Afu weye mbona hujanambia kama kuna sredi umeanzisha? Hivi gfsonwin bado uko kwenye mapenzi ya tamthilia? Ambia wote MwanajamiiOne, Mbu, nyumba kubwa, Mamndenyi Dark City na legends wote wa MMU... Kwenye penzi la kweli HAKUNA uvumilivu kwa kuwa penzi la kweli halina kisababisho cha mtu Kuvumilia. UVUMILIVU huja kwenye penzi la kulazimisha.... AMINA
Eiyer lakini pia nilisema kama mtu huyo atajifunza kwa kosa hilo, kamwe hatorudia tena...................gfsonwin,sikuuliza kama ulimuuliza siku ile ile,hata baadae,ila inaonekana hujawahi kumuuliza na hili ni kosa.Ni kosa kwa sababu kama wewe ndo ulisababisha unaweza kusababisha tena.Kujua chanzo cha tatizo ni tiba ya kudumu.Kuhusu changamoto uliyopitia pamoja na matokeo chanya uliyopata,hukupaswa kuteseka namna hiyo.Kwa nini uteseke hivyo?Trust me,matokeo yoyote hasi kama yangetokea yangekua juu yako.Samahani lakini sikupi sifa kwa uvumilivu huo,na siwezi kumshauri yoyote kufanya uliyofanya,"it's a suicide",leo tunazungumza hapa kwa sababu ulitokea tundu la sindano,plz usimshauri mtu kufanya huo mchezo huo wa kifo.Hayo uliyofanyiwa yalihatarisha maisha yako na Mungu asingehusika na lolote hapo na hakupanga hayo,kumbuka Mungu alitoa ruhusa kuachana kwenye jambo hilo.USIRUDIE!Nenda kasome uzi wa Mtambuzi wenye kichwa cha habari "Mwanaume haonji mara moja" . . . . .. . .!
Watafiti na wataalamu wengi wa masuala ya uhusiano wanakiri sasa kwamba, mwanaume akishatoka nje mara moja kwenye uhusiano wake, atatoka tena na tena. Kwa hiyo kama mwanamke amemfumania mpenzi wake au mumewe, basi ajue kwamba upo uwezekano mkubwa sana wa bwana huyo kumsaliti tena. Kutoka mara moja na kuacha siyo kawaida ya wanaume, labda tu kama atajifunza soma kubwa sana baada ya kutoka mara moja.
eversilin gal huyu rafiki yako analichukuliaje ilo la kuambiwa asifanye kazi wala kujiendeleza kielimu? je anaona kama ni changamoto ama limemzalia chuki kwa mwenzi wake kiasi cha kutaka kuondoka? hapo ndipo penye ugomvi mkubwa sana na wanawake wengi kwani kila mapungufu ya mwanaume yanachukuliwa kama chuki jambo ambalo ni baya sana.nimemsoma Gfsonwin nampa hongera na pole pia uvumilivu unategemea na mambo unayoyavumilia nadhani kwa wale waliosoma uzi uliosema ANATAMANI AFANYE MAAMUZI MAGUMu,ni kuhusu rafiki yaangu ambaye ameolewa lakini mume wake hataki afanye kazi wala ajiendeleze kielimu hatuna mkataba na Mungu je huyo mwanaume asipokuwepo leo je na yeye pia aendelee kuvumilia hayo maisha ya kuwa mama wa nyumbani ilhal amesoma au akimbie aangalie future yake
Afu weye mbona hujanambia kama kuna sredi umeanzisha? Hivi gfsonwin bado uko kwenye mapenzi ya tamthilia? Ambia wote MwanajamiiOne, Mbu, nyumba kubwa, Mamndenyi Dark City na legends wote wa MMU... Kwenye penzi la kweli HAKUNA uvumilivu kwa kuwa penzi la kweli halina kisababisho cha mtu Kuvumilia. UVUMILIVU huja kwenye penzi la kulazimisha.... AMINA
habari za ijumaa wana MMU.
Leo nimekuja na hii mada hapa iitwayo uvumilivu hasa katika maisha ya ndoa. Mara nyingi sana nimekuwa nikisema ndoa yahitaj uvumilivu lakin sidhani kama naeleweka ipasavyo juu ya hili neno.
wataalamu wa lugha watanisaidia kuidefine vizuri bali mimi naomba nieleze nguvu ya uvumilivu panapo mapenzi ya kweli.
Jamani kwanza naomba mnielewe kwamba kwenye mapenzi ya dhati uvumilivu hutangulia, na hii hutokana na ukweli kwamba upendo huvumilia. Panapo upendo ule usiosukumwa na mambo ya nje bali ule wenye msukumo wa ndani tu uvumilivu hutangulia na hii ni kwasababu kuu mbili nazo ni:-
1) uvumilivu huona mapungufu ya mwenza wako kama changamoto wala si kama chuki.
