Uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa, Yanga na Simba kutafuta viwanja vingine kwa mechi za Ligi na CAF

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen ni kuwa Simba na Yanga watalazimika kutafuta viwanja vingine kwasababu dimba la Benjamin Mkapa litaendelea na matengenezo makubwa mwezi huu hivyo kupisha mchakato huo matumizi ya uwanja huo yatafungwa kwa muda.

1759566864084.png
Uwanja wa Mkapa umefungwa kwa kipindi cha miezi sita (6) kupisha ukarabati mwingine mkubwa kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali aliyenukuliwa na gazeti la The Citizen.

Msemaji Mkuu amesema mchezo wa Simba dhidi ya Namungo ndio ulikuwa mchezo wa mwisho kwa Mkapa ambapo Klabu hizo mbili Simba na Yanga zinapaswa kuchagua Chamazi (Mbagala) na Amaan (Zanzibar) kwa ajili ya mechi zao.

Soma: Serikali yakamilisha ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Bilioni 31.3

Aidha Msigwa amesema kuwa dimba la Uhuru litakuwa tayari mnamo Novemba 21 ambapo klabu hizo zinaweza pia kulitumia baada ya kufungwa kupisha matengenezo makubwa.

Dimba la Mkapa halitotumika tena kipindi cha matengenezo hayo labda kuwe na ulazima mkubwa katika mechi ambazo hazitoathiri matengezo, tafsiri yake ni kuwa hata mechi za CAF za Watani ni kizungumkuti.
 
Jaman c juzi tu walisema wamefanya ukatalrabati wa 30+ B🤔
 
🤣🤣🤣

Seems Kuna Hela Huwa zinapigwa sana ktk hiyo project maana Kila wakati uwanja una karabatiwa ty
 
Jaman c juzi tu walisema wamefanya ukatalrabati wa 30+ B🤔
Imagine 🤣🤣🤣🤣

Hii nchi ifutwe Kmmk
So means ukarabati wa 30+ B ulisharudisha faida ama niaje !?🤣🤣🤣
 
Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen ni kuwa Simba na Yanga watalazimika kutafuta viwanja vingine kwasababu dimba la Benjamin Mkapa litaendelea na matengenezo makubwa mwezi huu hivyo kupisha mchakato huo matumizi ya uwanja huo yatafungwa kwa muda.

Uwanja wa Mkapa umefungwa kwa kipindi cha miezi sita (6) kupisha ukarabati mwingine mkubwa kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali aliyenukuliwa na gazeti la The Citizen.

Msemaji Mkuu amesema mchezo wa Simba dhidi ya Namungo ndio ulikuwa mchezo wa mwisho kwa Mkapa ambapo Klabu hizo mbili Simba na Yanga zinapaswa kuchagua Chamazi (Mbagala) na Amaan (Zanzibar) kwa ajili ya mechi zao.

Soma: Serikali yakamilisha ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Bilioni 31.3

Aidha Msigwa amesema kuwa dimba la Uhuru litakuwa tayari mnamo Novemba 21 ambapo klabu hizo zinaweza pia kulitumia baada ya kufungwa kupisha matengenezo makubwa.

Dimba la Mkapa halitotumika tena kipindi cha matengenezo hayo labda kuwe na ulazima mkubwa katika mechi ambazo hazitoathiri matengezo, tafsiri yake ni kuwa hata mechi za CAF za Watani ni kizungumkuti.
CCM mitano tena.....dadadeki!
 
Akufukuzae hakwambii toka. Ni muda wa Yanga na Simba kujenga viwanja vyao
 
Msigwa anataka atajirikie ukarabati wa uwanja huo!!

Mechi tano tu wameanza kukana et hawakufanya ukarabati wa pitch.

CAG mwenyewe huwezi kuona reports kwenye hili.
 
Hela zinazotumika kuukarabati huo uwanja kila siku zingeweza kabisa kujenga uwanja mwingine mpya na wa kisasa! Na cha kushangaza hata kinacho karabatiwa chenyewe hata hakionekani kivile! Mara bilioni 31 zimetumika! Awamu hii sijui zitatumika bilioni ngapi!

Yaani ni wizi mtupu!
 
Huu uwanja UNATAKIWA uchunguzwe Kuna kitu kinaendelea
 
Huu Uwanja Kuna Ufisadi Mkubwa Unaendelea kuna Siku Sekeseke litaanzia uwanjani acha waendelee
 
Back
Top Bottom