SoC02 Uvutaji wa sigara janga la Taifa

SoC02 Uvutaji wa sigara janga la Taifa

Stories of Change - 2022 Competition

Angina

Senior Member
Joined
May 13, 2018
Posts
142
Reaction score
137
Ilikua sku ya asubuhi sauti ya Babu mwenye umri wa kukadilia Kama miaka 68 aliyekuwa amelala kwenye kitanda wodini na kuwaambia ndugu zake "Mpira nliowekewa pembeni ya kifua changu na unapitisha damu kutoka kwenye mapafu yangu na madaktari wamenieleza mapafu yangu yamejaa damu na nina kansa ya damu " .Baada ya kuchukua mda kidogo kuongea na yule Babu alieza ujana wake wote alikuwa na uwezo wa kuvuta pakiti moja ya sigara[emoji849].

UVUTAJI WA SIGARA
Kwa kipindi cha karibuni dar es salaam na mikoa karibia yote ya Tanzania swala la uvutaji sigara lmekua too much .Alaf mbaya wavutaji hata aibu hawana unaweza kuta yupo kwenye mikusanyiko ya watu anavuta sigara tu bila hata kujari.Na wakati mwingine wanao mzunguka nao wana enjoy tu mtu anavyo vuta hio sigara bila kumwambia avutie pembeni.

Na kwa kiwango kikubwa vijana wadogo chini ya miaka 18 nao wamekua wahanga maana ndo kundi ambapo wanaongoza kuvuta sigara.Ndani ya sigara Kuna kemikali inayoitwa nikotini ambayo ndo hufanya mtu asisimuke baada ya kuvuta sigara.

Kitaalam wanasema unavovuta sigara mara kwa mara ndo chanzo kikubwa cha wewe kuhathirika zaidi.Na mara nyingi shida ztokanazo na uvutaji wa sigara uwezi kuziona ukiwa na umri mdogo mara nyingi zinatokea katika umri mkubwa.

Jambo lingine ambalo watu halijui ni kua hata yule ambae havuti lkn yupo jirani na mtu anaevuta sigara mfano mke na mme nae yupo katika hatari ya kupata shida Kama yule anaevuta.

MADHARA YA KIAFYA YATOKANAYO NA UVUTAJI WA SIGARA.

Uvutaji wa sigara unaharibu kila kiungo ndani ya mwili wa mwanadamu Kama vile mfumo wa upumuaji ,moyo na sehemu nyingine.Yafuatayo ni madhara ya sigara kutoka kiungo kimoja moja ndani ya mwili

1.Kansa ya mapafu
Ndani ya sigara Kuna kemikali inayoitwa nikotini.Kemikali hii ndo chanzo kikubwa cha kansa ya mapafu.Kutokana na utafiti katika vifo 9 Kati ya 10 vya kansa ya mapafu kisababishi kikuu ni uvutaji wa sigara.

Naona ni wakat sahihi wa serikali kuanzia vituo maalum pembezoni mwa ma barabara,kwenye mikusanyiko ya watu mfano sokoni ili wavutaji wanapovuta sigara moshi usiwaathir ambao hawavuti sigara.

2.Magonjwa ya moyo
Uvutaji wa sigara hupelekea uharibifu ndani ya mirija ya damu ,moyo na seli za damu .Kemikali iliyo ndani ya sigara hupelekea mishipa ya damu kusinyaa na wakati mwingine kupasuka kwa mirija ya damu ambayo huzuia damu kufika kwenye moyo au sehemu nyingine ya mwili hivyo kupungua kwa kiasi cha oksijen sehemu mbalimbali za mwili .Hii inaweza pelekea vitu Kama maumivu ya kifua ,Ikitokea damu kiasi kidogo imefka au haijafika kbsa kwenye ubongo hii uweza pelekea kiharusi (stroke) hivyo inaweza pelekea kifo.