2)uvumilivu hauhesabu gharama za kazi,upendo,kujitolea ama hela.
kwasababu hizi mbili siku zote mimi huwa naishi kwa kuvumilia mbele upendo ukafuata nyuma. na hii ni kwasababu ninapenda kwa dhati na wala si kwababu ya msukumo wa vitu ama kitu.
naona niifupishie hapa nisiwachoshe kwa maneno mengi mkashindwa kudadavua. nakaribisha maswali na maelezo ya nyongeza.
gfsonwin,sikuuliza kama ulimuuliza siku ile ile,hata baadae,ila inaonekana hujawahi kumuuliza na hili ni kosa.Ni kosa kwa sababu kama wewe ndo ulisababisha unaweza kusababisha tena.Kujua chanzo cha tatizo ni tiba ya kudumu.Kuhusu changamoto uliyopitia pamoja na matokeo chanya uliyopata,hukupaswa kuteseka namna hiyo.Kwa nini uteseke hivyo?Trust me,matokeo yoyote hasi kama yangetokea yangekua juu yako.Samahani lakini sikupi sifa kwa uvumilivu huo,na siwezi kumshauri yoyote kufanya uliyofanya,"it's a suicide",leo tunazungumza hapa kwa sababu ulitokea tundu la sindano,plz usimshauri mtu kufanya huo mchezo huo wa kifo.Hayo uliyofanyiwa yalihatarisha maisha yako na Mungu asingehusika na lolote hapo na hakupanga hayo,kumbuka Mungu alitoa ruhusa kuachana kwenye jambo hilo.USIRUDIE!Nenda kasome uzi wa Mtambuzi wenye kichwa cha habari "Mwanaume haonji mara moja" . . . . .. . .!
Eiyer nimekuelewa, lakini katika maoni yangu nilisema uvumilivu unalipa pale unapoambatana na imani isiyotetereka......... Kwa watu wenye imani isiyotikiswa na wala hawatetereki wanapopata changamoto mara nyingi hupata matokeo mazuri.Mtambuzi,nilichokua namueleza gfsonwin ni mtazamo wangu na msimamo wangu katika hatari aliyoifanya chini ya mwamvuli wa uvumilivu.Nauthamini sana uvumilivu na kuna mambo ya kufanyia uvumilivu,lakini sio kama alilofanya yeye.Ni kweli mtu yoyote anaweza kuwa mtu mpya pale atakapoishi na mvumilivu,lakini hilo linategemea ni mambo gani anatendewa huyo anaevumilia,mengine unaweza kuwa unadhani unavumilia kumbe hujiamini,unahofia utaanzaje ukiwa mwenyewe,hata kama unafanyiwa mambo ya hatari!
Umeona Eiyer. Ukiwa na dada anayevumilia hivi ndio unasikia makaka wameenda kumtoa dada yao kwenye ndoa.. maana ni kama amekuwa brain washed. Haya mambo yalikuwa zamani na ni ilikuwa ukimuuliza mtu kwa nini uchapi lapa anakwambia ni sababu za kiuchumi... labda yatima hana pa kwenda hivyo kuondoka na kukaa ni sawa.
Ila kweli karne hii ya 21 kama bado kuna mwanamke mvumilivu tena aliye well informed, mwenye elimu na kazi yake... siwezi kuelewa hata atoe maelezo gani
Kuna vya kuvumilia kama mume katimuliwa kazi, kaugua... lakini na akili zake timamu anakueletea vimada ndani na vimada wanafikia kukukashfu BIG NO. Kwanza hata huyo mwanaume unaweza kuwa unampa wakati mgumu kwani anataka umpishe aanza maisha upya na ampendae. Ni ung'ang'anizi. Labda kama kweli kuna kurogana.
nyumba kubwa kuvumilia kwangu hakukusababishwa na kutokuwa na kipato wala kazi wala mahali pa kwenda wala kutokujiamini ama woga. nilijiamini sana kuwa mimi ndiye mke sahihi no ways. tena bahati nzuri wazazi wangu wapo hai hadi leo and wako vizuri sana kiuchumi.labda nikwambie sababu na hizi kwenu ziwe za kijinga ama nini kwangu they remained to be critical reasonsUmeona Eiyer. Ukiwa na dada anayevumilia hivi ndio unasikia makaka wameenda kumtoa dada yao kwenye ndoa.. maana ni kama amekuwa brain washed. Haya mambo yalikuwa zamani na ni ilikuwa ukimuuliza mtu kwa nini uchapi lapa anakwambia ni sababu za kiuchumi... labda yatima hana pa kwenda hivyo kuondoka na kukaa ni sawa.
Ila kweli karne hii ya 21 kama bado kuna mwanamke mvumilivu tena aliye well informed, mwenye elimu na kazi yake... siwezi kuelewa hata atoe maelezo gani
Kuna vya kuvumilia kama mume katimuliwa kazi, kaugua... lakini na akili zake timamu anakueletea vimada ndani na vimada wanafikia kukukashfu BIG NO. Kwanza hata huyo mwanaume unaweza kuwa unampa wakati mgumu kwani anataka umpishe aanza maisha upya na ampendae. Ni ung'ang'anizi. Labda kama kweli kuna kurogana.
Kwenye ndoa kunatakiwa heshima sio uvumilivu vipi uvumilie kama mke wako au mme wako anaenda nje ya ndoa.
my dearest sister sasa huyo mama mdogo watu watasema alikuwa mjinga labda ama hana kazi ama elimu etc. mimi naomba nikupe ushuhuda kidogo tu wa kwangu binafsi na nisemapo nimepita namaanisha.
mume waliwah kununua gari zuri sana sikuwa kulipanda zaid ya kimada aitwae ANA. nakumbuka enzi hizo nikienda salun sinza anakuja na pikipiki ya mume wangu ananitukana matusi ya nguoni na kunidoboleshea wanayofanya na mr ndani ya gari. sikuwah kumjibu hata siku moja wala kulia nillisema silii.
haikuishia hapo nyumba tuliyojenga alijua atahamia yeye akaja kunipa mchambo mtakatifu nikiwa nasuka nywele saluni moja mitaa ya sinza, kurudi home mr ukimweleza anakwambia kabisa wewe kwanini ulienda kusuka huo si unamfuta mwenyewe, ngoja akuumize. hapo napo nilivumilia.
kibaya zaid nilichukulia kama changamoto sikushtaki kwa nani wala nani na niliua hisia za hasira manake natoka kabila moja hivi so sikupende watu wachukulie kama sababu, wala sikumchukulia Rb. nikiwa navumilia bado mr alisafiri aliporudi alishukia kwake na zawadi zote za ulaya nakumbuka sitasahau. na baada ya siku kama 5 ndipo wanakuja wote home usiku nikamkaribisha. waliingia wote ndani hadi kwa rum, sikufichi walilala nikalala na watoto.
asbh wanaamka wanakuta hadi chai na supu iko mezani, walihisi nimetia sumu but niliwahakikishia kwa kula pamoja nao na watoto na nikafuta meza nkawaualiza mchana watakula nini. mtoto wa mume wangu ndiye aliyeuliza baba huyu ni nani? yule mwanamke aliapotaka kujibu tu ikawa kama mume wangu kaumizwa akamwambia tena kwa ukali wewe kahaba toka ndani mwangu. Nilishtuka kama naimepigwa shoti ya umeme. Mr alikasirika sana akataka kumpiga lakini nilimtetea yule mwanamke ili asije akaumizwa. mimi na wanangu tulilia sana.
yule ANA alitolewa ndani kama mwizi kwa mateke akiwa amejifunga kitenge changu kiunoni. na hapo bado mume wangu alikuwa na mtoto wa mashtuzi ambaye nilimkuta na niko nae hadi leo.
mume wangu alishangaa sana moyo wangu jinsi ulivyo, uvumilivu na upendo wangu kwake ulimbadilisha ndio maana nimwambiapo King'asti kuwa uvumilivu humbadilisha hata shetani kuwa malaika ni kweli nimeshuhudia. leo hii nina miaka zaid ya 10 na naifurahia ndoa. naamini hakuna binti ambaye anaweza kupita hapa ila mimi nilichoangalia ni nataka nini kwenye maisha yangu? na je kwanini nitaabishe amani yangu?
haikuwa kazi rahisi kuvumilia ila ni Mungu tu alinivusha sikuwah kushtaki hata siku moja kwa mama wala ndgu wa pande zote mbili wala kwa shosti zaid ya Mungu. niliia hadi mto ukalowa machozi nilisali hadi kung'ata sura za biblia nakumbuka zab 16&17. hadi leo hii hiyo biblia inaalama za meno ambazo nilizitia miaka kama 7 hivi iliyopita.
nihitimishe kwa kumtia mama mwenzangu moyo kuwa Mungu anaweza yote usimweleze mtu sema na Mungu. halafu omba amani uone yani muujiza hutokea punde.
Girl! Thats why i do say i love u! Ur coments, and posts shows and tells how strong ur! Ur my heroine cuz u live heroic and u encourage others! To some extent I saw myself in ths post of urs bt i wasnt strong enough to wait up to the finishing line....u inspire me! Be blesed my dada.
Du gfsonwin kwanza pole na hongera pia; mshukuru pia Mungu wako ambaye amekupa hicho kipaji cha uvumilivu na mwisho akaendelea kuwa mwaminifu kwa kukureward (kumrudisha mumeo ndani).
Mimi Mungu hajanijlia kipaji hicho, na nafikiri alijua l am better off this way. Ambavyo kanijalia na kunipa nguvu ya kumilia nitavumilia; ambavyo sina stamina navyo sijilazimishi navyo. I wouldn't wanna be you, pamoja na kwamba nakuadmire.
Bishanga usisahau kwamba kuna mambo mengine huna jibu lake yaani solution comes at the scene. and to it is like that. manake nikuulize hivi wewe Bishanga waweza kumsamehe mkeo anapocheat?Mimi bishanga abashaija nikiwa na akili timamu bila kushurutishwa na wana jamvi,hasa gfsonwin,nakuchukua wewe The secretary uwe mke wangu,katika tabu na raha,hata ukini cheat na Eiyer nitavumilia tu.
Huo ndo uvumilivu,bishanga anaku cheat we umo tu,gfsonwin uko tayari mzee akufanzie na Kaunga kisha uvumilie tu?