JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Tunaweza kusema kuwa kuna uwajibikaji wa kidemokrasia katika utoaji huduma pale ambapo wananchi au wawakilishi wao wanahoji au kutoa mrejesho kuhusu huduma za umma halafu watendaji wa kisiasa na watoa Huduma ama wayafanyie kazi maoni hayo au wawajibishwe.
Kutokana na dhana hiyo ya msingi, uwajibikaji unabeba uhusiano kati ya watendaji wa aina mbili:
Wawajibikaji ni maafisa wa kuchaguliwa na wasio wa kuchaguliwa au watoa huduma wa sekta binafsi wenye mamlaka na wajibu wa kufanya kazi yao na kutoa maelezo na kuhalalisha matendo yao na pia wanaoweza kuwajibishwa kwa matendo yao, mazuri au mabaya.
Wadai haki ni wananchi au Taasisi za kisiasa zinazowawakilisha wananchi na zenye haki au mamlaka ya kuangalia/kusimamia
Upvote
1