KWELI Uwanja wa Mkapa kufungwa kwa muda baada ya CAF kushauri uboreshwe

KWELI Uwanja wa Mkapa kufungwa kwa muda baada ya CAF kushauri uboreshwe

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Asubuhi ya leo, Februari 22, 2023, kumekuwepo taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikisema kuwa Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) limeufungia uwanja wa Mkapa kutokutumika kwa mwezi mmoja ili kuruhusu kufanyika kwa maboresho ya sehemu ya kuchezea (Pitch) ambayo imeharibika na kukosa ubora unaotakiwa.

Tanzania_National_Main_Stadium_Aerial.jpg
 
Tunachokijua
Baada ya kuibuka tetesi zinazodai kuwa Uwanja wa Mkapa umefungwa na CAF, JamiiForums imefanya mawasiliano na Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo Ili kupata ufafanuzi.

Ndimbo amesema “Hizo taarifa hazina ukweli hata kidogo, wanaosambaza waache kuupotosha umma. Kilichotokea ni wakaguzi wa CAF (Shirikisho la Soka la Afrika) walikuja kuukagua Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya michuano ya Super League kisha wakatoa mapendekezo ya nini kifanyie, ambayo yanafanyiwa kazi.”

Zaidi ya hayo, inaelezwa kuwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limeshauri Uwanja wa Benjamini Mkapa uliopo jijini Dar es Salaam kutotumika kwenye mechi zao kwa kile kilichoelezwa kuwa umeharibika eneo la kuchezea (pitch), ambapo sasa utafungwa kwa mwezi mmoja kupisha marekebisho.

Hivyo basi, baada ya mechi ya leo Jumatano, Februari 22, 2023 ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya KMC, itakayochezwa kuanzia saa 10:00 jioni uwanja huo utafungwa.

Kwa mujibu wa matumizi ya uwanja huo, unapaswa kutumika mara tatu kwa wiki lakini hadi leo itakuwa ni mara ya nne kinyume na matumizi ya uwanja huo ambao hata kabla ya hapo ulilalamikiwa kutokuwa katika hali nzuri hasa eneo la kuchezea (pitch), kwani matumizi yamekuwa makubwa.

Meneja wa Uwanja anena
Meneja wa Uwanja huo, Salum Mtumbuka ameeleza kuwa baada ya mechi mbili za CAF zilizochezwa wikiendi iliyopita walikutana na maofisa hao ambao waliwapa maelekezo namna ya kufanya marekebisho hasa eneo la kuchezea.

"Simba na Yanga ndiyo wanaotumia huu uwanja kama uwanja wao wa nyumbani, ila ndani ya kipindi cha marekebisho haya hawatatumia mechi zao za Ligi Kuu kwenye uwanja huu, tunawapa Uwanja wa Uhuru ama watakavyoona wao," alisema.

Ukweli wa taarifa hii ukoje?
Si kweli kuwa uwanja huu umefungiwa na CAF bali Wakaguzi wa CAF walitoa mapendekezo ya kufanya maboresho na marekebisho katika sehemu mbalimbali za uwanja ikiwamo sehemu ya kuchezea. Hivyo TFF imechukua hatua ya kuufunga uwanja huu kwa muda ili kufanikisha marekebisho.
Asubuhi ya leo, Februari 22, 2023, kumekuwepo taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikisema kuwa Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) limeufungia uwanja wa Mkapa kutokutumika kwa mwezi mmoja ili kuruhusu kufanyika kwa maboresho ya sehemu ya kuchezea (Pitch) ambayo imeharibika na kukosa ubora unaotakiwa.

View attachment 2525875
Hapa tofauti ni nini? Kufungwa na kutotumika mpaka ufanyiwe marekebisho, ujumbe ni mmoja.
WaTz tuwe na utamaduni wa kutunza mali zetu, zinaingiza pesa ila matunzo duni, hadi vinaharibika.
 
ndio kabisa bora hata wameona make uwanja ulianza kuaribika
 
Back
Top Bottom