Uwajibikaji wa kidemokrasia

Uwajibikaji wa kidemokrasia

Eliud Ambrose

New Member
Joined
Sep 21, 2021
Posts
4
Reaction score
3
Dhana za Tathmini

Kwa maana ya jumla, kwa watu wengi duniani, demokrasia maana yake ni nguvu ya wengi katika kufanya maamuzi yanayohusu umma na kuweka usawa wa kisiasa katika matumizi ya nguvu hiyo (International IDEA 2008: 20-21). Demokrasia ni lazima iwape wananchi uwezo wa kujieleza na kuwasilisha hoja zao kwa utaratibu mzuri unaowafikia wawakilishi wao. Wazo la msingi ni kwamba kuwepo kwa mifumo ya uwajibikaji katika demokrasia kuhakikisha maafisa wa serikali kutoa huduma za viwango vya juu kabisa kwa watu, vinginevyo wanawajibishwa ipasavyo ikiwa hawatafanya hivyo.

Maafisa wa serikali wanapowajibishwa, na misingi ya kidemokrasia inapoheshimiwa na kufuatwa kuna uwezekano mkubwa wa huduma za umma kuboreshwa, kwa haraka, kwa wakati muafaka, kwa ubora wa juu au kutekelezwa vizuri zaidi. Mbinu hii inayoongozwa na wananchi wenyewe katika kutathmini uwajibikaji wa kidemokrasia katika utoaji wa huduma, imejikita kwenye imani kwamba raia wa nchi husika wapo katika nafasi nzuri ya kutathmini iwapo hali ya kidemokrasia katika nchi yao inafanana na mawazo yao na inakidhi matarajio yao. Aidha, utaratibu huu umebeba mbinu kadhaa zilizounganishwa zenye lengo moja la kuleta mabadiliko.

1.1. Uwajibikaji wa kidemokrasia ni nini?

Kuwawajibisha maafisa wa serikali ni kitovu cha demokrasia. Uwajibikaji wa kidemokrasia unawapa wananchi na wawakilishi wao
nafasi na njia ya kutoa maoni yao na kupatiwa maelezo kuhusu utendaji kazi wa maafisa wa kuchaguliwa na wale wasio wa kuchaguliwa, na inapobidi wanashauri hatua za kuchukua kwa maafisa walioshindwa kutekeleza majukumu yao.Dhana ya uwajibikaji wa kidemokrasia inajumuisha vyote viwili uwajibikaji wa kisiasa na ule wa kijamii—iwe moja kwa moja au kinyume chake,kwa wima, kwa ulalo au kimshazali au kwa namna yoyote ile iliyo katika msingi mkuu wa kidemokrasia wa nguvu ya wengi katika maamuzi yanayohusu umma. Uwajibikaji wa kidemokrasia unajumuisha uwezo wa wananchi wa kuelezea.

Matakwa yao ili kushawishi maamuzi, kwa mfano, kupitia michakato ya uchaguzi. Njia nyingine za kidemokrasia ni pamoja na maandamano, habari za kiuchunguzi, mikakati ya kibunge, midahalo ya umma au kura za maoni. Uwajibikaji wa kidemokrasia pia unahusu mbinu ambazo sio za moja kwa moja, kama vile mfumo wa kuchunguzana na kurekebishana pamoja na taratibu nyingine zinazotumika kwenye taasisi moja moja ili kushawishi uendeshaji wa nchi.

Mifano ya mbinu hizo ni usikilizaji wa kesi katika kamati za kibunge, maswali yanayoulizwa na vyama vya siasa vya upinzani pamoja na mapitio au uchunguzi unaofanywa na ofisi ya uchunguzi wa malalamiko ya wananchi au taasisi kuu za ukaguzi wa hesabu za seikali, n.k. Uwajibikaji siyo sifa inayoishia kwenye demokrasia tu bali uwajibikaji unapokuwa wa kidemokrasia, unasaidia sana kuboresha utendaji wa serikali. Hivyo, kwa kutumia istilahi uwajibikaji wa kidemokrasia, mwongozo huu unalenga kujenga dhana iliyojumuisha yote, pana na ya msingi kabisa badala ya dhana baguzi, finyu na yenye mipaka.

