Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Plato...Mohammed Said Mimi si mjuzi wa lugha, unaweza kupitia aya ya kwanza kwenye bandiko namba 15 juu ya maelezo ya Sal Davis.
Hapafu naona umeghabidhika sana bila sababu kumhusu Azarel. Pengine hajarejea kwa sababu Jukwaa hili la historia si maarufu hapa Jf kwa uchangiaji
Hata mie si mjuzi hivyo wa lugha hii na nimeeleza kwenye jibu langu
kuwa ikishakuwa lugha si yako ni ya kujifunza hutoweza kukwepa
kukosea.
Na nikamshukuru nikasahihisha.
Lakini sikupendezewa na namna alivyozungumza na mimi hakuwa
muungwana.
Nashangaa kuwa wewe hili hulioni.
Hebu msome upya.
Kaonyesha kukosa adabu ya elimu na hicho ndicho nilichomuasa.
Bahati mbaya unamjibia wewe.
Ama hili la kuwa Jukuwaa la Historia si maarufu sijui uhakika wake
lakini mimi nimefahamika na wengi na nimefanya mijadala mingi
ya kuvutia hapa.
Fanya utafiti kuthibitisha hili.
Kuhusu mstari wa 15 nifahamishe ikiwa pana kosa nitasahihisha.
Umetumia neno ''aya,'' kwangu mimi ''aya,'' ni kitu kingine kabisa.
Kuhusu, ''kughadhibika sana bila sababu,'' hapana sijaghadhibika.
Ningeghadhibika ningeandika fedhuli kama alivyofanya yeye.
Ila nimetaka anifahamu na nimlipe kwa wema wake.
Yeye kanisaidia kusahihisha mswada wa kitabu changu nami
nimehisi nina deni kwake la kumfunza kuwa kuna adabu ya elimu
ili na yeye anufaike kama nilivyonufaika mimi kwa ujuzi wake.