3.Uharibifu ndani ya mfumo wa uzazi
Kemikali iliyo ndani ya sigara ndo chanzo kikubwa cha mabadiliko ya hormone kwa wanawake hivyo hupelekea mwanamke kutokuwa na uwezo wa kushika mimba.Na Kama mwanamke akishika mimba huweza kupelekea mimba kutungwa sehemu ambayo si sahihi,kujigungua kabla ya mda,kuzaa mtoto mwenye mzito mdogo na inaweza kuwa chanzo Cha vitu Kama mdomo sungura .

Kwa wanaume hupelekea uume kushindwa kusimama na hupunguza ubora wa mbegu za kiume hivyo mwanaume kushindwa kutungisha mimba.

4.Kisukari aina ya pili.
Tafiti znasema anaevuta sigara anauwezekano mkubwa wa kupata kisukari ukilinganisha na yule ambae havuti.Pia mtu mwenye kisukari akiwa anavuta sigara inakuwa ni ngumu sama kwa uyo mtu ku control sukari yake na pia ni chanzo kikuu cha magonjwa ya Figo na moyo kwa mtu ambaye tayari ana kisukari

5.Kinywa kichafu
Mtu anaevuta sigara Kwanza mara nyingi wanakua wanatoa harufu mbaya mdomo ,watu hawa pia huvimba fizi na wakati mwingine kutoa damu wakati wanapiga mswaki ,pia hili swala ni chanzo Cha meno kulegea na wakati mwingine kutoka menyewe na wakati mwingine watu wanaovuta sigara huwa wanakuwa na uchafu kwenye meno yao ambao hautoki kwa kupiga na mswaki.Na wakati mwingine watu hawa wanakua na midomo mikavu maana kiasi cha mate kinapungua kuzalishwa.

6.Kansa ya kinywa ,Koo na wakati mwingine tumbo.

FAIDA ZA KUACHA UVUTAJI WA SIGARA

Unapoacha uvutaji wa sigara maana yake viungo vyote vya mwili vinarudi katika hali ya kawaida .Mfano mapigo ya moyo,mfumo wa uzazi kujifungua mtoto mwenye uzito kamili na katika sku kamili ,uwezo wa kusimamisha na kuongezeka kwa ubora wa mbegu za kiume na mtu kuwa na afya nzuri ya kinywa na mwili.

NINI KIFANYWE NA SERIKALI

Japokuwa sigara ina madhara yote hayo lkn ndo zao linalopewa kipaumbele zaidi ndani ya Tanzania.Ni ngumu Sana kwa serikali kupiga marufuku ulimwaji wa hili zao la kibiashara .Lkn inaweza punguza uzalishaji wake kwa kufanya uwekezaji zaidi kwenye mazao ya chakula ambayo yana uhitaji ukubwa ukilinganisha na mazao ya biashara.

Lakini serikali inabid iweke sheria ambazo zitafanya vijana wa chini ya miaka 18 kuacha kbsa kutumia sigara .

Pia ndani ya jamii matumizi horera ya sigara kila mahali nayo yapunguzwe .Serikali ifanye mpango wa kuweka vituo maalum hasa pembeni ya barabara ambavyo vitakua kwa ajili ya wavuta sigara.Na yoyote atakefuta sigara Tofauti na hayo maeneo apigwe faini .Hii itasaidia watu ambao hawavuti sigara kuepukana na uvutaji wa hewa yenye sigara.
 
Upvote 18
babu yangu alivuta hadi 2014 akiwa na miaka 108 tena alikuwa akipiga nyota zile na tumbaku ya kutosha. Madhara yake nafikiri yanatofautiana kabisa maana kuna wazee kabisa wana 90+ na wanapiga fresh tu wala hawaumwi chochote
Yaaah ni kweli haya madhara nayo yanatofautiana toka mtu adi mtu na kinachotofautisha ni hali ya maisha na uchumi kwa ujumla ,ulaji wa mlo kamili,utumiaji wa vilevi vingine Kama pombe ,bangi na ugoro na pia magonjwa mengine Kama kisukari ,UKIMWI .Mtu mwenye kisukari au UKIMWI na akiwa anavuta sigara madhara yake ni tofauti na mtu ambae hana UKIMWI au kisukari
 
Pia bila kusahau stress
 
Kwa nini sigara zinazalishwa na tena zinauzwa kwa wingi bei poa?

