Uvuvi wa dagaa ziwa Victoria: Mtaji faida na changamoto

Mkuu mimi nataka tufanye biashara,uwe unanitumia dagaa huku niliko.nimejaribu kufata mwenyewe gharama imekuwa kubwa sana nashindwa kupata faida.huwa nafata kasalazi na gembale.kama uko tayari nijulishe mkuu tufanye kazi
 
Mkuu mimi nataka tufanye biashara,uwe unanitumia dagaa huku niliko.nimejaribu kufata mwenyewe gharama imekuwa kubwa sana nashindwa kupata faida.huwa nafata kasalazi na gembale.kama uko tayari nijulishe mkuu tufanye kazi
Upo mkoa gani mkuu? Vipi kama unaweza ukaja mwisho wa giza tukaonana mwanza ili kuzungumza zsidi?
 
Wakuu,
Mimi ninafikilia kuanzisha Kampuni yangu, nataka kununua samaki Mwanza kutoka kwa wavuvi, niwakaushe kwa Oven na kuwakaanga kwa kutumia Air fryer alafu niwa pack kwenye package moja moja ,kwa mfano, Sato mmoja awe kwenye package yake na dagaa fungu la Tsh 5000, 2000 nk alafu nipeleke super market na madukani

Swali langu sasa kwenu, je biashara hii italipa ? Je mna ushauri wowote wa kuboresha hili wazo langu ? .kwa kifupi ni mnanishauri nini juu ya hili wazo ?

Oven na Air fryer naweza kununua,
N.B
Target yangu ni mkoa wa Arusha, Singida, Dodoma na wilaya ya Moshi kwa kuanzia
 
Hii biashala inalipa ila kikubwa ni kwamba je soko umelifanyia utafiti uliothabiti, na kama umelifanyia utafiti basi utawez kufany biashala hii vyema kabisa ila changamoto ni kwamba je watakapokuwa wanafunga ziwa kwaajili sangala sato, na hata dagaa utakuwa na ww unasimama mpaka wafungue ziwa ama inakuwaj
 
Mkuu, kwa utafiti wangu mdogo niliofanya ni kwamba mikoa hiyo ina shida ya upatikanaji wa samaki au tuseme kuna uhitaji wa samaki, lakini mimi sasa kichwani mwangu ninawaza niifanye hii biashara kwa mtindo wa kiwanda kidogo yaani nisiuze hao samaki wa kukaanga na kubanika kwenye masoko haya ya kawaida,nimevutiwa zaidi na supermarket ,maduka au hata kufungua fish point/fish butcher

Tukirudi kwenye swali uliloniulieza, kwanza kabisa sina ufahamu na hicho kitendo cha kufunga ziwa, ningependa unieleweshe,lakini kama kina maanisha kwamba hakutokuwa kuna upatikanaji wa samaki, tunarudi kule kwenye wazo langu,mimi nataka kufungua kiwanda kidogo sana yani kama hao samaki kuna miezi hawatopatikana mimi nitawanunua kwa wingi kipindi wanapatikana na kuweka kwenye freezer ndipo hapo nitawagawa, wa kuuza fresh na kuuza smoked na fried naamini stock yangu inanitosha kuendelea biashara kipindi upatikanaji ni mdogo

Nitashukuru sana ukinisaidia kuboresha wazo langu la biashara, usisite kunishauri ,lifanye kama ni wazo lako ungefanyaje hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…