SoC03 Uwajibikaji kwenye kutunza mazingira

SoC03 Uwajibikaji kwenye kutunza mazingira

Stories of Change - 2023 Competition

Chalala04

New Member
Joined
Jun 24, 2023
Posts
4
Reaction score
4
Mazingira ni kitu chochote kinachomzunguka binadam
Uchafu ni kitu chochote kilichokaa sehemu isiyo sahihi
Kutunza mazingira ni kuweka Kila kitu kwenye sehemu yake, (sehemu sahihi)
Kwa kiasi kikubwa nchi yetu haina elimu ya kuhifadhi mazingira mfano unaweza ona mtu anatupa ganda la pipi bila kujali hata kama anaona sehemu sahihi ya kuweka taka

Changamoto za Kutunza mazingira

1. Upungufu wa elimu, jamii yetu kwa kiasi kikubwa hawana elimu ya juu ya utunzaji mazingira, namna ya Kutunza mazingira, athari na faida

2. Kuna Upungufu wa sehemu za kutupa taka, sehemu za kutupa taka imekuwa changamoto kubwa, mfano unaweza tembea hata kwa mbali mrefu bila kukuta pipa za taka

3. Kutobadilisha ya matumizi au kurudia matumizi (recycling), hii ni mbinu rahisi zaidi ya Kutunza mazingira mfano, unaweza tumia mabaki ya chakula cha binadam kwa kutengeneza chakula cha mifugo na kinyesi cha mifugo kutengeneza mbolea

Maoni
1. Kutoa elimu ya mazingira, kwenye elimu hapa tuzingatie, mbinu za Kutunza mazingira, umuhimu wa kutunza mazingira nk
2. Kutenga maeneo/mapipa ya taka ili iwe rahisi mtu Kutunza taka hata akiwa mbali na nyumbani kwako
3. Taka kuzirudisha kwenye matumizi mfano, karatasi kuna uwezekano wa kutengeneza maua hivyo bidhaa nyingi zinaweza kutengenezwa kutokana na taka
4. Kutunga sheria zinazo tekelezeka, sheria na kanuni za mazingira walio wengi hawazijuhi hivyo lazima wasimamie kwenye utekelezaji, sheria na kanuni kama zifuatiliwa basi uwajibikaji utakuwa mkubwa kwa Kila mtu msimamia sheria na hata wanaotakiwa wazitekeleza watawajibika
 
Upvote 1
Back
Top Bottom