Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Uwajibikaji wa kidemokrasia umejikita kwenye kanuni tatu ambazo zinawawezesha wananchi na wawakilishi wao—wadai haki—
kuwawajibisha maafisa wa umma na sekta binafsi wenye wajibu wa kutoa huduma, ambao kwa maneno mengine, wanaitwa ‘wawajibikaji’. Kanuni hizo tatu ni uwajibikaji, usikivu, na utekelezaji.
Kanuni hizo zitawasaidia wathamini kubainisha mazingira yaliyopo au kama yanaweza kuboresha zaidi mahusiano ya kiuwajibikaji. Kama ilivyoelezwa, wathamini ni lazima wathibitishe kama kanuni zinafuatwa katika mwingiliano halisi wa kikazi kati ya wawajibikaji na wadai haki.
Uwajibikaji unapima kiwango ambacho serikali inatekeleza majukumu yake katika kuelezea na kuhalalisha maamuzi yake kwa
umma. Ufanisi mkubwa wa uwajibikaji unaanishwa kwa namna ambavyo wadai haki wanaelezea mahitaji yao, lakini pia unahusiana na nafasi, uwezo na utayari wa maafisa kuwajibika kwa matendo yao.
Kwa mfano, sheria za uchaguzi (kanuni za uchaguzi au za wilaya) au sheria za mashirika za kuajiri, kusimamia na kuwafukuza kazi watumishi wa umma ambao ni wa kuchaguliwa na wasio wa kuchaguliwa, kila mmoja anapaswa kuwajibika.
Usikivu unahusiana na ama maafisa wa serikali wanapanga muda wa kukusanya maoni ya wananchi au wawakilishi wao kabla sera au sheria haijapitishwa rasmi, ili maudhui ya maamuzi hayo yatokane na maoni yao na matakwa ya wananchi au kanuni za haki za binadamu (International IDEA 2008: 24).
Kwa kiasi kikubwa, motisha ya kisiasa kwa serikali kuwa sikivu kwa wananchi inategemea na mfumo wa vyama, sheria za uchaguzi, pamoja na taratibu nyingine za kitaasisi. Motisha pia inaweza kuathiriwa na upatikanaji wa nyenzo za kiteknolojia, rasilimali watu au fedha. Usikivu pia unaweza kujionesha kupitia mwingiliano usio rasmi baina ya wawajibikaji na wadai haki, kama vile tafiti za kitaifa za maoni, mikutano ya siri, kampeni za utetezi au maandamano.
Utekelezaji ni kuhusiana na matokeo rasmi au yasiyo rasmi ambayo wawajibikaji wanaweza kukumbana nayo na kulazimika kuwajibika kutokana na matendo yao. Uwezekano wa kutoa adhabu na tuzo unachangia kuboresha uwajibikaji. Adhabu au tuzo hizo zinaweza kuwa zimeainishwa kisheria au zikakubalika isivyo rasmi kutumika kutokana na mazoea.
Baadhi ya wadai haki wanaweza kuwa na mamlaka ya kutekeleza adhabu au tuzo hizo, kama ilivyo, taasisi kuu za ukaguzi wa hesabu ambazo zina mamlaka ya kisheria na kiutawala katika kutoa hukumu, kamati za bunge zina mamlaka ya kuagiza kufanya mabadiliko katika sera, au mahakama yenye mamlaka ya kubatilisha mchakato wa uchaguzi uliotawaliwa na ulaghai na udanganyifu.
Wadai haki wasio na mamlaka rasmi ya kutekeleza hukumu (kama vile makundi ya wananchi, kamati za bunge zisizo na mamlaka ya kuhoji zaidi, au ofisi ya malalamiko katika baadhi ya nchi) wanapaswa kushirikiana na taasisi zilizopewa mamlaka kushinikiza utekelezaji. Uwezo wa kifedha na uhuru wa kisiasa wa taasisi hizo vinaathiri uwezekano wa kutekeleza jukumu hili
Ushiriki na uwazi unaweza kuchangia kufanikisha kanuni hizi tatu za demokrasia. Ushiriki unahusu haki ya wananchi kushirikiana, kukusanyika, kutoa maoni na kuwa na sauti katika mchakato wa sera. Uwazi ni upatikanaji wa taarifa sahihi, zilizo wazi, na zinazopatikana kwa urahisi kuhusu utendaji, mpango, usimamizi na ahadi kati ya serikali na wananchi au kati ya wakala mmoja wa serikali na mwingine.
Unapotathmini kanuni hizi na jinsi zinavyohusiana na taratibu za uwajibikaji, ni lazima kuchunguza iwapo misingi hii inatumika kwa usawa, au makundi fulani katika jamii yanatengwa au kubaguliwa.
Pia, motisha ya kisiasa kwa wanasiasa na kushindwa kwa mifumo ya siasa kuwakilisha wananchi ni mambo muhimu ya kuzingatia. Kwa mfano, je wanawake wana uwezo na nafasi sawa kama wanaume katika kupata majibu kutoka kwa wawajibikaji?
Je, viongozi wa serikali ni wasikivu kwa wananchi masikini kama ilivyo kwa matajiri?