SoC02 Uwajibikaji

SoC02 Uwajibikaji

Stories of Change - 2022 Competition

Omari Frank

Member
Joined
Jul 22, 2022
Posts
14
Reaction score
5
Mada kuu: UWAJIBIKAJI

Uwajibikaji ni hali ya kutimiza majukumu bila shuruti. Uwajibikaji unahusisha kufanya kazi kwa bidii, kujitoa katika shughuli za kijamii, kutunza familia na kulitumikia Taifa kwa nidhamu kubwa na uzalendo.

Kwa mataifa yaliyoendelea kama vile CHINA, JAPAN, MAREKANI n.k uwajibikaji umekua silaha yao kubwa inayochagiza maendeleo ya kiuchumi katika mataifa yao.

Kwa upande wa nchini kwetu Tanzania uwajibikaji upo lakini bado kuna changamoto kadhaa katika baadhi ya maeneo nchini ambapo tumekua tukishuhudia kesi nyingi za utekelezaji wa familia, Wizi, Uhuni, Ulevi uliopitiliza na mengineyo ambayo yote haya yanatokana na watu kutowajibika ipasavyo.

Wengine wanaadiriki kukwepa kulipa kodi na kuchangia kurudisha nyuma uchumi katika ngazi ya kitaifa.

NINI KIFANYIKE?
  1. Elimu
Wananchi wawe wanapewa elimu mara kwa mara juu ya suala la uwajibikaji katika nyanja mbalimbali za kimaisha na umuhimu wa kufanya hivyo. Hii itasaidia kupunguza kesi na matukio ya hovyo pia kuliweka Taifa katika dira kubwa ya maendeleo.
  1. Sheria kali
Ni lazima sheria kali ziwekwe na zifuatwe. Watu ambao hawatakua tayari kuwajibika basi ni lazima wakutane na mkono wa sheria ili wajifunze na hii haina lengo la kuwaumiza bali ni kwa maslahi mapana ya Taifa letu la Tanzania.
  1. Wazazi na walezi wakishirikiana na walimu wawafundishe watoto uwajibikaji tangu wakiwa wadogo, kuwajengea uzalendo na mapenzi na nchi yao, kuwajengea nidhamu na ukakamavu.
Hivyo basi, Uwajibikaji kwa ujumla wake ni nyenzo muhimu sana katika maendeleo ya watu mahali popote pale duniani. Nitoe wito kwa jamii mbalimbali nchini kuhakikisha zinajijengea misingi ya uwajibikaji kwa maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.
 
Upvote 0
Ivi unahisi ni elimu gani inapasa itolewe kwa wananchi waelewe kwa hizi tozo ndombadala wa kuleta maendeleo katika hili taifa?
 
Kaka mchakato wowote wa maendeleo una maumivu ndani yake, inawezekana kabisa ongezeko la tozo na kupanda kwa gharama za maisha ni chumvi kwenye vidonda vya watanzania walio wengi lakini ikiwa kama tozo hizo zinatumika kuboresha elimu, Afya, Miundo mbinu, Umeme, Maji, Kulipa madeni ya Taifa n.k basi sioni kama kuna ubaya.

Nadhani ni muhimu kuongeza jitihada kwenye kazi na sio kuishia kulalamika tu wakati zinapotangazwa huduma za bure huwa tunashangilia bila kujali serikali inatoa wapi hizo pesa.

Mimi naamini hakuna serikali duniani inayopenda kuona wananchi wake wanaumia, wawekezaji wanakimbia n.k

Hivyo basi, ni suala la muda tu. Tuwajibike tu kaka, things will be just fine.
 
Amna nakataa kijana mwenzangu kama wwe mpambanaji but unaamini katika katika tozo kama chanzo cha kupata mapato apo nikukosa maarifa nakukusa haki yako ya msingi ya Freedom of expression na huwezi hukanitia moyo kuwa mambo yatakuja kuwa sawa wengi wape mimi apa nadaiwa millions 100+ katika deni la taifa je utalipa kwa kutegemea tozo think twice
 
Back
Top Bottom