Uwanja mkubwa wa mpira Chato wa nini?

Uwanja mkubwa wa mpira Chato wa nini?

kwa uwanja hautasaidia wananchi? uwanja sio tu kucheza, kuna wengine watakua na mashelf ya biashara kwenye huo huo uwanja: we unadhan uwanja unagusa tu wachezaji? usafiri pia, nini cha kudebate apa wakati vitu vinaonekana, we unataka uchumi wote uishie dar? kwamba chato sio watanzania ama
Uchangiaji wa uwanja nitofauti na hosptl ama shule,inamaana hamtaki hata shule zijengwe huko wasukuma waelimike?
Kweli hii ni itaendelea kuwa mtoto kuwaza kwanini baba yangu asingekua Mo Dewji na mzazi kuwaza kwanini mwanangu asingekua Samatha
 
Uchangiaji wa uwanja nitofauti na hosptl ama shule,inamaana hamtaki hata shule zijengwe huko wasukuma waelimike?
Kweli hii ni itaendelea kuwa mtoto kuwaza kwanini baba yangu asingekua Mo Dewji na mzazi kuwaza kwanini mwanangu asingekua Samatha

uwanja hakuna chato, hospital zimejaaa mbna: hujawahi fika chato nn
 
Economically kujenga kiwanja ni kusaidia chato kusogea: wale watu wa chato watapata pa kuuza endapo mechi zitakua zinachezeka apo: Tanzania Sio Dar tu, Raisi angekua ana mawazo kama yako ndo yale ya kenya nairobi uchumi mkubwa wakati turkana watu mil 1 wamekufa kwa njaa: Tunashukuru raisi hana akili kama yako
Wesijui ndio umeandika nini Sasa hapo uwanja mkubwa ndio unaleta chakula ajenge soko kubwa
 
Mkuu, sisi hatushindani na Rwanda wala inchi yoyote.
Kama chato ipo ndani ya eneo ya United Republic of Tz kwani kuna tatizo gani mkuu??

Mbona SGR inajengwa From Dar to morogoro watu wa mtwara na Tanga hawajalalamika??

Binafsi sioni tatizo, maana kiwanja cha chato sio ndio kitakuwa cha mwisho kujèngwa... Mwanźa, Arusha, Mbeya, Kigoma vitajengwa tu mkuu, tujipe muda boss
Mkuu kuna watu humu wanamatope kichwani.
 
Mkuu, sisi hatushindani na Rwanda wala inchi yoyote.
Kama chato ipo ndani ya eneo ya United Republic of Tz kwani kuna tatizo gani mkuu??

Mbona SGR inajengwa From Dar to morogoro watu wa mtwara na Tanga hawajalalamika??

Binafsi sioni tatizo, maana kiwanja cha chato sio ndio kitakuwa cha mwisho kujèngwa... Mwanźa, Arusha, Mbeya, Kigoma vitajengwa tu mkuu, tujipe muda boss

Kweli ccm apologetics wote akili hawana. Yaani neno capacity kwako halina maana kabisa!
 
Tunataka Rais wetu awe anacheza mpira kama Pierre Nkurunzinza.
Halafu Chato ni lazima kupewe kipaumbele kuliko sehemu nyingine yoyote, Chato ni ardhi takatifu
Chattle ni taifa teule, Chattle ni nchi ya ahadi
By 2025 Chattle itakuwa jiji la kwanza ikifuatiwa na Dodoma
 
Huo mfano ndugu yangu haufanani kamwe na Chato, kwa taarifa yako mji mdogo wa chato upo kwa miaka mingi ikiwa ni pamoja ginnery ya kuchambua pamba ilijengwa hapo miaka mingi iliyopita na umeme ulikuwepo. Aidha, chato iko kwenye mwambao wa ziwa na ni bandari ndogo na kwa sasa mji huu ni makao makuu ya wilaya, hivyo usitegemee chato eti kuja kuwa magofu kama unavyodai wakati Raisi akiondoka madarakani. Chato pia iko kwenye barabara kuu ya kwenda Bukoba hadi nchi jirani. Kwa hiyo chato itabaki mji forever hadi mwisho wa dahari.
Katika mji wa Gbadolite alikotoka, Rais Mobutu Sese Seko alijenga kasri kubwa la kifahari na uwanja wa ndege ambao ndege za kusafirisha bidhaa za anasa kama vile mvinyo ghali kutoka Ulaya zilitua na kupaa.

Njia ya kutumiwa na ndege kupaa na kutua katika uwanja huo ilikuwa kubwa kiasi cha kuweza kutumiwa na ndege kubwa ya wakati huo Concorde - ambayo aliikodi mara kwa mara.

Lakini alipotimuliwa madarakani mwaka 1997, kila kitu kilisimama. Sasa ni mahame.
 
Mkuu, sisi hatushindani na Rwanda wala inchi yoyote.
Kama chato ipo ndani ya eneo ya United Republic of Tz kwani kuna tatizo gani mkuu??

Mbona SGR inajengwa From Dar to morogoro watu wa mtwara na Tanga hawajalalamika??

