my dearest
sister sasa huyo mama mdogo watu watasema alikuwa mjinga labda ama hana kazi ama elimu etc. mimi naomba nikupe ushuhuda kidogo tu wa kwangu binafsi na nisemapo nimepita namaanisha.
mume waliwah kununua gari zuri sana sikuwa kulipanda zaid ya kimada aitwae ANA. nakumbuka enzi hizo nikienda salun sinza anakuja na pikipiki ya mume wangu ananitukana matusi ya nguoni na kunidoboleshea wanayofanya na mr ndani ya gari. sikuwah kumjibu hata siku moja wala kulia nillisema silii.
haikuishia hapo nyumba tuliyojenga alijua atahamia yeye akaja kunipa mchambo mtakatifu nikiwa nasuka nywele saluni moja mitaa ya sinza, kurudi home mr ukimweleza anakwambia kabisa wewe kwanini ulienda kusuka huo si unamfuta mwenyewe, ngoja akuumize. hapo napo nilivumilia.
kibaya zaid nilichukulia kama changamoto sikushtaki kwa nani wala nani na niliua hisia za hasira manake natoka kabila moja hivi so sikupende watu wachukulie kama sababu, wala sikumchukulia Rb. nikiwa navumilia bado mr alisafiri aliporudi alishukia kwake na zawadi zote za ulaya nakumbuka sitasahau. na baada ya siku kama 5 ndipo wanakuja wote home usiku nikamkaribisha. waliingia wote ndani hadi kwa rum, sikufichi walilala nikalala na watoto.
asbh wanaamka wanakuta hadi chai na supu iko mezani, walihisi nimetia sumu but niliwahakikishia kwa kula pamoja nao na watoto na nikafuta meza nkawaualiza mchana watakula nini. mtoto wa mume wangu ndiye aliyeuliza baba huyu ni nani? yule mwanamke aliapotaka kujibu tu ikawa kama mume wangu kaumizwa akamwambia tena kwa ukali wewe kahaba toka ndani mwangu. Nilishtuka kama naimepigwa shoti ya umeme. Mr alikasirika sana akataka kumpiga lakini nilimtetea yule mwanamke ili asije akaumizwa. mimi na wanangu tulilia sana.
yule ANA alitolewa ndani kama mwizi kwa mateke akiwa amejifunga kitenge changu kiunoni. na hapo bado mume wangu alikuwa na mtoto wa mashtuzi ambaye nilimkuta na niko nae hadi leo.
mume wangu alishangaa sana moyo wangu jinsi ulivyo, uvumilivu na upendo wangu kwake ulimbadilisha ndio maana nimwambiapo
King'asti kuwa uvumilivu humbadilisha hata shetani kuwa malaika ni kweli nimeshuhudia. leo hii nina miaka zaid ya 10 na naifurahia ndoa. naamini hakuna binti ambaye anaweza kupita hapa ila mimi nilichoangalia ni nataka nini kwenye maisha yangu? na je kwanini nitaabishe amani yangu?
haikuwa kazi rahisi kuvumilia ila ni Mungu tu alinivusha sikuwah kushtaki hata siku moja kwa mama wala ndgu wa pande zote mbili wala kwa shosti zaid ya Mungu. niliia hadi mto ukalowa machozi nilisali hadi kung'ata sura za biblia nakumbuka zab 16&17. hadi leo hii hiyo biblia inaalama za meno ambazo nilizitia miaka kama 7 hivi iliyopita.
nihitimishe kwa kumtia mama mwenzangu moyo kuwa Mungu anaweza yote usimweleze mtu sema na Mungu. halafu omba amani uone yani muujiza hutokea punde.