1.2. Uwajibikaji wa kidemokrasia unafanyaje kazi katika utoaji wa huduma za
umma?

Tunaweza kusema kuwa kuna uwajibikaji wa kidemokrasia katika utoaji huduma pale ambapo wananchi au wawakilishi wao wanahoji
au kutoa mrejesho kuhusu huduma za umma halafu watendaji wa kisiasa na watoa huduma ama wayafanyie kazi maoni hayo au
wawajibishwe. Kutokana na dhana hiyo ya msingi, uwajibikaji unabeba uhusiano kati ya watendaji wa aina mbili:

• Wawajibikaji ni maafisa wa kuchaguliwa na wasio wa kuchaguliwa au watoa huduma wa sekta binafsi wenye mamlaka na wajibu wa
kufanya kazi yao na kutoa maelezo na kuhalalisha matendo yao—na pia wanaoweza kuwajibishwa kwa matendo yao, mazuri au mabaya.

• Wadai haki ni wananchi au taasisi za kisiasa zinazowawakilisha wananchi na zenye haki au mamlaka ya kuangalia/kusimamia utendaji wa wawajibikaji, kuwahoji na kuwahukumu pamoja na kutoa adhabu inapohitajika.2 Mifano ya wawajibikaji na wadai haki Wawajibikaji wanaweza kuwa serikali ya nchi au ofisi ya manispaa, wizara, ofisi ya uchunguzi wa malalamiko, kamati ya bunge, bunge lenyewe, shirika binafsi, au ofisi yoyote ya umma au binafsi au shirika lililopewa mamlaka ya kutoa huduma. Kwa kawaida mamlaka hayo yanakuwa chini ya zaidi ya mdau mmoja.

Kwa upande mwingine, wananchi ni mfano mzuri zaidi wa wadai haki. Kwa sababu wao ndio wanaowapa mamlaka wawajibikaji na pia mara nyingi wanalipia huduma wanazopata. Mifano mingine ya wadai haki ni vyama vya kisiasa vya upinzani, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, kamati ya bunge yenye wajibu wa kusimamia utekelezaji wa sera za serikali, au watendaji mbalimbali wa kisiasa na kijamii wenye mamlaka ya kuwasimamia wale wenye wajibu wa kutoa huduma. Mara nyingi demokrasia hudhaniwa kuwa inapokuwepo basi na mifumo ya uwajibikaji inakuwa inafanya kazi pia. Kwa uhalisia dhana hii ni changamani zaidi. Aina mbalimbali za mivutano, makundi na mazingira halisi huathiri namna huduma zinavyotolewa na jinsi mfumo wa uwajibikaji unavyofanya kazi. Mara nyingi taratibu hizo huwa hazipo kabisa, hazifai au zinabagua kwa misingi ya utambulisho (kama vile, ubaguzi kwa misingi ya lugha, kabila, dini au jinsia), mwelekeo wa jinsi,3 umri, kipato, ulemavu au mamlaka.

Uwezo wa bunge kama mdai haki Uezo na nafasi ya bunge katika kuiwajibisha serikali kuu unategemea kwa mfano, taratibu za ndani za kuwajibishana ndani ya bunge na baina ya bunge, serikali kuu pamoja na mahakama. Sababu nyingine za msingi zinazoweza kuathiri ni ufanisi na uwezo wa kamati katika kupata, kuchambua na kufanyia kazi taarifa, na namna ambavyo kamati husika zimeundwa na wanasiasa wanaojali maendeleo, na maafisa wenye uwezo mkubwa kiutendaji.Nafasi ya wananchi kudai uwajibikaji Kuna nafasi nyingi ambazo wananchi wanaweza kuzitumia kutoa hoja zao na kudai uwajibikaji wa maafisa, kwa mfano kupitia michakato ya uchaguzi, upitishaji wa wagombea ndani ya vyama, mitandao ya kijamii, maandamano, migomo, mikutano ya hadhara na nyingi nyinginezo. Nafasi hizi na nyinginezo ni majukwaa muhimu kwa kupaza sauti zao, kujenga mifumo itakayokuza uelewa wa wananchi na kuhakikisha majibu yanapatikana.

