Hongera kwa andiko zuri Sana....!!!!
Bahati mbaya au nzuri hauja eleza kuhusu muundo wa klabu ya Simba na namna ambavyo watapata hasara kupitia Mo kutoa Bilioni 2.
Simba sio Mali ya Wana Chama peke yao, bali ni kampuni.
Ili kujadili kuhusu klabu ya Simba ni lazima kufahamu mambo yafuatayo.
1.Simba Sport Club
2.Simba Holding company Limited
3.Mo Simba Company Limited
4.Simba Sports Club Company Limited
Ukifatilia Kuna Simba nne ambazo zipo kwenye miundo Tofauti Tofauti.
Simba ya kwanza...SIMBA SPORTS CLUB mwenyekiti ni Mangungu....!!
Hii ni club ya Simba ambayo ndio imeunda kampuni yao brella ambayo inaitwa SIMBA HOLDING COMPANY yenye hisa asilimia 51.
Simba nyingine ni MO SIMBA COMPANY LIMITED hii ni kampuni ya Mo ambayo imesajiliwa Brella ina asilimia 49.
Kampuni za SIMBA HOLDING COMPANY na MO SIMBA COMPANY LIMITED zimeungana na kutengeneza kampuni Moja ambayo inaitwa SIMBA SPORTS CLUB COMPANY LIMITED.
Kampuni hii ndio Ina endesha klabu ya Simba Kwa kupitia Bodi ya wakurugenzi ambayo imeajili C.E.O ambae ana endesha klabu katika shughuli za Kila siku kwa niaba yao.
Kimsingi Mali za Simba na Madeni ya Simba ni ya Mo Dewji pamoja na Wana Chama wa Simba, maana na yeye ni sehemu ya umiliki kupitia kampuni yake ya Mo Simba Company Limited.
Kwaiyo basi maendeleo,Mafanikio au hasara zina mgusa Mo Moja kwa Moja kwa maana ni muwekezaji ndnai ya Simba.
Ni rudi kwenye hoja yako ya Mo kutoa Bilioni 2 kwneye ujenzi kati ya kiasi Cha Bilioni 30 zinazo hitajika.
Jambo Moja la msingi kutambua ni kwamba hivi ndani ya klabu ya Simba Kuna mwana Chama ambae ameweza kuchangia kiasi Cha kuanzia Bilioni 1 na kupanda juu...?
Wewe imechukua jumla ya michango inayo hitajika nakuona Mo katoa pesa kidogo kuliko Wana Chama.
Bila kujua kumbe Wana Chama Hawa Wana changia kuanzia buku au elfu tano,elfu hamsini, laki, milioni na kuendelea.
Lakini Mo yeye mtu mmoja katoa Bilioni 2 lakini Wana Chama wao kwa umoja wao wana toa bilioni 28.
Hapa kimantiki Mo katoa nyingi kama mtu mmoja kulinganisha na mtu mmoja mmoja kwenye mchango wake.
Kwaiyo kama tugesema tutafute msimamizi wa mradi kwa kuangalia mchango wake yeye ndio ana stahili kuwa mwenyekiti wa mradi kwa pesa yake kuwa nyingi kuliko mwana Chama yoyote.