Ni bora viwanda vikafungwa ili kuzuia madhara hayo.

Kinyume chake ni kelele za chura tu, wavutaji wataongezeka sana tu.
Haiko hivyo...

Binadamu amepewa utashi wa kuchagua.

Na ukiangalia vizuri karibu kila kitu kinachozalishwa na binadamu kwa matumizi yake kina madhara. Unajua kuwa mafuta ya kupikia ndiyo chanzo kimojawapo kikuu cha lehemu (cholesterol) inayosababisha kuziba kwa mishipa ya damu na hatimaye kuleta mashambulizi ya kiharusi na moyo? Unajua kuwa ma hamburger haya ya McDonald's na kuku wa KFC ni hatari sana kwa afya yako? Unajua madhara ya soda katika kuharibu ufanyakazi wa kongosho na kusababisha kisukari? Unajua kuwa ajali za barabarani ndiyo chanzo kimojawapo kikuu cha vifo duniani? Unayajua madhara ya pombe? Unajua kuwa kuzama chumvini sasa ni kisababishi kikuu cha kansa ya koo na kinywa?

Pointi yangu ni kwamba ukiamua kupiga mafuruku kila kitu chenye madhara kwa binadamu utajikuta unapiga marufuku karibu kila kitu.

Hitimisho: Binadamu ni kiumbe mwenye utashi. Aachwe aamue mwenyewe kinachomfaa na kisichomfaa ali mrdi halazimishwi na mtu. Na kitakachompata kutokana na maamuzi yake hayo na kimpate tu kwa sababu hakuna namna!
 
babu yangu alivuta hadi 2014 akiwa na miaka 108 tena alikuwa akipiga nyota zile na tumbaku ya kutosha. Madhara yake nafikiri yanatofautiana kabisa maana kuna wazee kabisa wana 90+ na wanapiga fresh tu wala hawaumwi chochote
Watu wa aina ya babu yako katika tafiti huwa tunawaita vighairi (exceptions) na vipo kila mahali. Lakini kuwepo kwavyo hakutengui mahitimisho ya jumla kwamba kihusikacho ni hatari. Ndiyo maana kuna watu hawapati UKIMWI na hata Malaria. Na kuwepo kwao hakutengui ukweli kwamba Malaria na UKIMWI ni hatari.

Na mara nyingi watu kama babu yako wanakuwa na vitu katika DNA zao vinavyowalinda. Au kinga nzuri sana ya mwili. Na kama umevirithi kutoka kwa babu yako hata wewe unaweza kuwa unavuta pakiti mbili za sigara kwa siku bila madhara yo yote....na mwingine akifanya hivyo hata miaka mitano hafikishi tayari anapumulia kwenye mrija katika koromeo...
 
umefafanua vizuri kabisa Mkuu hapa sasa nimekuelewa.
 
Nimekuelewa sanji
Haiko hivyo...

Binadamu amepewa utashi wa kuchagua.

Na ukiangalia vizuri karibu kila kitu kinachozalishwa na binadamu kwa matumizi yake kina madhara. Unajua kuwa mafuta ya kupikia ndiyo chanzo kimojawapo kikuu cha lehemu (cholesterol) inayosababisha kuziba kwa mishipa ya damu na hatimaye kuleta mashambulizi ya kiharusi na moyo? Unajua kuwa ma hamburger haya ya McDonald's na kuku wa KFC ni hatari sana kwa afya yako? Unajua madhara ya soda katika kuharibu ufanyakazi wa kongosho na kusababisha kisukari? Unajua kuwa ajali za barabarani ndiyo chanzo kimojawapo kikuu cha vifo duniani? Unayajua madhara ya pombe? Unajua kuwa kuzama chimvini sasa ni kisababishi kikuu cha kansa ya koo na kinywa?

Pointi yangu ni kwamba ukiamua kupiga mafuruku kila kitu chenye madhara kwa binadamu utajikuta unapiga marufuku karibu kila kitu.

