Uvutaji sigara 'unaozesha' ubongo

Uvutaji sigara 'unaozesha' ubongo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
121027135610_smoking_woman_304x171_e_nocredit.jpg

Uvutaji sigara ni hatari kwa ubongo kulingana na wanasayansi nchini Uingereza


Kuvuta sigara “kunaozesha” ubongo kwa kuathiri vibaya kumbukumbu, uelewa wakati wa masomo na uwezo wa kushauriana. Hii ni kulingana na wachunguzi wa King’s College, nchini Uingereza.

Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri wa zaidi ya miaka 50 ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito kupita kiasi pia ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi.


Wanasayansi walisema ni sharti watu wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili.

Wachunguzi nchini Uingereza walikuwa wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya shtuko wa moyo na kiharusi.


Shirikisho la kuhamasisha kuhusu ugonjwa wa Alzheimer, unaoathiri ambavyo watu wanakumbuka mambo, ulisema: "Sote tunafahamu

ya kwamba uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu, kipimo cha Cholesterol au kiwango cha juu cha mafuta mwilini, huathiri vibaya moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote hivi pia vinaathiri ubongo.


"Ni sharti watu wale chakula chenye lishe bora, wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara, wapimwe shinikizo la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara."


Kuvuta sigara “kwaozesha” ubongo kwa kuathiri vibaya kumbukumbu, masomo na uwezo wa kushaurianana, kulingana na wachunguzi wa King’s College, London.

Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri wa zaidi ya miaka 50 ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito uliopita kiasi pia ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi.

Wanasayansi walisema ni sharti watu wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili.


Wachunguzi wa King's College walikuwa wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya mshtuko wa moyo na kiharusi.

shirikikisho la kuhamasisha ugonjwa wa Alzheimer, unaoathiri kumbumkumbu, ulisema: "Sote tunafahamu ya kwamba uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu, kipimo cha cholesterol cha juu, huathiri vibaya moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote hivi pia vinaathiri uongo.

"Ni sharti watu wale chakula chenye lishe bora, wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara, wapimwe shinikizo la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara."
BBC Swahili - Habari - Uvutaji sigara 'unaozesha' ubongo
 
Tatizo nilionalo ni kuwa pamija ni kuwa matumizi ya aina zote za sumu ikiwemo sigara na hata pombe zina madhara kuna uhaja wa kuonyesha kiwango cha matumizi hayo ni kwa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom