SoC02 Uwajibikaji katika kutunza hadhi ya Familia pamoja na kuhudumia ndugu

SoC02 Uwajibikaji katika kutunza hadhi ya Familia pamoja na kuhudumia ndugu

Stories of Change - 2022 Competition

Z K Ahmad

Member
Joined
Mar 16, 2019
Posts
29
Reaction score
36
Suala la kuwajibika ni muhimu sana unapokuwa kiongozi Katika Familia, Hususani Baba, Mama, Kaka au Dada. Kwani Sio baba pekee ndio anaetakiwa kuwajibika kwa maana hata Mama pia huwajibika kwa nafasi yake kama mlezi na mshauri kwa mume na Watoto wake, ndipo nafasi ya dada pamoja na kaka vilevile hutokea Katika kuwajibika hukohuko ili kuwaongoza Ndugu zake Katika misingi Bora yakimaisha na hii huchangia kwa kiasi kikubwa Ndugu kumjali Ndugu mwengine na Mara kadhaa kufanya hata wapate moyo wakuwahudumia iwapo watakuwa wamekwama.

Haya ni baadhi ya mambo muhimu ambayo yanafaa kuzingatia Katika kuwajibika kwenye kutunza familia pamoja na kuhudumia Ndugu.

01. Kujitoa: Nikianza na mfano mzuri wa Baba ambae ndo kichwa cha familia, Mama ambae atasimama Kama nguzo ya familia, Kaka na dada wakisimama nakuwajibika Kama Mipaka ya familia.

Hawa wote iwapo watajitoa ipasavyo kwenye kuwajibika basi hakuna familia itakayoyumba hata Kama ikitokea mmoja ameondoka (amefariki). Baba anao wajibu wakuhakikisha familia inapata matunzo mazuri Kama malazi, mavazi na makazi ambayo yatakuwa sababu nzuri ya kupata huduma zinazostahili, isitoshe mama nae anaweza kuwajibika vilevile Kama baba lakini Kama itatokea vinginevyo kutokana na hali za familia zetu nyingi zakimasikini basi mama wa nyumbani yeye Kama nguzo, anatakiwa kuhakikisha anawajibika kwa mume wake (baba), anakuwa kwenye hali nzuri kimuonekana wakati anapoenda kutafuta kwaajili ya familia.

Upande wa kaka na dada wote wanatakiwa kujitoa katika kushauriana wao kwa wao katika mienendo mizuri na hata wao na wazazi wao, hutokea familia kadhaa hawapati muda wakukaa pamoja kujadili mienendo ya wanafamilia kiujumla Hali ambayo upelekea familia kuwa na mikwaruzano.

02. Heshima au Nidhamu: Msingi mkubwa wakujenga familia zenye kuwajibikika na Kupata huduma nzuri zitakazofanya kila mmoja Ndani ya familia ajione mwenye furaha Ni heshima, Heshima Ambayo kila mwanafamilia analo jukumu yakuilinda.

Kwa upande wa Baba anapomuheshimu mke wake (Mama), basi furaha huzidi ndani ya nyumba hata kumfanya Mama aweze kuwajibika ipasavyo katika kila Jukumu linalomuhusu, vilevile hata Mama Akiwa na Nidhamu kwa Mumewe, yaani Mfano amerudi kazini akampokea kwa maneno mazuri yenye kunfariji itafanya mume azidi kumuheshimu mke, Hali hii itafanya kila mmoja kuwajibika kwa Juhudi kubwa kuhakikisha huduma zote zinapatikana, Hususani za kutunzana Kama wanafamilia.

Watoto nao wazazi inabidi wawaangalie Sana kwenye malezi yao, baadhi ya familia wanawakuza Watoto kwakuwadharau wengine, Jambo ambalo mtoto hata akikua nalo hawezi kujua nani anapaswa kumpa heshima yake Kama inavyostahili, hili linasikitisha sana kwani Watoto wa namna hiyo huwa wanakosa maelewano mazuri hata na Ndugu zao, kiasi wanashindwa kuwapa huduma za mahitaji yoyote wanapokwama.

