Uwanja wa Sheikh Amri Abeid | Vodacom Premier League VPL, Coastal Union Vs Simba SC

Uwanja wa Sheikh Amri Abeid | Vodacom Premier League VPL, Coastal Union Vs Simba SC

Leo nashangilia mara mbili. Timu yangu inashinda pia mkeka ushatiki.
 
Issa Abushehe anatandika shutiiii kali lakini linatoka nje lango..!

Ilikuwa hatari sana lango la Simba
 
Mechi na Tunisia Boko hata kutuliza mpira hawezi,eti leo na yeye star.
 
Uzuri wa Coast hawanaga masifa kama kina Ruvu shooting.
 
34' gooo laaaaaa, Difenda wa Coastal anaokoa bao la wazi kwenye chaki

Mpira uliopigwa na Nyoni, ilikuwa hatari sana
 
37' Bocco Gooooooooooooal goooooal

John Bocco anaandika bao la nne (Hat-Tick) akifumua shuti kutoka kwenye mstari wa D na kuzama wavuni moja kwa moja akimuacha golikipa Abbas akichumpa bila mafanikio.

Coastal Union 0-4 Simba SC
 
41' mpira umesimama baada ya golikipa Abbas wa Coastal kupata rabsha huku Kocha Mgunda akitoa maelekezo kwa wachezaji wake

Amesimama mpira unaendelea
 
45+2' Goooooal gooooooooaaal Morisson

Bernard Morrison anatandika shutiiii kali na kuzama wavuni kuandika bao tano.

Coastal Union 0-5 Simba SC

Naaam mpira ni mapumziko uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha
 
download.png
vs
download (1).png
 
Back
Top Bottom