Uwanja wa Mkapa kufanyiwa maboresho makubwa kwa michuano ya Africa Super League

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Uwanja wa Mkapa kufanyiwa maboresho makubwa kwa michuano ya Africa Super League

Serikali imeahidi kufanya marekebisho makubwa yanayohitajika katika uwanja wa Benjamin Mkapa ili kukidhi viwango vya kimataifa vinavyohitajika katika michuano ya Africa Super League ambayo Klabu ya Simba ndio mwakalishi wa ukanda wa Afrika Mashariki.

Hayo yamesemwa na Bwana Saidi Yakubu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo alipokutana na uongozi wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ambao unaongozwa na Bw.Mohammad Sidat, Mkuu wa Kitengo cha ufundi alieambatana na wataalaam kutoka Italia waliokodiwa na Shirikisho hilo.

Bwana Yakubu alieleza kuwa maeneo yote yaliyoainishwa yatafanyiwa kazi kabla ya ziara nyingine ya ukaguzi itakayofanywa na CAF.

Aidha, Bwana Yakubu pia aliwaeleza viongozi hao kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inakusudia kujenga viwanja vingine vya michezo na watategemea sana miongozo ya kitaalamu toka FIFA na CAF.

Kwa upande wao, Ujumbe huo wa CAF waliarifu kuhusu hatua za haraka zinazotakiwa kufanywa ili uwanja uendelee kutumika kimataifa na kupongeza maendeleo ya soka nchini.

Uongozi wa klabu ya Simba uliandaa hafla hiyo ya chakula cha jioni iliyohudhuriwa pia na Naibu Spika,Mussa Azzan Zungu kwa nia ya kufanya tathmini baada ya ukaguzi kufanyika.

IMG-20230217-WA0006.jpg

IMG-20230217-WA0010.jpg
IMG-20230217-WA0009.jpg
IMG-20230217-WA0008.jpg
 
Unajua kama unaona mbali Kuna kitu inakuja inaitwa word super leauge Benjamin lazima ifanyiwe ukarabati wakufa mtu ili kuweze kualika vilabu vikubwa vya Dunia uo ukarabati sio Kwa ajili ya Ahaly Wala esperance
 
Hivi ujenzi wa huu uwanja uliishaga au kuna phase zingine zilikuwa zifanyike? Nakumbuka mipango ya awali walikuwa wanaongelea kujenga hoteli, maduka, migahawa mule mule ndani. Sidhani kama hata idadi ya vyoo inaakisi mahitaji ya uwanja siku za mechi.

Serikali ingeacha tabia za kusubiri watu kutoka nje watuambie vitu vya kuboresha wakati sisi wenyewe wananchi huwa tunavisema.
 
Unajua kama unaona mbali Kuna kitu inakuja inaitwa word super leauge Benjamin lazima ifanyiwe ukarabati wakufa mtu ili kuweze kualika vilabu vikubwa vya Dunia uo ukarabati sio Kwa ajili ya Ahaly Wala esperance
Malengo ya sasa ya mafanikio kwa Simba ni nusu fainali ya Champions league ila imagine ichukue kombe halafu ikacheze FIFA Club World Cup na wanyama wenzie kina Real Madrid na Flamengo, oyaaa.

Chama langu endeleeni kupambana na kuboresha kikosi, nyama ziko chini.
 
Achaga ndoto za kijinga.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Uwanja wa Mkapa kufanyiwa maboresho makubwa kwa michuano ya Africa Super League

Serikali imeahidi kufanya marekebisho makubwa yanayohitajika katika uwanja wa Benjamin Mkapa ili kukidhi viwango vya kimataifa vinavyohitajika katika michuano ya Africa Super League ambayo Klabu ya Simba ndio mwakalishi wa ukanda wa Afrika Mashariki.

Hayo yamesemwa na Bwana Saidi Yakubu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo alipokutana na uongozi wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ambao unaongozwa na Bw.Mohammad Sidat,Mkuu wa Kitengo cha ufundi alieambatana na wataalaam kutoka Italia waliokodiwa na Shirikisho hilo.

Bwana Yakubu alieleza kuwa maeneo yote yaliyoainishwa yatafanyiwa kazi kabla ya ziara nyingine ya ukaguzi itakayofanywa na CAF.

Aidha,Bwana Yakubu pia aliwaeleza viongozi hao kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inakusudia kujenga viwanja vingine vya michezo na watategemea sana miongozo ya kitaalamu toka FIFA na CAF.

Kwa upande wao, Ujumbe huo wa CAF waliarifu kuhusu hatua za haraka zinazotakiwa kufanywa ili uwanja uendelee kutumika kimataifa na kupongeza maendeleo ya soka nchini.

Uongozi wa klabu ya Simba uliandaa hafla hiyo ya chakula cha jioni iliyohudhuriwa pia na Naibu Spika,Mussa Azzan Zungu kwa nia ya kufanya tathmini baada ya ukaguzi kufanyika.

Wanatafutwa "wabunge" wa viti maalum.

Back
Top Bottom