Uwanja wa gwambina unamilikiwa na nani?

Uwanja wa gwambina unamilikiwa na nani?

Kupitia mpira wadau wa mpira wilaya ya Misungwi mkoani mwanza wameamua kujenga uwanja mpya wa kisasa zaidi ambao uko nje kidogo na jijini la Mwanza wenye uwezo wa kubeba zaidi ya watazamaji elfu kumi na moja.

Akizungumzia kuhusu ujenzi huo ambao uko katika hatua ya mwisho meneja wa ujenzi Bw.Nyanda Mnyeti amesema kuwa walianza ujenzi kwa na mkandarasi mwingine ambaye alizungushia tofali na baadae wakapata mkandarasi mwingine ambaye alichimba na kuweka udongo ambayo unaofaa kwa ujenzi kama tofauti na awali.

Ameongeza kuwa uwanja huuo ni wa kisasa kwani ujenzi wa uwanja huo wamejifunza kupitia viwanja vya nje ya nchi ambapo maegesho ya magari yatakuwa nje wakati wa mechi huku makazi ya kocha,Viongozi na wachezaji watakuwa wanaishi karibu na uwanja ambapo kuna nyumba (Hostel) zao tayari za kuishi.
(Hii ni kwa mujibu wa tarifa za awali zizonikuliwa toka kwenye magazeti ya michezo)

Lakini leo wakati wa uzinduzi wa uwanja huo meneja Mnyeti ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Manyara amesema uwanja huo umegharimu kiasi cha shilingi 838,000,0000.

Akifafanua chanzo cha fedha killipopatikana kwaajili ya ujenzi huo, Mnyeti amesema alikopa Benki ya CRDB shilingi 300,000,000 kwaajili ya kujenga pitch na kiasi kingine aliuza magari yake binafsi 4, akapata shilingi 300,000,000, pia alisema alimuomba mke wake wauze gari yao ya kutembelea ndipo wakapata kiasi kilicho baki cha kumalizia uwanja huo.

View attachment 1133553View attachment 1133554
Hawa ndio watoto wa mfalme wanaoruhusiwa kufanya ufisadi wa kutisha bila kuguswa
 
Ule uwanja pitch yake ni nzuri sana ila tatizo ni kwamba umbali toka kwenye pitch hadi kwenye stands ni karibu sana yaani ni kama hatua tatu tu kitu ambacho ni hatari kwa afya na maisha ya wachezaji. Mf ile motion wanayokuwaga nayo wachezaji wanapokimbiza mpira halafu wakapigana vikumbo au tackles mtu anaweza kwenda kujibamiza kwenye jukwaa. Halafu ameubana sana ilifikia kipindi mipira kama mitatu au minne hivi ilipigwa ikavuka paa la jukwaa na kutoka nje kabisa. Kwa mahali kama uswahilini hivi hyo mipira inakuwa ni sadaka,na hivi tff huwa wana mpira mmoja tu basi hata mechi inaweza ishia hapohapo. Ila amejitahidi sanaaa mana si vema kubeza ilihali Simba na Yanga hawana hata sehemu ya kufanyia mazoezi
 
Kwenye hio habari kuna maneno haya
"Lakini leo wakati wa uzinduzi wa uwanja huo meneja Mnyeti ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Manyara amesema uwanja huo umegharimu kiasi cha shilingi 838,000,0000."

Wewe hujayaona hayo au ni msukuma wewe?
Hivi hiyo figure ya 838,000,000 inatamkwaje hapo? Ulimaanisha au ni error?
 
Huu uwanja na ule wa Mo kule bunju upi mzur? Maana Simba hawana uwanja watakuwa wanatumia wa Mo
 
Ni kweli jukwaa na pitch vipo karibu sana. Arsenal waliwahi kuwa na ttz km hili pale Highbury London, tulikuwa tunapata changamoto sisi mashabiki kuwadaka wachezaji waliosukumwa huko japo advantage ilikuwa rahisi kuomba jezi ama kumpa mkono mchezaji km nlivofanya mm kwa Thierry Henry ktk ile mechi ya UEFA Arsenal v Inter Milan ambayo arsenal alibidua meza kibabe kwa ushindi wa 5-1 baada ya kupigwa 3-1 Milan!
Ule uwanja pitch yake ni nzuri sana ila tatizo ni kwamba umbali toka kwenye pitch hadi kwenye stands ni karibu sana yaani ni kama hatua tatu tu kitu ambacho ni hatari kwa afya na maisha ya wachezaji. Mf ile motion wanayokuwaga nayo wachezaji wanapokimbiza mpira halafu wakapigana vikumbo au tackles mtu anaweza kwenda kujibamiza kwenye jukwaa. Halafu ameubana sana ilifikia kipindi mipira kama mitatu au minne hivi ilipigwa ikavuka paa la jukwaa na kutoka nje kabisa. Kwa mahali kama uswahilini hivi hyo mipira inakuwa ni sadaka,na hivi tff huwa wana mpira mmoja tu basi hata mechi inaweza ishia hapohapo. Ila amejitahidi sanaaa mana si vema kubeza ilihali Simba na Yanga hawana hata sehemu ya kufanyia mazoezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom