Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro uboreshwe

Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro uboreshwe

Kwanaza kabisa unatakiwa utambue huo uwanja ulijengwa kwenye eneo ambalo lilikuwa ni nia ya wanyama kuhama toka Arusha kwenda Kilimanjaro. Uwanja huo ulijengwa na Waisraeli enzi ya Hayati Mwalimu Nyerere baada ya kuona watalii wanashukia Nairobi kwa ajili ya kuja kupanda mlima Kilimanjaro. Turudi kwenye mada yako ni kweli kwa sasa uwanja unahitaji baadhi ya vitu siyo tu kwa watalii wanaotembelea hata wananchi wanaokwenda kupokea wageni. Inasikitisha hakuna sehemu nzuri ya kukaa kama Dar Es Salaam ambapo utapata huduma ya chakula na kinywaji na hata screen kwa kuangalia news na mambo mengine. Yes hata jengo lingeangaliwa upya liendane na mahitaji ya sasa kama eneo la kuondoka wageni ni dogo na hata wanaowasili. Lakini pia magetini kumekuwa na njia moja ya kuingia na moja ya kutoka kitu ambacho kinaleta foleni kubwa sana kwa wanaoingia na kuondoka uwanjani. Kwenye hoteli hapo kidogo ntatofautiana na wewe kwani ukishaweka hoteli maeneo hayo kunaweza changia mahoteli ya Arusha na Moshi kukosa boashara lakini pia kwa wenzetu wanaofanya biashara ya usafirishaji. Uzuri uliopo wa asili ndiyo kivutio kikubwa mandhari ya ukiwa unatoka KIA kuelekea Arusha-Moshi Road unaweza uona mlima Kilimanjaro kwa ukaribu na unavyopendeza.Kumbuka lengo la watalii ni kuja kuona vivutio vilivyopo hasa Mlima na Mbuga. Sasa tukijenga mahoteli ile madhari yote ya kivutio kuwa uwanja wa ndege upo kwenye mazingira ya kitalii itapoteza maana.
Nakunga mkono sehemu kubwa ya maoni yako. Uwanja wa ndege unapanuliwa kulingana na idadi ya ndege na wasafiri wanaotumia. Huwezi kuweka shopping centers nying na kubwa wakati watumiaji ni wachache. Kitu ambacho sikubaliani na wewe ni hili la kusema ukijenga hotel pale basi hotel za Arusha na Moshi zitakosa wateja na wasafirishaji watakosa soko. Pale panatakiwa paboreshwe na ikiwezekana wajenge hotel moja hata ndogo bila kuathiri mazingira.
 
Mkuu doha ni transit tu. Usikute katokea newzealand, Australia, Canada ama marekani huko.
Kwani ukitokea Australia huwezi kua mshamba?
Elewa kwamba hata Canada Kuna washamba Kama ilivyo Shinyanga.
Vile vile kumbuka ushamba Ni kipaji Kama upumbavu au urefu.
 
KIA Airport mimepita karibuni nikitokea Doha, walishuka watalii zaidi 200.

Bahati ilikuwa asubuhi nimeweza kuona vizuri mandhari na mazingira yake, ni Airport iliyo eneo zuri na panaweza kuwezeshwa kuwa Airport ya kipekee hapa nchini kwani pana nafasi kubwa sana ya kuwezesha kujenga runways kwa namna yo yote kuwezesha ndege kutua kwa usalama zaidi.

Jambo la kushangaza Airport hii ni ya miaka mingi tangu zama za Nyerere na ikiwa ni gate way ya watalii, lakini anayefika kwa mara ya kwanza anaweza kupata wasiwadi maana panaonekana ni porini kana kwamba ndege imetua Loliondo au Seronela.

Abiria hushuka kwenye ndege na kutembea kwa miguu kwenda nyumba ya checkout for security checkpoint, hiyo ni international Airport. Sikuona movement ya huduma kwa disable passengers.

Pako kimya sana, na hakuna hata jengo la hotel lililo karibu na Airport hata lodge hakuna. International Airports nilizoona nchi mbalimbali bara la Ulaya, Asia na America pale pale Airport huwa kuna hoteli za kitali. Mjini Arusha na Moshi yes zipo lakini baadhi hupendelea karibu na airport.

Kawaida mazingira ya Airport husaidia watalii kupata picha ya hali ya nchi ilivyo kwa maendeleo na uchumi, kwa hali ilivyo ukiongozana na wageni wakati ulikotokea nao ulijidai na ukifika utaanza kujisikia vibaya.

Nashauri serikali iwe na mipango ya kuboresha KIA Airport kwa kujenga hotel za kitalii kwa kuwa KIA ni gate way ya watalii nchini.

Pafunguliwe shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kiuchumi ili kuwezesha kuondoa hali iliyopo inayoonekana ndege imetua porini.