Mwongozo huu, kwanza unasaidia kutathmini iwapo mifumo ya uwajibikaji kati ya wawajibikaji na wadai haki inafanya kazi vizuri katika mchakato mzima wa sera itakayosaidia utoaji wa huduma za umma, na pili, kubuni hatua ambazo zitasaidia kuboresha mifumo hiyo ya uwajibikaji.

1.3. Ni Hatua gani za Sera Zinazohusiana na Uwajibikaji wa Kidemokrasia?

Utoaji wa huduma kwa umma, kama vile maji safi na salama ya kisima au ya bomba ni hatua ya mwisho katika mchakato changamani unaohusisha wanasiasa, maafisa wa serikali, wananchi au wawakilishi wao, harakati za kijamii, makundi ya watu wenye maslahi ya pamoja na sekta binafsi. Mchakato wa sera ni mrefu unaohusisha watu na ofisi nyingi. Unaweza kuanzia kwenye vipaumbele vilivyowekwa na ukaguzi wa wakala wa ufuatiliaji na ukaguzi, paneli la wahariri, uchambuzi wa kina wa vyombo vya habari kuhusu mpango wa taifa unaosimamiwa na wizara, hadi kufikia kwenye makubaliano kuhusu taratibu na sheria za kusimamia huduma, kwenda kwenye utekelezaji wa sheria hizo katika utoaji wa huduma na matumizi ya huduma hizo.

Hivi ndivyo mchakato wa sera ulivyo. Mwongozo huu unajikita katika hatua tatu kuu za mchakato huu:

• Kupanga ajenda ni hatua ambayo masuala au kero zinakuwa vipaumbele kwa wananchi, wanasiasa, viongozi au vyombo vingine binafsi au vya kimataifa ambavyo vinatengeneza ajenda ya umma. Vipaumbele vinaweza kuelezwa kupitia kampeni za uchaguzi, mijadala ya umma na mikutano ya kimataifa, vilevile mikutano baina ya maafisa wa serikali na wa sekta binafsi. Katika mazingira halisi, upangaji ajenda unaweza kuathiriwa na ripoti rasmi kutoka vyombo vya usimamizi,, kama vile wakala wa serikali wa udhibiti, ofisi ya
mchunguzi wa malalamiko, taasisi kuu ya ukaguzi, au kupitia uteteziwa wanaharakati na makundi ya watu wenye maslahi ya pamoja. Jinsi ambavyo masuala yanakuwa vipaumbele na nani anayapatia msukumo, ni maswali ya msingi kuhusu mamlaka, nguvu na ushawishi.

Mifano ya kupanga ajenda:
− tathmini za sekta au huduma, mapitio au kaguzi zinazofanywa, kwa mfano, ofisi ya mchunguzi wa malalamiko au kamati za bunge;
− matukio ya kampeni za uchaguzi kama vile mijadala na uzinduzi wa ilani za vyama;
− mikutano ya mara kwa mara au mikutano maalum ya vyama vya siasa;
− vikao vya bajeti au uangalizi wa matumizi ya bajeti pamoja na mijadala husika katika bunge na vikao vya mabaraza ya madiwani katika halmashauri;
− midahalo, maoni ya wahariri, na ripoti maalum au habari nyinginezo zinazotangazwa na vyombo vya habari;
− kampeni za wanaharakati wa kijamii na makundi ya watu wenye maslahi ya pamoja;
− mijadala ya uandaaji wa mpango wa maendeleo wa taifa;
− mapitio ya kubadilisha katiba;
− harakati za vyama vya wafanyakazi, jumuiya za wasomi mbalimbali, watoa huduma wa sekta binafsi na taasisi za serikali za mitaa;
− mashauri katika bunge la taifa na katika mabaraza ya serikali za mitaa;
− maandamano ya amani pamoja na migomo ya watumiaji wa bidhaa au huduma.

