Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kipi cha ccm kiliwahi kuwa sawa?Wakazi na mashabiki mbalimbali wamekuwa wakilalamikia hali ya huduma katika Uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza, Tanzania wakisema kuwa ukosefu wa vyoo vya kutosha ndani ya uwanja huo umekuwa changamoto kubwa.
Hali hiyo imewafanya baadhi ya watu kutumia maeneo ya pembeni ya uwanja huo kujisaidia, jambo linalozua kero ya usafi na harufu isiyofaa, hasa wakati wa mikusanyiko mikubwa ya michezo na matukio mbalimbali.
Soma Pia: Uwanja wa CCM KIRUMBA una matundu manne 4 tu ya vyoo
Nashauri uongozi husika kuchukua hatua za haraka kuboresha miundombinu ya vyoo ili kudhibiti tatizo hilo na kuhakikisha mazingira ya uwanja yanabaki safi na salama kwa watumiaji wote.
Mfano angalia tukio hili lililotokea wakati wa mchezo wa Nusu Fainali ya CRDB Bank Federation Cup 2025/2026 kati ya Azam FC na Yanga hakikuwa na afya kwa Watu.
Halafu utasikia Mwigulu anasema wazungu wanatuonea wivu kwa kuwa tuna raslimali nyingi. Yaani mzungu atuonee wivu watu ambao tuko kwenye hatua ya kujisaidia vichakani?Aise hiki chama kinaweza nini sasa hivi viwanja kimepora hakiwezi kuviendesha yaani ustaarabu wa chini kabisa huanzia kwenye choo kama sehemu ya kujisaidia haipo safi jua fika hiyo jamii ni duni na hatari kuliko
Mambo ya mipira sijadili ndio yanasababusha watu kuwa wajinga sawa na dini na siasa za makeleleMambo ya ajabu sana,
ChoiceVariable fikisha malalamiko kwa mwenyekiti wa chama😁
Ni fremu za CCM hizo, watu wanakojoa hovyo hovyo.Mambo ya mipira sijadili ndio yanasababusha watu kuwa wajinga sawa na dini na siasa za makelele
Waulize Wana CCM,Mimi sio mwanachama waoNi fremu za CCM hizo, watu wanakojoa hovyo hovyo.
Wakazi na mashabiki mbalimbali wamekuwa wakilalamikia hali ya huduma katika Uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza, Tanzania wakisema kuwa ukosefu wa vyoo vya kutosha ndani ya uwanja huo umekuwa changamoto kubwa.