Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Katika pitapita zangu nyumbani kwenye albamu nikaja kukutana na hii picha ya UWANJA WA JANGWANI aisee nilipatwa na simanzi nzito nilipoona huu uwanja kwani kuna kumbukumbu ilinijia kipindi hicho natumwa na mmoja ya mabosi zangu kuja kuuza Ice cream na bei ya askilimu likuwa ni shilling 10.
Panapotokea mechi kali kama vile za Villa squard , Tambaza nk basi huwa namaliza kuuza mpaka Ice cream mia tàtu,( 300) maana kipindi hicho muda wa mapumziko ya wachezaji basi mwendo wa kula ice cream tuu
Na pia nakumbuka tarehe 27/09/1999 tukikusanyika ktk huu uwanja watu wa Imani za dini mbalimbali kuja kufanya maombi ya kumuombea mwl Nyerere maana Rais mkapa alituambia Hali ya Mwalimu ilikuwa mbaya sana hivyo tuzidishe Dua na maombi.
Huu uwanja ulikuwa na manufaa mkubwa sana kwetu na tulikuwa hatuna sehemu ya kwenda kumwagilia moyo zaidi ya kuja huku aidha kuangalia mpira au kusikilkza miziki ya injili pamoja na kuwasikiliza wahubiri mbalimbali wa kimataifa walikuwa wakija kuweka kambi daaahhh ilikuwa Raha, akina Reinhard Boke, TLS Osbon, Morris CErrulo, Don Moen, Billy Graham, Egon Falk , Ask Emmanuel Mwasha lazaro, Getrude, Kakobe na Mwakasege.
Shetani bhana, kaona injili inamchoma akatumia mbinu , au ni mawazo ya wajinga kumsingizia shetani? Nani alaumiwe kwa kinachoendelea pale ?
CJUI NANI KAUHARIBU UWANJA WETU KAMA NI MAFURIKO MBONA MVUA ZILIKUWA ZINANYESHA NA UWANJA ULIENDELEA KUWA SALAMA??