Uwanja wa Simba Bunju Wanoga

Uwanja wa Simba Bunju Wanoga

MO amepiga pesa sana hapo kwenye huo ujenzi wa viwanja. sijaona uwanja wa ajabu hapo, yaani mwekezaji wa bilioni 20 anashindawa kujenga uwanja aibu sana
Lile bwawa pale kwenye lile gofu mmeshindwa kufuga samaki mlishe wachezaji mmeishia kujaza fusi, nyie ndio chazo cha mbu muhimbili
 
Hapa ndio umeharibu sasa.

Azam ana Uwanja miaka nenda rudi ambao unachezewa mpaka mechi za Kimataifa na hakuna aliyejinyonga ije kuwa huo ambao hata majukwaa hauna. [emoji848]

Tooba. [emoji2088][emoji2088][emoji2088]
Unaongea kinyoooonge ule wenu ndondo cup unaanza lini
 
Ungekuwa unanifahamu kwanza ungeona aibu hata kufungua mdomo kuongea au kuogopa kabisa kuanza kujibizana NA Mimi. Unataka nikuambie Mali nilizonazo NA kipato nilichonacho ili uwajulishe TRA wanipe Kesi ya uhujumu uchumi wa Tz kusudi niingie kwenye mapatano haramu NA Serikali ya kugawana Mali zangu na ili ipate pesa za kumalizia miradi yao ya ujenzi wa ma-fly over ya Ubungo, SGR, Stiglers , etc?? sitanasa kwenye mtego huo kamwe.

Anyway, Ni kweli kabisa kuwa Mimi ninaishi ktk nyumba ya kupanga , KWA sababu siwezi kujenga nyumba kwenye nchi za Watu ugenini.Huku Mimi nachuma tu pesa Lakini kujenga nyumbani Tz, isitoshe nchi yao yenyewe tayari imeshajengeka yote imemalizika NA hakuna Ardhi tena iliyobaki wazi ambayo Unaweza kujenga nyumba, labda ununue nyumba kisha uibomoe NA hatimaye uweze kujenga tena nyumba nyingine.
Subiri tuje tukuopoe jangwani na mvua hizi, huna hela wewe kutwa unashinda pale makumbusho ya club kucheza bao.
 
Tanzania bado kuna safari ndefu sana ktk suala zima LA maendeleo endelevu.
Timu za Simba NA Yanga kama zingekuwa kwenye nchi zingine hadi Leo hii ndio zingekuwa timu "bilionea" KWA ukwasi WA pesa. Kununua tu kiwanja basi Watz wameona kama timu imeendelea sana kumbe Ni majanga tupu.Kutokana NA ukongwe WA timu hizi, mpaka sasa ingekuwa hata NA viwanja viwili vikubwa vya kuweza kuchukua watazamaji angalau 45,000 kwenye kila mji mkubwa hapa nchini Tz. KWA kuwa vichwani KWA Watu weusi wengi hakuna kitu matokeo yake ndio hivi tena
sawa mtu wa blue>
 
Wenye wivu wajinyonge baba wenye wivu wajinyonge *2
Hajinyongi MTU hapa labda awe mnyalu, ila tutajipanga kushinda changamoto tulizonazo na kufanya mambo mazuri zaidi ya mliyofanya. Wivu wa maendeleo rukusa
 
Wakati wowote Simba itaanza kujifua kwenye uwanja wake ulioko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam baada ya kukamilika kwa uwanja wa nyasi asili

Kwa sasa matengenezo ya vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji ndio yanayoichelewesha Simba kuhamia Bunju
Lakini mpaka mwisho wa mwezi huu Simba itaanza rasmi kutumia uwanja wake na kuepukana na gharama za viwanja vya kukodi

Aidha ujenzi wa uwanja wa nyasi bandia unaendelea ambapo baada ya matengenezo ya awali, zoezi la kutandika nyasi ndio linalofuata

Hii ndio Simba ambayo wengi walikuwa wakiisubiri kwa hamu

Kwani lilikuwa jambo la aibu kwa klabu kongwe kama Simba kutokuwa na uwanja hata wa mazoezi

Baada ya kukamilika awamu ya kwanza, awamu ya pili itawashirikisha Wanasimba wote ambapo ujenzi wa majukwaa pamoja na miundombinu mingine utafanyika
Lengo likiwa kuhakikisha uwanja huo unaweza kubeba kuanzia mashabiki 10,000 na kuendelea

View attachment 1226128
Tuusubili kwa hamu
 
Hivi sasa haujageuka kichaka cha chatu na kenge kweli🤣
 
Back
Top Bottom