Binafsi sioni tatizo, maana kiwanja cha chato sio ndio kitakuwa cha mwisho kujèngwa... Mwanźa, Arusha, Mbeya, Kigoma vitajengwa tu mkuu, tujipe muda boss
Kuna watanzania wanapenda kuishi na maumivu ya moyo pasipo sababu, huyu mleta mada ni mmojawao.
 
Kamgomoli,

Uwanja wa Mpira haujengwi kwa Kigezo cha eneo husika kuwa mbali au kwamba halina Watu wengi au halina Michezo.

Ujenzi wa Uwanja unaweza ukawa ndiyo chachu kubwa ya muamko wa Kimichezo katika eneo husika lakini pia Ujenzi wa huo huo Uwanja unaweza pia kuwa ni Chanzo cha Mapato kwa Halmashauri na Serikali husika ya Mkoa.

Kama haitoshi Uwanja huo huo mkubwa wa hapo unaweza kuwa ni Chanzo cha Kiuchumi hasa kwa Wakazi kwani wanaweza wakawa wanauza bidhaa zao pale Michuano ikiwa inachezwa hapo.

Baada ya Ujenzi wa Uwanja huo wenye Mamlaka nao wanaweza wakawa wanautumia kwa Kuukodisha kwa Timu Kubwa Kubwa nchini au hata wakawa Wanaandaa Mashindano ambayo yatazikutanisha hizi Klabu Kubwa hivyo Mapato Kuongezeka lakini hata na Hamasa ya Kimpira na Kimichezo eneo husika nayo ikaongezeka.

Na Viwanja havijengwi kwa matumizi tu ya sasa basi Viwanja vinajengwa hata kwa matumizi ya baadae na kwa Vizazi vijavyo.

Na Kinachofanya Uwanja Kujaa siyo Watu (Wakazi) husika wa hapo bali ni ' Hamasa ' na ' Mwamko ' unaojengwa na Wahusika wa Kimichezo kutokana na Mipango yao waliyonayo katika Kuendeleza Mchezo wa Mpira wa Miguu hapo.

Na hakuna mahala popote pale nchini Tanzania pameandikwa kwamba ndiyo pawe na Uwanja wa Mpira na pengine pasiwepo.

Umeleta Mada hii Kiuanaharakati / Kisiasa zaidi kwakuwa tu una Chuki zako na Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kuwa nae anatokea hilo eneo la Chato na huenda pia na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Na hii Serikali nina uhakika Uwanja huu huu ungesikia Unajengwa eneo jingine wala usingekuja na haya ' Majungu ' yako. Kwani sehemu atokayo Rais ikiwa na Maendeleo ni Kosa au Dhambi?
Watanzania na malalamiko baba mmoja mama mmoja.
 
Hesabu za wanasiasa huwa ni za kujua wao wenyewe tu. Hivi kweli Chato kunahitajika uwanja mkubwa wa mpira wa miguu kama wa Taifa (kwa Mkapa) wa kazi gani?

Kama huu mmoja Dar na uwingi wote wa watu tunashindwa kuujaza je Chato? Huu utakuwa ni upotevu mwingine wa fedha kama za ESCROW.

Sifa zikizidi haya ndo madhara yake. Nilitegemea uwanja kama huu ujengwe kwenye Majiji makubwa kama Mwanza, Mbeya, Arusha au Morogoro. Kiukweli kwa hili hata kama ndio charity begins at home, this is too much.

Mimi niko pamoja na mzee Meko na nakubali mambo mengi anayoyafanya ila kwa hili HAPANA. Hapa ndipo Kagame anapotupiga bao. Hesabu zake ni very strategic. Hakurupukagi. Mwezi uliopita tumeona Rwanda wakiufungua uwanja bora na wa kisasa kabisa maarufu kama Kigali Arena.

Sisi bado maamuzi yetu ni ya sifa sifa na mihemko. Kagame anaijenga Kigali inaonekana. Sisi hatueleweke mara, tujenge Arusha tunaacha tunahamia kuijenga Dodoma. Wakati huo huo Dar nayo inatakiwa ijengwe sasa tunahamia Chato.

Sisemi mikoa mingine isijengwe lakini kuna miradi ya kimkakati ambayo inahitaji kufikiri na kutafakari kwa kina. Yawezekana kwa sasa kipaumbele cha watu wa Chato ni hospitali ya kisasa au vyuo vya ufundi na si uwanja mkubwa kiasi hicho. Hakunaga mipango ya namna hiyo!

Nadhani Chato wanahitaji uwanja mdogo tu kama wa Azam Complex unawatosha.

Wahusika tafakarini. Kwa mipango yetu mibovu ndio maana hadi leo hii hatuna ukumbi wowote wa maana kwa ajili ya kuhost mikutano mikubwa, hatuna kumbi kubwa za kisasa za burudani. Na hakuna anayeona hilo.

Cheap political popularity inatugharimu sana tena sana.

View attachment 1244923
6 years later, unaonekana ulikuwa na point.
 
Kila jiji na kila mkoa tunahitaji viwanja vya maana, utajiri tunao na uwezo wa kujenga tunao, why not?
 
Back
Top Bottom