SoC03 Uwajibikaji

SoC03 Uwajibikaji

Stories of Change - 2023 Competition

0036 savage

Senior Member
Joined
Apr 30, 2019
Posts
189
Reaction score
238
Katika nchi yetu ya tanzania kumekuwa na ukosefu wa uwajibikaji kwenye nyanja nyingi sana kuanzia jinsi ya kupata ajira mpaka kazi inavyofanyika,kwa mfano mtu anaaniriwa kwa kufanyiwa usahili na anaonekana kufanya vizuri huko kwenye usahil ila akishafika eneo la kazi anaanza kufundishwa kazi na vibarua ambao walishindwa kufaulu usahil huo hichi kitu kinaumiza sana na kukatisha tamaa.

Kingine walioko makazini wengi wao awana uwezo wa kufanya kazi yani mtu kaajiriwa kwaajil ya kazi fulan kwa mfano dereva,lakin ajui kuendesha gari vizur au hata gari lenyewe aendeshi anakaa tu ofisini au wakati mwingine hata ofisini afiki kabisa kwa kipind anachojipangia yeye mwenyewe na aulizwi na mtu yoyote,ikitokea kazi imeharibika wanaanza kukingiana vifua na ili kumtetea huyo anaehujumu uchumi.

Kinginge kuna utofauti mkubwa katika mishaara ya serkali kwa mfano mtu mwenye bachela ya uhasibu anaefanya kazi bandarini(TPA)anakuwa na mshaara mkubwa kuliko alieko manisipaa hili linafanya watu kutokujituma kabisa inakuwaje mtu mwenye ngazi ya cheti anaefanya kazi bandarini amzidi mshaara mwalimu mwenye bachela hii mishaara inawezekanaje ikawa hivi hili linakatisha tamaa sana na ukiuliza unajibiwa hoooo mara huku wanafanya uzalishaji mkubwa mshaara wa serikali upangwe kutokana na elimu sio uzalishaji hilo alipo sawa hata kidogo kuna watu kama madaktari na walimu awazalishi pesa nyingi ila wana umuhimu mkubwa sana inakuaje walipwe kidogo kisa awazalishi je wote tusisome twende veta ili tuwe wazalishaji tulipwe zaid???mbona thaman ya elimu aina maana nchi hii hili serikali ailioni aion kuna aja ya mshaara kufanana kote bila kujali ni wapi bora tu no serikalini basi mshaara upangwe kutokana na elimu sio uzalishaji.

Na kuna hili jambo la kuingia ofisi fulani unakuta kilamtu hapo ni kabila fulani yani wote ni kabila moja hili nalo linakatisha sana tamaa hata kama watu awawekani ila linafikirisha sana kwa wewe ambae kilasiku unaomba kazi alafu unakosa.

Nashauri serikali iweke mifumo itakayomfanya mtumishi awajibike vile inavyopaswa mfano kamera ambazo zitarekodi kilakitu kinachoendelea maeneo ya kazi,itumie alama za vidole kama maudhurio ya wafanya kazi kazini na malipo yao yaingizwe kutokana na maudhurio,kuwe na ukaguzi wa mara kwa mara ili kujiridhisha na utendaji wa watumishi iliowaajili.

Asante nawasilisha.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom