Uwanja wa Sokoine Mbeya Ufungiwe, haufai kuchezea soka

Uwanja wa Sokoine Mbeya Ufungiwe, haufai kuchezea soka

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kila anayeangalia soka inayochezwa kwenye uwanja huo aweza kuwa shahidi, hata mvua isiponyesha soka halichezeki, unaweza kudhani ni njia ya ng'ombe, Kwetu Kyela njia ya ng'ombe ina jina lake, inaitwa IGULUMBILO, unaweza kudhani ni barabara, ila hakuna gari linaloweza kupita.

Kinachofichwa ni namna uwanja huu ulivyoharibika, Tulia Ackson na CCM Mbeya Mjini ndio waliharibu uwanja huu kutokana na mipango yao ya kampeni za Uchaguzi, Waliweka katikati ya Pichi kigodolo cha Singeli Usiku kucha.

Tangu wakati ule uwanja ule haufai kwa soka, ni Vema TFF ikatoa tamko la kuufungia bila kujali vyeo vya aliyeuharibu.

Naomba kuwasilisha.
 
Kila anayeangalia soka inayochezwa kwenye uwanja huo aweza kuwa shahidi , hata mvua isiponyesha soka halichezeki , unaweza kudhani ni njia ya ng'ombe , Kwetu Kyela njia ya ng''ombe ina jina lake , inaitwa IGULUMBILO , unaweza kudhani ni barabara , ila hakuna gari linaloweza kupita...
Kwa kweli ule siyo uwanja bali ni mahali pa kulala mbuzi!
 
Hata mimi nimekuja na uzi humu kuhusu huu uwanja! Lakini TFF na Bodi ua Ligi wameweka pamba masikioni.

Ule uwanja pichi yake inafaa kuwa shamba la mpunga! Na siyo kuchezea mpira.
 
Back
Top Bottom