Uvunjaji wa sheria za usalama barabarani unaofanywa na madereva bodaboda

Uvunjaji wa sheria za usalama barabarani unaofanywa na madereva bodaboda

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
346
Reaction score
522
picha kwa hisani ya Masoud Kipanya,toka mtandaoni!

IMG_6813.jpeg


👉🏾
Kwani toka lini bodaboda hasa katika jiji la Dar Es Salaam ,mkapata exceptions kwenye mataa na junction mbalimbali hasa taa za barabarani zinapowaasa msimame??,Kwanini kwenu kufuata taa na alama za barabarani imekuwa nongwa?? Mnahatarisha maisha yenu na ya wengine hasa watumiaji wa barabara!.

👉🏾 Bodaboda kwanini mnang’oa Site-mirror kwenye pikipiki zenu ??,Je ni rahisi zikiwa hivyo bila site-mirror?, Je inarahisiha kujichomeka (sandwich) katikati ya malori mawili yatokayo bandarini kwenda mikoani kwa njia ya Morogoro??? Ni raha eeh ?

👉🏾Wengine mnatujazia kelele ,mnatuletea Noise pollution,si mnaona sifa kutoboa Exhaust ili iwe na muungurumo kama gobore za kizamani ! Najua mnapenda kelele si vichwani kwenu mmejaa visengeri na nyimbo za kiswazi ,sawa tupigieni kelele maana yawezekana huo ndio ustaarabu wenu!

👉🏾Mko busy kuendesha chombo cha moto ilhali miguuni mmevaa Vindala huku mnavining’iniza kwa style ya kuchovya vumbi haya mtasagika vidole muone mtakuwa na muondoko wa aina gani?.

👉🏾Nasikia mkikoswakoswa kwenye bodaboda mnahamia kwenye bajaji ,mkiona abiria popote mnasimama bila kuangalia nyuma nani anakuja ,Shauri yenu mtabambiwa ,fuateni sheria!

Mwisho japo si kwa umuhimu Israel yupo kazini ,msimpe kazi ambayo bado muda wake kufanyika hamumlipi overtime allowance msituletee vilio! Mnamaliza sana nguvu kazi ya taifa !,

Tanzania Police,hawa madereva wazembe msiishie kuwapa fine tu ,bali tundikeni mahakamani limeni Mvua hata 2 wakajifunze utu! Maana wakati meingine visungura vinawafanya wafikiri bodaboda ni ndege !

-kila la heri kwenu katika mabadiliko🙏
 
Mi naendesha kazini Huwa naenda na pikipiki siku zote ila sijawahi kuelewa kwanini Huwa wanazitoa side mirror mi nilijua hawapendi Ile reflection ya mwanga wa magari usiku.

We ndio umenijuza kuwa sababu ni kujichomeka
 
Mi naendesha kazini Huwa naenda na pikipiki siku zote ila sijawahi kuelewa kwanini Huwa wanazitoa side mirror mi nilijua hawapendi Ile reflection ya mwanga wa magari usiku.

We ndio umenijuza kuwa sababu ni kujichomeka
Hawataki usumbufu wakati wakijisandwichi katikati ya malori makubwa yenye mizigo na makontena😆
 
Back
Top Bottom