• Utungaji sera ni hatua ambapo wawakilishi au viongozi wanapima mapendekezo ya sera ili kuamua mapendekezo ambayo yanaweza
kutekelezeka na kuyabadili kuwa sheria. Hatua hii inajumuisha makubaliano baina ya wanasiasa wa vyama tofauti vya kisiasa pamoja na wawakilishi wa makampuni binafsi, mashirika ya kujitolea na yale ya kijamii, wafadhili, na makundi mengine yenye maslahi na matokeo ya sera husika. Hili huwa linahusisha kufikia maafikiano kati ya ufanisi wa vipaumbele, vipaumbele vya kisiasa na mgawanyo wa rasilimalifedha. Kimsingi, utungaji sera unaweza kuchangiwa kwa mawazo pia kutoka katika vyombo vya ufuatiliaji na usimamizi.
Mifano ya utungaji sera:

− mijadala ya wazi na upigaji kura kwa ajili kurekebisha sheria au
kutunga sheria mpya, inayofanywa katika vikao vya bunge la
taifa au vikao vya mabaraza ya halmashauri; − hukumu na maamuzi ya mahakama;
− maamuzi ya serikali na mipango kazi;
− utetezi wa makundi ya maslahi ya pamoja kwa serikali pamoja na
vyombo vingine vya maamuzi;
− wakala maalum wa serikali anayeandika rasimu za sera za kiseta
na vipaumbele; na
− mipango ya serikali kuu inayopelekwa kuchunguzwa na kujadiliwa na bunge au mabaraza ya serikali za mitaa.

• Utekelezaji hufanyika pale serikali inapoagiza wakala wa sekta ya umma au binafsi kutekeleza sera kwa matendo na kwa kutoa huduma husika. Katika hatua hii rasilimali zilizotengwa zinaelekezwa kwenye matumizi yake husika na huduma zinapaswa kutolewa kwa watu.

Mifano ya utekelezaji sera ni hii ifuatayo:

− kupeleka mgao wa bajeti katika ngazi tofauti tofauti za serikali ili kuwezesha utoaji huduma;
− makubaliano ya huduma itakayotolewa kati ya serikali na watoa huduma wa sekta binafsi;
− kupanga bei na mifumo ya ukusanyaji malipo na kodi mbalimbali;
− kuweka mipango ya miundombinu ya huduma na namna ya kufanya kazi;
− kuweka mifumo ya usambazaji na ugavi, kama vile mifumo ya maji, umeme, gesi au chakula;
− manunuzi ya serikali ya bidhaa na huduma, kama vile madawa, vitabu vya shule, magari au matengenezo;
− taratibu za kuajiri wafanyakazi, kama vile kupima maarifa/sifa za kuajiri waalimu, sheria za uajiri na mifumo ya ulipaji mishahara
− huduma kwa watumiaji na mifumo ya utoaji maoni kuhusu ubora wa huduma;
− huduma bora ya afya, usalama, kutokuwepo ubaguzi, rushwa pamoja na utunzaji wa mazingira;
− maafisa wa serikali wanaoshughulikia maombi ya hati-miliki kutoka kwa watu mbalimbali;
− Maafisa kilimo kutoa ushauri wa bure kwa vyama vya wakulima.Mchakato wa usimamizi, ufuatiliaji na tathmini unaleta malalamiko katika mijadala ya umma, na hivyo ili kuziba pengo katika mchakato wa sera katika kupanga ajenda: kwanza, malalamiko yanabadilika kuwa vipaumbele, na kisha machaguo ya kisiasa yanaweza kufanywa na utekelezaji wa sera unaweza kufuatia.

Baada ya mapitio, ukaguzi au tathmini katika mzunguko wa sera, matokeo, mijadala na marekebisho vinajumuishwa katika awamu mpya ya kupanga agenda. Usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa huduma vinaweza kuanzia juu kushuka chini, kupitia mamlaka za ufuatiliaji kama vile taasisi kuu za ukaguzi au kuanzia chini kwenda juu, kupitia wanaume na wanawake wanaotumia au kupokea huduma, wakitoa malalamiko yao kwa pamoja.

