Wadau habari zenu!
Leo naomba nitoe elimu kuhusiana na uvuvi wa dagaa katika ziwa letu pendwa Victoria. Kwa muda kadhaa sasa nipo najihusisha na uvuvi ktk ziwa hili hivyo nimeona niwaletee ukweli wa namna ya kuanzisha hii kazi.
Mtaji kwa kununua vifaa vyako ni kama ifataavyo.
Machine HP 9.9 = TSH 3650000
Bot Tsh 2000000
Kokolo la dagaa Tsh 1500000
Taa Tsh 300000
Spotlight Tsh 30000
Vifaa vinginevyo 80000.
Jumla = 7290000
Ila unaweza ukaanza na boti ya kukodi kwa gharama ya Tsh 300000 kwa Giza moja na machine ya kukodi kwa gharama ya Tsh 250000 hadi Tsh 300000.
Faida utakata gharama za kila kifaa ambacho mvuvi ameenda nacho kazini kila siku. Mfano
Machine na taa ni
Tsh 30000
Chakula 18000 na mafuta kwa bei ya Tsh 3800 per litre. Hivyo faida unapata Tsh 4000 kwa kila liter. Then pesa inayo baki wewe kama tajiri utachukua nusu yake. Unaona faida hiyo?
Changamoto: athari za hali ya hewa mfano upepo, badiriko ya bei kila siku, wavuvi kutokuwa waaminifu n.k
Karibuni ktk uvuvi wa dagaa ziwa Victoria kwani ni fursa iliyo na manufaa makubwa sana. Wa mikoani nipo tayari kuwa mwenyeji wako na nitakuelekeza mengi sana. Nipo GOZIBA, MULEBA KAGERA.
KARIBUNI SANA