03. Kujali: Mambo mengi Ndani ya familia huvurugina kutokana na kutokujali kwa hata Jambo dogo tu, Mke au Mume Anaposhindwa kuthamini au kujali Jambo lolote hata Kama kiwe na udogo vipi lazima kutatokea upande mmoja kushindwa kuwajibika, Familia nyingi zimekuwa na mazoea yakutokujali mwengine anahitaji Nini, Mfano Baba asipojali Watoto wake hii itapelekea Watoto wamuone mama ndo kila kitu hata Kama kuna matumizi Ambayo baba hutoa kwa mama Kisha mama akawapatia Watoto, Mzazi kwa namna yoyote unawajibika kuwasikiliza Watoto wanahitaji Nini na kwa wakati gani hii itasaidia waone Kuwa Unawajibika hata kwa kidogo utakachokitoa.

Pia Ndugu nao wanapaswa kufanya hivyo, jitahidi Sana kuijali Hali au shida au wazo la Ndugu yako katika Jambo lolote lenye tija katika kuwajenga, na kwakufanya hivyo mnaweza pia kuelimishana lipi linafaa na lipi halifai.

04. Kujenga Msingi mzuri wa Maelewano na mawasliano: Katika jamii inayotuzunguka, familia kadhaa zimekuwa zikijitahidi lutengeneza mahusiano na mawasiliano mazuri baina ya Ndugu kiasi hufanya waweze kuwajibika kwa pamoja katika kusaidiana na kuhudumiana panapohitajika.

Tuweze kuona na kuiga msano mzuri wa familia hizi, ambapo hata ikitokea baba au mama hayupo Bado dada, kaka na wadogo hushikamana na huwajibika sawa na walivyokuwa wakiwajibika Katika kipindi cha familia yote ipo pamoja.

Kuna Yale mazoea ambayo baadhi ya watu hujijengea, kwamba akishatoka kwenye familia kwenda kutafuta hakumbuki nyuma, Ninashauri Kuwa hilo Sio Jambo zuri unapotoka kwenda kutafuta kwaajili ya kesho yako, ikumbuke na Jana yako Ambayo ndiyo iliyokulea na kukukuza mpaka ulipofikia.

05. Usawa: Jambo la mwisho lakuzingatia Ni usawa wa majukumu na uwajibikaji, Leo hii Kama Hali ya dunia na ustaarabu wake ilivyobadilika, wanawake wanahitaji kuwepo na usawa ili nao wasiwe wanaonewa Kama ilivyokuwa hapo nyuma, basi usawa huu wanaouhitaji itawapasa waungalie kwa umakini Katika kuwajibika kweo kwenye familia.

Wamama Katika malezi yao wasiwapendelee Watoto au kuwadanganya nakuwaaminisha Watoto vinginevyo mpaka ikafika hatua Watoto wakachukia wazazi wao wakiume. Vilevile akina baba hawatakiwi kuwapendelea Sana Watoto wakike au wakiume pekee Bali wawajali wote na huko ndipo kuwajibika kunapotakiwa, ili Watoto wapate malezi Bora wakati wote.

Napenda nakumalizia kwakusema mambo kadhaa:-

Kila mmoja Ndani ya familia anao wajibu wa kuwajibika Katika kutunza hadhi ya Jamii Kama ilivyo kubomoa Heshima ya familia inawezekana kwa urahisi kutokana na kukosa nidhamu baina ya wanafamilia.

Tushikamane ili limapotokea tatizo tuweze kusaidiana kulitatua kwa pamoja, Nidhamu, Usawa, Haki, Kujali na Kujitoa Ni Mambo ya msingi kuzingatiwa ili kuziweka Jamii na familia Pamoja. Mawasiliano na Maelewano Mazuri Ni tunu Katika kukuza Na kuendeleza undugu hata Kama Kichwa na Nguzo Za Familia Hawatokuwepo.

Tupendane Ahsanteni sana.

IMG-20220409-WA0001.jpg
 
Upvote 2
Back
Top Bottom