- Source #1
- View Source #1
Wakuu hii taarifa ina ukweli kiasi gani?
- Tunachokijua
- Kuanzia Machi 28, 2026 Marekani na Israel waliishambulia Iran hali iliyopelekea kuanza kwa mgogoro baina ya mataifa hayo. Toka kuanza kwa mgogoro huo kumekuwa na mashambulizi kadhaa miongoni mwa mataifa hayo na mataifa washirika.
Madai
April 02, 2026 kumekuwa na picha inayosambaa kupitia mtandao wa X ikionesha uwanja wa ndege ulioshambuliwa huku ndege kadhaa zikionekana kuungua na nyingine ikiendelea kuwaka moto ni kueleza kuwa ni shambulizi katika uwanja wa ndege nchini Israel.
Mtumiaji mmoja amechapisha picha hiyo na ujumbe unaosomeka;
"Israeli airport destruction scenes — May Allah completely destroy Israel. Everyone say Ameen."
Uhalisia wa Taarifa pamoja na picha hiyo
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji kwa njia ya mtandao na kubaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Hakuna taarifa yoyote kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika ulimwenguni waliochapisha taarifa ya kushambuliwa kwa uwanja wa ndege nchini Israel kushambuliwa Aprili 02, 2026.
Picha iliyoambatanishwa na Taarifa hiyo pia siyo halisi ila imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya AKili Unde (AI). Nyenzo ya kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa AI ya Hive moderation inabainisha kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa teknolojia hiyo kwa zaidi ya 99% na AI iliyotumika ni Gemini.