Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Wakazi na mashabiki mbalimbali wamekuwa wakilalamikia hali ya huduma katika Uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza, Tanzania wakisema kuwa ukosefu wa vyoo vya kutosha ndani ya uwanja huo umekuwa changamoto kubwa.
Hali hiyo imewafanya baadhi ya watu kutumia maeneo ya pembeni ya uwanja huo kujisaidia, jambo linalozua kero ya usafi na harufu isiyofaa, hasa wakati wa mikusanyiko mikubwa ya michezo na matukio mbalimbali.
Soma Pia: Uwanja wa CCM KIRUMBA una matundu manne 4 tu ya vyoo
Nashauri uongozi husika kuchukua hatua za haraka kuboresha miundombinu ya vyoo ili kudhibiti tatizo hilo na kuhakikisha mazingira ya uwanja yanabaki safi na salama kwa watumiaji wote.
Mfano angalia tukio hili lililotokea wakati wa mchezo wa Nusu Fainali ya CRDB Bank Federation Cup 2025/2026 kati ya Azam FC na Yanga hakikuwa na afya kwa Watu.
Ufafanuzi ~ Meneja wa CCM Kirumba: Video ya watu wakijisaidia ovyo Kirumba ilipangwa ki-Propaganda ili kutuchafua