Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro uboreshwe

Nakunga mkono sehemu kubwa ya maoni yako. Uwanja wa ndege unapanuliwa kulingana na idadi ya ndege na wasafiri wanaotumia. Huwezi kuweka shopping centers nying na kubwa wakati watumiaji ni wachache. Kitu ambacho sikubaliani na wewe ni hili la kusema ukijenga hotel pale basi hotel za Arusha na Moshi zitakosa wateja na wasafirishaji watakosa soko. Pale panatakiwa paboreshwe na ikiwezekana wajenge hotel moja hata ndogo bila kuathiri mazingira.
 
Mkuu doha ni transit tu. Usikute katokea newzealand, Australia, Canada ama marekani huko.
Kwani ukitokea Australia huwezi kua mshamba?
Elewa kwamba hata Canada Kuna washamba Kama ilivyo Shinyanga.
Vile vile kumbuka ushamba Ni kipaji Kama upumbavu au urefu.
 
Ingependeza serikali iweke wazi juu ya ubinafsiswaji wa KIA Airport ili tujue nani ndiye mwajibikaji kwa sasa
Kweli kabisa maana uwazi ni uwajibakaji ulio bora maana ni mali ya umma ile.
 
Pale KIA ilikatazwa kuuendeleza mjini Kwa kiwango Cha matofali. Njia panda pale nna kiwanja kikubwa karibu na stendi nilitaka tengeneza Hotel na ofisi Kwa ajili ya tours company nikaambiwa na mamlaka kuwa siruhusiwi kujenga jengo la mwinuko. Na pale njia panda upande wa kushoto ni Arusha ambao wameruhusu na upande wa kulia ni Moshi wamekataza
 
Kwanza priority iwe kupunguza landing fees na tozo zingine ili kiwanja cha KIA kiweze kutumika na ndege nyingi zaidi.Makampuni mengi ya Ndege ya mechagua kutumia Uwanja wa Jomo Kenyatta kwa sababu ya landing fees nafuu na kodi.Baada ya kufanikiwa kuyashawishi Mashirika ya Ndege kuutumia uwanja huo kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya kazi ndio kiwanja kipanuliwe ili kukidhi mahitaji yatakayojitokeza.
Mashirika ya Ndege yanayotumia uwanja huo kwa sasa sio mengi ndio maana tiketi mpaka Kilimanjaro ni ghali sana kulinganisha na Nairobi na Dar.
 
Jadili hoja iliyoletwa, usimjadili metal hoja. Tujifunze kufanya debate kwa ustaarabu
Labda nileleze wapi nimemjadili mtu kwenye andiko langu au nimeongea kipi kibaya? Milichoweka ni history fupi ya kiwanja na nimekubaliana naye baadhi ya maeneo na mengine nimepingana naye tatizo ni lipi kupinga baadhi ya hoja?
 
Serikali yetu huwa haina wabeba maono
 
Gardening!
Recreation!

Palm Trees na Nyinginezo!

Avenue Road kutoka Airport mpk Arusha Road!

Yaani ule uwanja ungekuwa Garden kama zile za Mount Meru Hotels ule uwanja ungetulia sanaaaa

Lsnd Scape inahusu na ikiwezekana wakabidhi watu binafsi!

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…