Hitimisho: Binadamu ni kiumbe mwenye utashi. Aachwe aamue mwenyewe kinachomfaa na kisichomfaa ali mrdi halazimishwi na mtu. Na kitakachompata kutokana na maamuzi yake hayo na kimpate tu kwa sababu hakuna namna!
 
Hebu kwanza mtujuze yule jamaa aliyekuwa anaitwa Marboro alikufa na miaka mingapi maana alikuwa anavuta sana
 
Haiko hivyo...

Binadamu amepewa utashi wa kuchagua.

Na ukiangalia vizuri karibu kila kitu kinachozalishwa na binadamu kwa matumizi yake kina madhara. Unajua kuwa mafuta ya kupikia ndiyo chanzo kimojawapo kikuu cha lehemu (cholesterol) inayosababisha kuziba kwa mishipa ya damu na hatimaye kuleta mashambulizi ya kiharusi na moyo? Unajua kuwa ma hamburger haya ya McDonald's na kuku wa KFC ni hatari sana kwa afya yako? Unajua madhara ya soda katika kuharibu ufanyakazi wa kongosho na kusababisha kisukari? Unajua kuwa ajali za barabarani ndiyo chanzo kimojawapo kikuu cha vifo duniani? Unayajua madhara ya pombe? Unajua kuwa kuzama chumvini sasa ni kisababishi kikuu cha kansa ya koo na kinywa?

Pointi yangu ni kwamba ukiamua kupiga mafuruku kila kitu chenye madhara kwa binadamu utajikuta unapiga marufuku karibu kila kitu.

Hitimisho: Binadamu ni kiumbe mwenye utashi. Aachwe aamue mwenyewe kinachomfaa na kisichomfaa ali mrdi halazimishwi na mtu. Na kitakachompata kutokana na maamuzi yake hayo na kimpate tu kwa sababu hakuna namna!
Fact kabisa hii bro ndo maana wanasema adi shida iweze kumtokea mtu kinacho mata Sana hapo ni kwa kiasi gani mtu huyo ametumia hicho kitu

Na ni ngumu kusema kwamba ukivuta sigara leo af ukaacha eti uwe katika hatari ya kupata kansa hii ni uongo

Shida nyingi zinatokea baada ya kuwa expose na kitu flani mara kwa mara
 
Watu wa aina ya babu yako katika tafiti huwa tunawaita vighairi (exceptions) na vipo kila mahali. Lakini kuwepo kwavyo hakutengui mahitimisho ya jumla kwamba kihusikacho ni hatari. Ndiyo maana kuna watu hawapati UKIMWI na hata Malaria. Na kuwepo kwao hakutengui ukweli kwamba Malaria na UKIMWI ni hatari.

Na mara nyingi watu kama babu yako wanakuwa na vitu katika DNA zao vinavyowalinda. Au kinga nzuri sana ya mwili. Na kama umevirithi kutoka kwa babu yako hata wewe unaweza kuwa unavuta pakiti mbili za sigara kwa siku bila madhara yo yote....na mwingine akifanya hivyo hata miaka mitano hafikishi tayari anapumulia kwenye mrija katika koromeo...
iyo kweli kbsa na hii mfano wake ndo Kama ule wa mtu mwenye sickle cell kupata malaria
 
Fact kabisa hii bro ndo maana wanasema adi shida iweze kumtokea mtu kinacho mata Sana hapo ni kwa kiasi gani mtu huyo ametumia hicho kitu

Na ni ngumu kusema kwamba ukivuta sigara leo af ukaacha eti uwe katika hatari ya kupata kansa hii ni uongo

Shida nyingi zinatokea baada ya kuwa expose na kitu flani mara kwa mara
Umepiga mule mule bro 👏👏
 
Hebu kwanza mtujuze yule jamaa aliyekuwa anaitwa Marboro alikufa na miaka mingapi maana alikuwa anavuta sana
Sio kwamba hili ni kampuni la sigara huko america
 
Toa na Elimu namna ya kuacha, si unajua huo ni ulaibu.
Swala la kuacha inakuwa ni jitihada za mtu binafsi maana kwa kila Jambo unalotaka kuliacha au kulianzisha jitihada inabd zianzie ndan ya moyo wako
 
Back
Top Bottom