Serikal8 pia ifungue milango kwa wawekezaji ili wapapendezeshe KIA yetu.

Pale KIA Airport pajengwe jengo lenye hadhi ya shughuli za Airport kwa mazingira ya kuvutia watalii na wawekezaji.

Jamani KIA serikali ifungue macho zaidi, utalii huliingizia taifa pesa za kutosha kila mwaka. Itapendeza KIA kwa sasa iende na wakati.

TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE!
Pale KIA ilikatazwa kuuendeleza mjini Kwa kiwango Cha matofali. Njia panda pale nna kiwanja kikubwa karibu na stendi nilitaka tengeneza Hotel na ofisi Kwa ajili ya tours company nikaambiwa na mamlaka kuwa siruhusiwi kujenga jengo la mwinuko. Na pale njia panda upande wa kushoto ni Arusha ambao wameruhusu na upande wa kulia ni Moshi wamekataza
 
Kwanza priority iwe kupunguza landing fees na tozo zingine ili kiwanja cha KIA kiweze kutumika na ndege nyingi zaidi.Makampuni mengi ya Ndege ya mechagua kutumia Uwanja wa Jomo Kenyatta kwa sababu ya landing fees nafuu na kodi.Baada ya kufanikiwa kuyashawishi Mashirika ya Ndege kuutumia uwanja huo kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya kazi ndio kiwanja kipanuliwe ili kukidhi mahitaji yatakayojitokeza.
Mashirika ya Ndege yanayotumia uwanja huo kwa sasa sio mengi ndio maana tiketi mpaka Kilimanjaro ni ghali sana kulinganisha na Nairobi na Dar.
 
Jadili hoja iliyoletwa, usimjadili metal hoja. Tujifunze kufanya debate kwa ustaarabu
Labda nileleze wapi nimemjadili mtu kwenye andiko langu au nimeongea kipi kibaya? Milichoweka ni history fupi ya kiwanja na nimekubaliana naye baadhi ya maeneo na mengine nimepingana naye tatizo ni lipi kupinga baadhi ya hoja?
 
Serikali yetu huwa haina wabeba maono
 
KIA Airport mimepita karibuni nikitokea Doha, walishuka watalii zaidi 200.

Bahati ilikuwa asubuhi nimeweza kuona vizuri mandhari na mazingira yake, ni Airport iliyo eneo zuri na panaweza kuwezeshwa kuwa Airport ya kipekee hapa nchini kwani pana nafasi kubwa sana ya kuwezesha kujenga runways kwa namna yo yote kuwezesha ndege kutua kwa usalama zaidi.

Jambo la kushangaza Airport hii ni ya miaka mingi tangu zama za Nyerere na ikiwa ni gate way ya watalii, lakini anayefika kwa mara ya kwanza anaweza kupata wasiwadi maana panaonekana ni porini kana kwamba ndege imetua Loliondo au Seronela.

Abiria hushuka kwenye ndege na kutembea kwa miguu kwenda nyumba ya checkout for security checkpoint, hiyo ni international Airport. Sikuona movement ya huduma kwa disable passengers.

Pako kimya sana, na hakuna hata jengo la hotel lililo karibu na Airport hata lodge hakuna. International Airports nilizoona nchi mbalimbali bara la Ulaya, Asia na America pale pale Airport huwa kuna hoteli za kitali. Mjini Arusha na Moshi yes zipo lakini baadhi hupendelea karibu na airport.

Kawaida mazingira ya Airport husaidia watalii kupata picha ya hali ya nchi ilivyo kwa maendeleo na uchumi, kwa hali ilivyo ukiongozana na wageni wakati ulikotokea nao ulijidai na ukifika utaanza kujisikia vibaya.

Nashauri serikali iwe na mipango ya kuboresha KIA Airport kwa kujenga hotel za kitalii kwa kuwa KIA ni gate way ya watalii nchini.

Pafunguliwe shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kiuchumi ili kuwezesha kuondoa hali iliyopo inayoonekana ndege imetua porini.

Serikal8 pia ifungue milango kwa wawekezaji ili wapapendezeshe KIA yetu.

Pale KIA Airport pajengwe jengo lenye hadhi ya shughuli za Airport kwa mazingira ya kuvutia watalii na wawekezaji.

Jamani KIA serikali ifungue macho zaidi, utalii huliingizia taifa pesa za kutosha kila mwaka. Itapendeza KIA kwa sasa iende na wakati.

TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE!
Gardening!
Recreation!

Palm Trees na Nyinginezo!

Avenue Road kutoka Airport mpk Arusha Road!

Yaani ule uwanja ungekuwa Garden kama zile za Mount Meru Hotels ule uwanja ungetulia sanaaaa

Lsnd Scape inahusu na ikiwezekana wakabidhi watu binafsi!

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom