Uvuvi wa dagaa ziwa Victoria: Mtaji faida na changamoto

Uvuvi wa dagaa ziwa Victoria: Mtaji faida na changamoto

Chambichambi

Senior Member
Joined
May 23, 2022
Posts
139
Reaction score
229
Wadau habari zenu!

Leo naomba nitoe elimu kuhusiana na uvuvi wa dagaa katika ziwa letu pendwa Victoria. Kwa muda kadhaa sasa nipo najihusisha na uvuvi ktk ziwa hili hivyo nimeona niwaletee ukweli wa namna ya kuanzisha hii kazi.

Mtaji kwa kununua vifaa vyako ni kama ifataavyo.
Machine HP 9.9 = TSH 365,0000

Boat Tsh 200,0000

Kokolo la dagaa Tsh 150,0000

Taa Tsh 300,000

Spotlight Tsh 30,000

Vifaa vinginevyo 80,000.

Jumla = 729,0000

Ila unaweza ukaanza na boti ya kukodi kwa gharama ya Tsh 300,000 kwa Giza moja na machine ya kukodi kwa gharama ya Tsh 250,000 hadi Tsh 300,000.

Faida utakata gharama za kila kifaa ambacho mvuvi ameenda nacho kazini kila siku. Mfano

Machine na taa ni Tsh 30,000

Chakula 18,000 na mafuta kwa bei ya Tsh 3,800 per litre. Hivyo faida unapata Tsh 4,000 kwa kila liter. Then pesa inayo baki wewe kama tajiri utachukua nusu yake. Unaona faida hiyo?

Changamoto: Athari za hali ya hewa mfano upepo, badiriko ya bei kila siku, wavuvi kutokuwa waaminifu n.k

Karibuni ktk uvuvi wa dagaa ziwa Victoria kwani ni fursa iliyo na manufaa makubwa sana. Wa mikoani nipo tayari kuwa mwenyeji wako na nitakuelekeza mengi sana. Nipo GOZIBA, MULEBA KAGERA.

KARIBUNI SANA
 
naomba kujua miezi ambayo dagaa wanakuwa kidogo na miezi ambayo wanakuwa wengi?
 
Kwahy mtaji hasa kwa anae kodi boti na mtubwi makadirio yanaweza kuwa ngapi?
 
naomba kujua miezi ambayo dagaa wanakuwa kidogo na miezi ambayo wanakuwa wengi?
Dagaa waga wanakuwa wengi kulingana na kina cha maji. Mfano kuanzia mwezi 9 hadi mwezi 4 dagaa wanakuaga wengi karibia maeneo yote ila kwa mkoa wa Kagera wa bei inadhiriwa na mvua. Ila kuanzia mwezi 5 hadi 8 visiwa vya GOZIBA, Ukara, Ghana na kasarazi dagaa inakuwepo na bei inakuwa juu kwa kuwa ni wakati wa kiangazi. Pia kwa mwezi wa 7 kisiwa cha bwiro waga dagaa ina kuwa karibu sana.
 
Dagaa waga wanakuwa wengi kulingana na kina cha maji. Mfano kuanzia mwezi 9 hadi mwezi 4 dagaa wanakuaga wengi karibia maeneo yote ila kwa mkoa wa kagera wa bei inadhiriwa na mvua. Ila kuanzia mwezi 5 hadi 8 visiwa vya GOZIBA, ukara, Ghana na kasarazi dagaa inakuwepo na bei inakuwa juu kwa kuwa ni wakati wa kiangazi. Pia kwa mwezi wa 7 kisiwa cha bwiro waga dagaa ina kuwa karibu sana.
Chief habari za huko, aiseee long time sana toka nifike Kasarazi mwaka 2013
 
Mkuu hiyo Machine 9.9hp ile bei ni mpya Dukani?Na ni Jina gani Yamaha au nyingine?Kwa nini umechagua 9.9hp?
 
Mkuu habari ya Gozba, kama Kuna watu wanahitaji Yamaha Outboard engine 15hp used za Dubai na South Africa Kwa 4million utanicheki. Nikija huko nitakutafuta
 
Back
Top Bottom