Usimamizi unaonekana kuwa na ufanisi zaidi endapo ufuatiliaji kutoka juu kwenda chini na ule wa kutoka chini-kwenda juu unapoungana kwa pamoja. Usimamizi unawawezesha wabunge, vyama vya siasa, wakaguzi wa serikali, taasisi kuu za ukaguzi, na viongozi wa umma na watoa huduma wa serikali na wa sekta binafsi kutathmini tena huduma, kubainisha kero mpya, kuchagua sera za baadaye na kuboresha utekelezaji wake.Kinadharia, utekelezaji lazima ufuatiliwe kwa karibu ili kupata mrejesho juu ya maendeleo, matatizo, na ufanisi wa utendaji kazi. Vyombo vya udhibiti vya serikali, kama vile idara ya serikali ya ukaguzi wa shule za msingi na sekondari, zinaweza kufanya kazi nzuri ya kufuatilia uzingatiaji wa viwango, kanuni na sera ilimradi ziwe na nafasi na uwezo wa kufanya kazi hizoMfano halisi wa Usimamizi Usafi wa mazingira nchini Ghana ni mfano mzuri wa namna ambavyo usimamizi unaweza kubainisha matatizo ya utoaj huduma katika uhalisia.

Utafiti unaonesha masuala yaliyolengwa kufanyiwa mageuzi na usimamizi wa jamii kuboresha vyoo vya umma: wanasiasa wa maeneo hayo walitumia mikataba ya kusimamia vyoo kama takrima kwa washirika wao. Hali hii ya vyoo vya umma kugeuzwa kuwa mradi wa kujiingizia kipato kwa wanasiasa, pamoja na kukosekana kwa nidhamu ya urasimu kulisababisha kukosekana kwa huduma ya vyoo safi na salama, licha ya kuwepo mipango na sera za serikali. Aidha, ufuatiliaji haukuwezekana kwa sababu Idara ya Usimamizi wa Taka pamoja na mabwana afya hawakuweza kuwawajibisha wasimamizi wa vyoo vya umma. Wanasiasa wa maeneo husika walilindwa sana na mfumo uliokuwepo (Ayee na Crook 2003).

1.4. Kanuni za Uwajibikaji wa Kidemokrasia ni Zipi?

Uwajibikaji wa kidemokrasia umejikita kwenye kanuni tatu ambazo zinawawezesha wananchi na wawakilishi wao—wadai haki— kuwawajibisha maafisa wa umma na sekta binafsi wenye wajibu wa kutoa huduma, ambao kwa maneno mengine, wanaitwa ‘wawajibikaji’.

Kanuni hizo tatu ni uwajibikaji, usikivu, na utekelezaji. Kanuni hizo zitawasaidia wathamini kubainisha mazingira yaliyopo au kama yanaweza kuboresha zaidi mahusiano ya kiuwajibikaji. Kama ilivyoelezwa, wathamini ni lazima wathibitishe kama kanuni zinafuatwa katika mwingiliano halisi wa kikazi kati ya wawajibikaji na wadai haki. Uwajibikaji unapima kiwango ambacho serikali inatekeleza majukumu yake katika kuelezea na kuhalalisha maamuzi yake kwa umma. Ufanisi mkubwa wa uwajibikaji unaanishwa kwa namna ambavyo wadai haki wanaelezea mahitaji yao, lakini pia unahusiana na nafasi, uwezo na utayari wa maafisa kuwajibika kwa matendo yao. Kwa mfano, sheria za uchaguzi (kanuni za uchaguzi au za wilaya) au sheria za mashirika za kuajiri, kusimamia na kuwafukuza kazi watumishi wa umma ambao ni wa kuchaguliwa na wasio wa kuchaguliwa, kila mmoja anapaswa kuwajibika. Usikivu unahusiana na ama maafisa wa serikali wanapanga muda wa kukusanya maoni ya wananchi au wawakilishi wao kabla sera au sheria haijapitishwa rasmi, ili maudhui ya maamuzi hayo yatokane na maoni yao na matakwa ya wananchi au kanuni za haki za binadamu (International IDEA 2008: 24). Kwa kiasi kikubwa, motisha ya kisiasa kwa serikali kuwa sikivu kwa wananchi inategemea na mfumo wa vyama, sheria za uchaguzi, pamoja na taratibu nyingine za kitaasisi.

