Uwanja wa Sheikh Amri Abeid | Vodacom Premier League VPL, Coastal Union Vs Simba SC

Uwanja wa Sheikh Amri Abeid | Vodacom Premier League VPL, Coastal Union Vs Simba SC

90+3'

Ni wakati wa Sambusa uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Vodacom Premier League ambapo Simba wanaongoza kwa mabao Saba bila majibu.

Manula kwake Ame, anacheza kwake Ndemla, inapigwaa lakini wanachukua Coastal Union

Naaam mpira umekwishaaaa ambapo Simba wanaibuka kwa mabao Saba bila majibu

Ghazwat.....

Coastal Union 0-7 Simba SC
 
Alihamndulilahi walahi swadakta takbir subaana wataala
 
Wewe ndo mzigo. Nadhani wewe ni Yanga mwenzangu unataka kujifanya Simba. Onyango ni bongea beki mtulivu sana. Mnyama mugalu nashukuru hakucheza siku ile tumetoa draw,Larry sisi Yanga tuliporwa kihuni. Ni bonge la mchezaji.


HATA KAMA TUNASHIDA.
1. JOASH ONYANGO.
2. PASCAL WAWA.
3. GERSON FLAGA.
4. KAHATA NYAMBURA.
5. CRISS MUGALU.
6. LARRY BWALYA.

NAMTAFAKARI MORISON....BENARD MORISON

HAWA NI WACHEZAJI MIZIGO KWA SIMBA WOOTE WAONDOKE.
 
Sisi Simba sc hatuzitaki hizo Billion 20 Mo hizo atuzitaki jamaaaaaaaaani
 
Ila pamoja na kushinda Dilunga amekuwa mlaini sana akiguswa kidogo kaanguka ile mechi ya kazi ns Tunisia asingeweza kucheza.
Wawa leo amepoteza mipira mingi kwa pasi ndefu kwani ilikuwa haifiki sehemu sahihi.
Nyoni ameendelea kuonyedha ubora wake.
 
Kijiwe Cha wahenga[emoji2957][emoji2957]
255737905502_status_eb34436e99b54edea5936ad6b6feb266.jpg
 
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kuvurumishwa leo November 21, 2020 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha, ambapo Wagosi wa Kaya, Coastal Union, wanapambana na Mnyama Mkali, Simba SC.

Ni mechi kali na ya kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 za mchezo huku kila timu ikihitaji alama tatu muhimu VPL.

Kocha wa Coastal Union Juma Mgunda amesema wao wapo tayari kabisa kwenye mchezo huu, huku akisisitiza kwa wachezaji wake kuwa makini wawapo uwanjani.

Na upande wake Kocha wa Simba SC Sven Vanderbroeck amesema wanatarajia kukutana na ushindani kwani mechi haitakuwa rahisi, lakini tupo tayari kwa mapambano.

Kumbuka mtanange huu wa VPL ni kuanzia saa 10: 00 jioni.. Usikose Ukaambiwa.

Kulipewa Mwana.. Kulitaka Mwana

Update,

Timu ya Simba SC wakiwa ugenini wameitandika bila huruma Coastal Union mabao 7-0 kwenye Ligi Kuu Tanzania VPL' mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco amefunga mabao 3 Hat-Tick, Cloutius Chama mabao 2 huku Dilunga na Morrison wakifunga bao 2 kwa mmoja.



View attachment 1631473
Simba kama CCM.

#MITANOTENA.


SIMBA TUNASENA

#UBINGWATENAVPL.
 
Ongera kwa kupata pt 3, Ila mnacheza Kama walevi, sijaona biriyani bali mataputapu.
 
Back
Top Bottom