SoC03 Uwajibikaji

SoC03 Uwajibikaji

Stories of Change - 2023 Competition

Ladymae

New Member
Joined
May 28, 2023
Posts
2
Reaction score
1
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa JamiiForums kwa kuandaa na kutoa nafasi hii ya kipekee kwa wananchi. Huu ni mtazamo wa mfano mzuri katika uhuru wa vyombo vya habari kwa jamii.

Napenda nitoe maoni yangu kuhusu uwajibikaji.

Nitaanza kwa kufafanua maana ya neno uwajibikaji. Neno uwajibikaji lina maana mbili:

"Uwajibikaji ni kuchukua hatua ya dharura baada ya matokeo yoyote yenye utata au yanayohitaji utatuzi wa haraka katika utekelezaji wa majukumu yanoyomkabili mhusuka. Hatua hii inaweza ikawa hata kuondoka katika nafasi ambayo mhusika alikua anaitumikia katika jamii, taasisi au hata ngazi ya familia."

"Uwajibikaji ni utekelezaji wa majukumu ambayo umekabidhiwa na mwajiri au majuku binafsi katika ngazi ya familia."

Aina ya kwanza ya uwajibikaji niliyoifafanua hapo juu imekua tatizo kubwa kwa maana kwamba wengi hawakubali kuwajibika kwa kuachia nafasi ambazo walikua wamekabidhiwa mara tu baada ya kushindwa kuleta ufanisi kwa hiari yao. Watendaji wengi wamekua wagumu kuachia nafasi zao kutokana na kwamba waliopo juu yao wamekua wagumu pia kufanya hivyo.

Hili limesababisha mlolongo wa viongozi na watendaji wabovu kuanzia ngazi ya juu ya utekelezaji mpaka ngazi ya chini kabisa. MAONI yangu kwa watanzania wenzangu ni kwamba, tuwe watu ambao tunakubali makosa, tuwajibike kwa makosa hayo na tubadilike ili kuleta utendaji wenye tija katika Taifa letu.

Hii itaepusha madhara zaidi katika maeneo yetu husika na jamii yote kwa ujumla. Utajeshimika pia kwa kuithamini nchi yako na kutoa nafasi kwa watendaji wengine kutekeleza majukumu hayo. Ni funzo pia kwa wengine ambao watashuhudia hilo, taongeza uchapa kazi, uadilifu na umoja katika utekelezaji wa majukumu.

Katika aina ya pili ya uwajibikaji, ni vyema kuzingatia muda wa kazi. Masaa ambayo mtu anatakiwa awepo kazini na atelekeleze majukumu yake, ni muhimu kuutumia vizuri ipasavyo na kuepuka utoro kazini, uzembe, uvivu na kutokujali na kuzingatia kazi ambazo umekabidhiwa. Wizi wa muda wa kazi ni tatizo katika ofisi za umma na baadhi ya ofisi za taasisi na mashirika ya binafsi.

Si vyema kufanya kazi za ziada za kujiongezea kipato kwa kutumia muda wa mwajiri. Ni vyema kua na utaratibu katika mambo mengine ya ziada mbali na yale ambayo mtu amekabidhiwa kutekeleza. Ni vyema kujifunza namna ya kujisimamia na kujitawala.

Vinginevyo wasimamizi nawashauri katika idara zote wanatakiwa kua makini kwa kuwatambua wafanyakazi wote na kuzielewa tabia zao ili kuweza kuwasimamia vizuri. Maeneo mengine hasa taasisi binafsi, wameweka vifaa vya utambuzi wa alama za vidole. Hii inawasaidia watendaji kutambulika pale wanapoingia na kutoka katika eneo la kazi.

Hivyo basi, ili uwajibikaji uweze kutekelezeka, ni lazima kua na NIDHAMU na BIDII katika kazi, katika kila sekta ya utendaji hapa nchini. Sekta hizo ni kilimo, ufugaji, biashara na utumishi katika ofisi za serikali na sekta binafsi. Mtumishi mwenye nidhamu atakua muadilifu na atafanya bidii katika utendaji wake.

Nia na lengo la uaminifu na uadilifu kwa mtumishi linachochewa na matokeo ya kodi yake anayolipa kutumika vizuri kwa kumletea maendeleo na huduma muhimu za kijamii kama huduma za afya na huduma za elimu.

Haya ni maeneo muhimu ambapo kila mwananchi anategemea kuyaona yakiwa katika viwango vizuri ili aweze kupata huduma hizo yeye pamoja na familia yake.

Afya ikiwa na matatizo ni lazima uzalishaji utapungua kwa kiwango kikubwa. Elimu nayo isipokidhi mahitaji, malengo hayatafikiwa.

Elimu hii si ya darasani tu, ni pamoja na elimu ya ukulima na ufugaji bora ambayo watendaji wake ni kama hawapo maana hata huku kijijini tulipo hatuwaoni msimu wa mvua wakielimisha watu namna ya kupata mazao mengi na bora. Wafugaji wengi wanafuga tu kwa uzoefu wa ufugaji wa zamani wenye matokeo madogo.

Vile vile Elimu ya vyuo vikuu bado bado ni tatizo maana si kila mwenye sifa anapata mkopo wa kumuwezesha kusoma.

Matatizo haya yote yanatokana na kutowajibika katika kusimamia pato la Taifa. Wote sisi ni mashahidi wa kusikia ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali kila mwaka imejaa ubadhirifu, matumizi mabaya ya fedha za umma na hakuna uwajibikaji. Maoni yangu ni kwamba, wahusika hao wawe mfano bora wa uwajibikaji na kuondoka katika nafsi zao.

Itambulike kwamba, mwananchi anayelipa kodi anategemea kuona maendeleo yakimfikia kwa ukaribu, apate bidhaa za msingi kwa bei nzuri za kawaida ambazo atazimudi na ugumu wa maisha upungue. Hii ingeongeza chachu ya ukusanyaji kodi kwa hiari na kuongeza pato la Taifa.

Kama vile ambavyo serikali ndio msimamizi wa sheria na miongozo ya utendaji na ukusanyaji wa kodi na vyanzo vingine vya mapato nchini, ni jukumu lake kuhakikisha kwamba kile kinachopatikana kinatumika vizuri bila ubadhirifu kwa faida ya wananchi wote.

Hii itaongeza ufanisi, nidhamu, uadilifu, bidii na kuleta umoja wa kitaifa.

Hivyo basi, tunataka kusikia taarifa nzuri kutoka kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali. Nina uhakika hakuna atakayekata tamaa ya kulipa kodi, kuiba mali ya umma au binafsi. Matukio kama hayo yataisha na UWAJIBIKAJI utashamiri katika kila sekta, maendeleo yatachanua na amani yetu itazidi kuimarika kwa kiwango kikubwa

Nimalizie kwa kutoa maoni ya ushauri kwa wananchi wenzangu kwamba, tufanye kazi halali ili tuepuke matatizo. Kuvunja sheria kunapoteza muda wa uzalishaji, muda mwingi utautumia kutatua matatizo yasiyokua na msingi na ambayo ungeweza kuyaepuka.

Ladymae.
 
Upvote 2
Sheria kichwa kianzie maneno manne wewe kenge umeandika neno moja

Usituchoshe
 
Back
Top Bottom