.

Mama yangu alikuwa mvumilivu mpaka tulikuwa tunajiuliza huyu mama vipi...? ukichanganya kuwa si muongeaji alikaa kwenye ndoa zaidi ya miaka ishirini, baba aliona kapata zoba; siku alipotoa mguu kwenye geti hakurudi tena... Baba alikuwa ame relax anajua anamtishia tu atarudi kwa kuwa ni mke mvumilivu na hajawahi kuondoka. Mbona aliisoma namba na sasa wana miaka zaidi ya 20 ya separation plus divorce.

Shishangilii watu kutengana lakini walipofikia hasa kwa upande wa mama watoto wote tulifurahi walipotengana maana mama alikuwa anakondeana tu kwa mawazo; hata kuona tabasamu lake ilikuwa ni ndoto. Though tunampenda baba kwa kuwa ni baba mzuri sana kwa watoto ila mume mbaya
 
Dada yangu wewe!!!!I realy feel sory 4 u,ninachotaka ni ulipotoa huo uhakika.Mungu alikuambiaje?Alikuoneshaje hayo maandiko?Kinachonishangaza ni wapi na ni namna gani na ni kwanini u-risk maisha yako na wanao kwa binadamu kama wewe,for what?Yeye ni nani?Ana nini?Ungekufa mateso ya wanao ya kukukosa mama yangekua on u!Narudia tena USIRUDIE.Jamani wanawake wa JF yapo ya kuvumilia,lakini mengine ni kujidhalilisha.Huu mchezo msifanye.Kuhusu msimamo wako wa kutomvulia nguo mtu mwingine ni moja kati ya mambo ninayoweza kusema ni mabaya sana.Unajifunga kwa kauli zako mwenyewe.Kwanini ujifungie kwenye kiberiti na ukijiaminisha maisha yote ni kama hayo?Kwanini unaamini hakuna mwanaume bora mpaka ufikirie hata utakaempata mwingine atakua wa hovyo zaidi?Kwanini unakua hasi?Kumbuka kile unachowaza na kukiamini ndicho unachokipata.Ulijiapiza hutovua nguo zako kwa mwanaume mwingine,sasa unakua mtumwa wa kauli na maapizo yako.Najua hakuna anaeanzisha ndoa ili ife lakini kuna mambo yasiyokwepeka hata Mungu anajua hilo.Pia hujiamini hata kauli na matendo yako yana vinaashiria hivyo.Uvumilivu ni mzuri,ila ulipoutumia siyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…