Motisha pia inaweza kuathiriwa na upatikanaji wa nyenzo za kiteknolojia, rasilimali watu au fedha. Usikivu pia unaweza kujionesha kupitia mwingiliano usio rasmi baina ya wawajibikaji na wadai haki, kama vile tafiti za kitaifa za maoni, mikutano ya siri,
kampeni za utetezi au maandamano. Katika mahusiano halisi ya uwajibikaji wa kidemokrasia, wawajibikaji:

• wanawajibika, wanafafanua na kuelezea uhalali wa utendaji wao;
• ni wasikivu, wanaingiza maoni na mapendekezo ya wananchi kuhusu sera katika maamuzi yao; na
• wanawajibishwa kwa namna inayotekelezeka.

Utekelezaji ni kuhusiana na matokeo rasmi au yasiyo rasmi ambayo wawajibikaji wanaweza kukumbana nayo na kulazimika kuwajibika kutokana na matendo yao. Uwezekano wa kutoa adhabu na tuzo unachangia kuboresha uwajibikaji. Adhabu au tuzo hizo zinaweza kuwa zimeainishwa kisheria au zikakubalika isivyo rasmi kutumika kutokana na mazoea. Baadhi ya wadai haki wanaweza kuwa na mamlaka ya kutekeleza adhabu au tuzo hizo, kama ilivyo, taasisi kuu za ukaguzi wa hesabu ambazo zina mamlaka ya kisheria na kiutawala katika kutoa hukumu, kamati za bunge zina mamlaka ya kuagiza kufanya mabadiliko katika sera, au mahakama yenye mamlaka ya kubatilisha mchakato wa uchaguzi uliotawaliwa na ulaghai na udanganyifu.

Wadai haki wasio na mamlaka rasmi ya kutekeleza hukumu (kama vile makundi ya wananchi, kamati za bunge zisizo na mamlaka ya kuhoji zaidi, au ofisi ya malalamiko katika baadhi ya nchi) wanapaswa kushirikiana na taasisi zilizopewa mamlaka kushinikiza utekelezaji. Uwezo wa kifedha na uhuru wa kisiasa wa taasisi hizo vinaathiri uwezekano wa kutekeleza jukumu hili.Mfano mzuri wa mahusiano ya uwajibikaji wa kidemokrasia, wadai haki:

• wanapata taarifa kuhusu utendaji wa wawajibikaji;
• wanawahoji wawajibikaji;
• wana nafasi ya kutoa mawazo kuhusu sera; na
• wanatoa adhabu au tuzo kwa wawajibikaji kutokana na utendaji wao.

Ushiriki na uwazi unaweza kuchangia kufanikisha kanuni hizi tatu za demokrasia. Ushiriki unahusu haki ya wananchi kushirikiana, kukusanyika, kutoa maoni na kuwa na sauti katika mchakato wa sera. Uwazi ni upatikanaji wa taarifa sahihi, zilizo wazi, na zinazopatikana kwa urahisi kuhusu utendaji, mpango, usimamizi na ahadi kati ya serikali na wananchi au kati ya wakala mmoja wa serikali na mwingine.

Unapotathmini kanuni hizi na jinsi zinavyohusiana na taratibu za uwajibikaji, ni lazima kuchunguza iwapo misingi hii inatumika kwa usawa, au makundi fulani katika jamii yanatengwa au kubaguliwa. Pia, motisha ya kisiasa kwa wanasiasa na kushindwa kwa mifumo
ya siasa kuwakilisha wananchi ni mambo muhimu ya kuzingatia. Kwa mfano, je wanawake wana uwezo na nafasi sawa kama wanaume
katika kupata majibu kutoka kwa wawajibikaji? Je, viongozi wa serikali ni wasikivu kwa wananchi masikini kama ilivyo kwa matajiri? Kupunguza utoro wa walimu katika shule za msingi nchini Ghana ‘Katika nchi ambayo inatumia asimia 80 ya bajeti yake ya elimu kuwalipa walimu mishahara, utoro wa waalimu unaweza kusababisha matumizi mabaya ya pesa za umma katika elimu.

Japo ilikuwa inajulikana wazi kabisa kuwa waalimu muda mwingi wamekuwa hawaingii darasani nchini Ghana, Kituo cha Maendeleo ya Kidemokrasia nchini Ghana (CDD-Ghana) kiliamua kupima kiwango cha utoro katika shule za msingi na kuangalia kwa karibu zaidi mienendo, sababu na ufumbuzi wa tatizo hili sugu’. ‘Mwanzoni mwa mwaka 2008 timu ya watafiti kutoka CDD￾Ghana, ilianza kutembelea mara kwa mara shule 30 za msingi ili kuchunguza matukio ya utoro wa walimu katika shule hizo.

Katika ziara yao ya kwanza kwa kila shule walikusanya taarifa za kiidadi na zile za ubora kuhusu walimu na shule, pia kuhusu umbali kutoka ilipo shule na vituo vya afya au benki. Kisha walifanya ziara nyingine zisizopungua mbili […] ili kuhakiki uwepo wa walimu kwa kutumia orodha waliyopewa na uongozi wa elimu wa wilaya husika. Mwishoni, timu ya CDD-Ghana waliendesha majadiliano katika vikundi vya mjadala […] jumuiya za wazazi na walimu pamoja na kamati za uongozi wa shule ili kuthibitisha […] sababu za utoro, na iwapo ufuatiliaji ulifanyika au adhabu zilitolewa’.

‘[...] CDD-Ghana iligundua kuwa asilimia 47 ya walimu walikuwa watoro angalau katika moja ya ziara, na wastani wa kiwango cha utoro kwa walimu 192 waliochukuliwa kama sampuli walikuwa ni asilimia 27. [...] Ingawa sababu za utoro zilizotolewa mara nyingi zilikuwa ni ugonjwa na kuhitaji kufanyiwa uchunguzi wa afya, sababu nyingine iliyotolewa mara nyingi ilikuwa ni “Kuhudhuria vipindi vya mafunzo yanayotolewa mbali na shule yao” [siku ya Ijumaa]. [...] Programu za mafunzo ya elimu masafa, zinazoendeshwa na vyuo vikuu nchini kote, zilikuwa zinafanyika mwishoni mwa wiki kuanzia siku ya Ijumaa baada ya kumalizika vipindi katika shule za msingi na sekondari.

Hata hivyo, ili kuhudhuria programu hizo iliwalazimu walimu walioteuliwa waliopo mbali na chuo kikuu husika kuacha vipindi vyao shuleni ili wawahi vipindi vyao vya mafunzo ya elimu masafa’. CDD-Ghana ilitoa taarifa za utafiti huu kwa waandishi wa habari na kupokelewa kwa shauku. Makala kuhusu matokeo ya utafiti yalichapishwa katika magazeti sita. CDD-Ghana ikapendekeza kwa maafisa wa serikali, akiwemo mkurugenzi wa elimu ya msingi katika kituo cha huduma ya elimu nchini Ghana (GES), kwamba ratiba ya mafunzo ya elimu masafa kwa walimu irekebishwe ili isiingiliane tena na muda wao kufundisha vipindi katika shule za msingi.

Pendekezo hili liliishawishi GES kurekebisha programu ya mafunzo kwa waalimu. CDD-Ghana ilielezea tatizo kwa namna ambayo ilisababisha wawajibikaji kutilia maanani mawazo ya umma, na wakati uo huo CDD-Ghana ilipendekeza ufumbuzi ambao ulikuwa unatekelezeka kwa urahisi.
 
Back
Top Bottom